Mgombea ambaye atalifanya taifa hili lijitegemee ndio mgombea wangu

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Kwanini ni muhimu kwa taifa kujitegemea na ina maana gani taifa kujitegemea ?. Hili ni swalii muhimu kujiuliza kama taifa. Je ni jambo lenye thamani kwetu ama hapana?. Siku za hivi karibuni jamii yetu pamoja na viongozi wetu wamelitupa pembeni hili jambo. Ambalo ni muhimu sana kwa uhuru wetu.

Ni muhimu kujua kujitegemea kunaanza katika fikra. Hili ni jambo la msingi sana bila kujitegemea kifikra kujitegemea kwingine ni kugumu mno. Kwahiyo hatua ya kwanza kwa taifa hili kuendelea ni kwa watu wetu kujitegemea kifikra. Hatua ya pili ni kufanya kazi. Ukiwa unazoea kuletewa kamwe hautaweza kujitegemea. Na kama hautoweza kujitegemea kujitawala kwako itakuwa ngumu.

Kujitegemea ina maana ya kwamba unajitawala na unakuwa na uwezo wa kuzalisha na kutosheleza mahitaji yako bila kuhitaji mtu mwingine hatua ya kwanza ya huku kujitegemea ni fikra, ni kujikomboa kifikra. Kujiita unajitawala wakati bado ni tegemezi ni kutokuwa na ufahamu wa kutosha. Kama huwezi kufanya chochote mwenyewe hujajitawala. Kama budget yako iwe nyumbani kwako au katika serikali inategemea watu wa nje bado hujajitawala unatawaliwa. Watu wanaokufadhili wana nguvu dhidi yako. Kujitegemea maana yake ni kuwa na nguvu ya kufanya mambo yako mwenyewe bila kuhitaji nguvu kutoka nje.

Angalia mfano wa vikinda vya ndege vinavyopanua na kulishwa na mama yao huo ndio mfano wa mtu au nchi ambayo haijajitegemea na inahitaji misaada kujiendesha. Vikinda vya ndege havijiwezi kiakili wala kimwili ndio maana vinasaidiwa. Lakini kuendelea kusaidiwa hadi unapokuwa mkubwa ni ugonjwa. Nchi yetu tuko na uhuru kwa miaka hamsini sasa miaka hii ni umri wa mtu mzima. Kuendelea kutegemea wafadhili ni ulemavu kama vile ambavyo mtu mzima anayepaswa kujitegemea kuendelea kuwalilia wazazi kwa mahitaji yake. Vikinda vinapokua na kupata mbawa hujitegemea na kuruka angani kutafuta chakula hawategemei tena wazazi wao. Huu ugonjwa tulio nao ni mbaya sana haufai kwa taifa letu unapaswa kupingwa kwa nguvu zote. Ni lazima tuwa inspire watu wetu kufanya kazi ili tujitegemee. Ili tuweze kuendesha mambo yetu vyema ni lazima tufikiri na ni lazima tufanye kazi. Hatuwezi kuwa sovereign country kama tunategemea wafadhili. Malengo yetu kama taifa iwe ni lazima tujitegemee katika kila nyanja na hili linawezekana kama tukijipanga. Ni lazima tuzalishe mali zetu wenyewe. Iwe silaha au kitu kingine chochote kile na asilimia kidogo sana vinunuliwe. Tunaweza hili kama tutawekeza akili zetu na nguvu zetu.

Leo Jioni nimesikia mgombea wa uraisi kupitia CCM ndugu magufuri akiongea alinishangaza sana kwa fikra alizonazo. Yeye ni daktari mimi sio daktari. Kauli aliyotoa alinisikitisha sana. Nilifikiri angekuwa na fikra nzuri kwasababu ameenda shule. Angekuwa na mtizamo tofauti na chanya kwa taifa hili. Lakini alionyesha udhaifu wa fikra. Na kwa jambo hili elimu yake ameitia mashaka . Mtu mwenye elimu lazima awe na uwezo wa kuchanganua mambo na kufanya chaguzi zenye manufaa iwe kwake au kwa taifa. Kwa jambo hili ilikuwa ni kwa taifa. Kwahiyo ilimbidi kufikiri sawasawa kwasababu maamuzi atakayofanya yataathiri taifa kwa ujumla. Ndugu magufuri anataka kulilemaza taifa.

Alisema nini ndugu yetu magufuri? Ndugu yetu magufuri anatuambia ; tuichague CCM kwasababu wafadhili wanaiamini bado. hii kauli ina maana gani? Namuomba magufuri atuambie! Anataka kuendelea kulifanya taifa hili zezeta linaloendelea kutegemea misaada kila siku na lisilo jiweza? Mimi nilifikiri atakuja na mipango ya kufanya taifa hili lijitegemee. Angekuja na mipango hiyo ningemsupport kama mgombea bora wa kizazi hiki. Hana mipango hiyo ni wale wale wanaodumaza taifa hili linalohitaji ukombozi. Tunahitaji taifa letu na watu wetu wajitegemee. Mgombea ambaye atahubiri kulifanya taifa hili lijetegemee ni mgombea wangu na sijaona miongoni mwa waliopo.

Pamoja na kwamba tunahitajika kwa dhati kabisa kudhibiti rushwa na ufisadi, bado tunawajibika kulifanya taifa hili liwe la kujitegemea. Uwezo huo tunao. Ni muhimu kujenga elimu yetu kuwa bora. Kujenga uzalendo na kujitambua watu wetu kwa taifa lao. Kujenga utaifa na kujitambua ni jambo muhi
 
Back
Top Bottom