Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,777
Wakati watiania wanane wa ubunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Kibamba wakiendelea kunadi sera zao, ameibuka mtiania Alphonce Temba aliyeahidi kuwapeleka wajumbe Afrika Kusini kwa ajili ya kujifunza masuala ya bima ya kifo.
Amesema wataenda kupata elimu ya bima ya kifo itakayosaidia watu kuondokana na changamoto ya kuzuia maiti kwa kukosa fedha.
"Ninao mkakati wa kuja na bima ya kifo nitaondoka na wajumbe mmoja mmoja kila kata twende Afrika Kusini wakajifunze waione kama inafaa tuje tuitambulishe hapa ili iiwasaidie wanaopata vifo vya ghafla na hawana uwezo wa kumudu gharama" amesema Temba.
"Nikipatiwa nafasi nikawa Mbunge mwaka 2027 na 2030 hatukaa hapa tukaa kwenye hoteli nzuri yenye kuyoyozi," amesema Temba.
Watia nia wengine wanaoendelea kuzunguka katika kata za Goba, Mbezi na Saranga, ni Angellah Kairuki, Issa Mtemvu, Nestory Yamungu, Angelo Nyonyi, Joseph Chikongoye, Consolatha Rwiza na Mwamini Mbwambo.
Watiania hao wameahidi kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa Kibamba ikiwemo, ardhi, eneo la maziko, shule, maji, mazingira, soko na huduma za afya. Imeandikwa na Mintanga Hunda. Video na Sute Kamwelwe.