Mgombea mwenza kumwangusha Magufuli

Mgombea mwenza kumwangusha Magufuli

a4apple

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
927
Reaction score
1,143
Kuna sababu 3 zitakazopelekea CCM ianguke kwa kuwa na mgombea mwenza mwanamke:

1. Mfumo dume bado una nguvu katika makabila mengi hususani vijijini. Wananchi wengi hawaamini kama wanaweza kuongozwa na rais mwanamke hivyo kumnyima kura.

2. Kushindwa kwa Bi.Anne Makinda katika kulisimamia bunge lililopita ambalo lilitawaliwa na ubabe na kubebwa CCM. Ni katika bunge hili wananchi wameshuhudia sheria mbalimbali za hovyo zikipitishwa kibabe na serikali chini ya ulinzi mkali wa spika Anne.

3. Mgombea mwenza ndiye alikuwa makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba; chini ya usimamizi wake tulishuhudia kanuni zikivunjwa ili kuichakachua katiba ya wananchi.

Ni katika kipindi hicho tulishuhudia matusi, kejeli, na vitimbi kutoka kwa wajumbe, huku wakitetewa na uongozi wao. Na kutokana na uchakachuaji huo ndipo ukawa ilizaliwa rasmi chini ya mgombea huyu.

Leo hii anaenda kwa wananchi waliotoa maoni ya katiba kutaka achaguliwe urais...ccm na Magufuli mnalo mwaka huu.
 
Tatizo la ccm mwaka huu wagombea wao wa nafasi ya urais ni kama walikuwa wanajaribu bahati yao tu
Nina uhakika wote hawakuwa wamejiandaa kabisa yule mama ndo kabisa yani basi kwa kuwa yashamwagika
hamna jinsi na kinachofanyika ni kumlipa fadhila mwenyekiti tu ili kuondoa aibu tu
Dahh...jk anavyohahaa...
 
Kuna sababu 3 zitakazopelekea CCM ianguke kwa kuwa na mgombea mwenza mwanamke:
1. Mfumo dume bado una nguvu katika makabila mengi hususani vijijini. Wananchi wengi hawaamini kama wanaweza kuongozwa na rais mwanamke hivyo kumnyima kura.
2. Kushindwa kwa Bi.Anne Makinda katika kulisimamia bunge lililopita ambalo lilitawaliwa na ubabe na kubebwa CCM. Ni katika bunge hili wananchi wameshuhudia sheria mbalimbali za hovyo zikipitishwa kibabe na serikali chini ya ulinzi mkali wa spika Anne.
3. Mgombea mwenza ndiye alikuwa makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba; chini ya usimamizi wake tulishuhudia kanuni zikivunjwa ili kuichakachua katiba ya wananchi. Ni katika kipindi hicho tulishuhudia matusi, kejeli, na vitimbi kutoka kwa wajumbe, huku wakitetewa na uongozi wao. Na kutokana na uchakachuaji huo ndipo ukawa ilizaliwa rasmi chini ya mgombea huyu. Leo hii anaenda kwa wananchi waliotoa maoni ya katiba kutaka achaguliwe urais...ccm na magufuli mnalo mwaka huu...

Husinge yastua ma ccm
 
Huyo mama ZANZIBAR hawataki ata kumsikia

Nitawashangaa sana wazanzibar kama watampa kura huyu mama na kuzima ndoto ya wazanzibar ya kujipatia mamlaka kamili ndani ya muungano. Ndiye amezima ndoto za wazanzibar, ni fursa nzuri wazanzibar kuonyesha hasira zenu maana kinachofanyika huyu anataka kuzawadiwa kwa kuwasaliti maoni yenu leo eti awe makamu wa rais. Mkimchagua mtakuwa mmezika ndoto ya zanzibar kujipatia mamlaka na mtabakia mkilalamika
 
Huwa nashuindwa kuelewa ni kigezo gani kilitumika kumpatia huyu mama nafasi ya mgombea mwenza wa CCM Samia Salihu. Mama huyu nasindwa kuelewa anachokiongea pale anapopewa nafasi. Kama ukimtazama kwa makini utagundua ni mtu aliyezoea mipasho namajungu vibarazani. Hana staha katika uongeaji. Anapenda sana vijembe visivyo na maana. Watanzania wanataka uwaambie utawafanyia nini na sio kuwapa mipasho na vijembe vya Lowassa. Laana ya Jaji Ramadhani kumfukua kule alipo na kumpelekesha achukue fomu ya kugombea ili apewe urais au umakamu na kumtupa mbali itawatafuna mpaka kufa. Sijajua ni kwa nini walimchinja huyu mzee na kumpa huyu mama. Kikwete dhambi hii itakutafuna.
Tusubiri.

Shost.
 
Ninadhani ni uwezo wake wa kufuata maagizo ya Mafisadi kama alivyofuata na kufanikisha uchakachuaji wa rasimu ya judge Warioba na kura za mashetani kupigia kura katiba ya ccm upande wa zanzibar.
 
Back
Top Bottom