Mgogoro wa Ziwa Nyasa Tz tunaweza kufanya kile Iran alichokifanya dhidi ya Azerbaijan

Hata mimi nadhani kichapo ndo dawa ya huyu MSAGAJI binti Banda, ni bora kufa kishujaa kuliko kuishi kwa fedheha. Ni bora wakatushinda vitani kuliko kuwapa sehemu ya nchi yetu mezani. Tuwachapeni tuu hawa wamalawi watie adabu. Kama hawataki kuzungumzia mpaka wa katikati ya ziwa ina maana wanataka tuwaachie ziwa loote, kitu ambacho Tanzania haijawahi kukifikiria. Wanajeshi tujiandaeni tumchape huyu msagaji, kesharuhusu mahusiano ya jinsia moja kinyume na tamaduni za kiafrika hana maana na si ajabu hata akili yake imeshaharibika.
 
Nilishasema tangu awali dawa ni kichapo mazungumzo baadae. Ni falsafa ya Wachaga kuhusu vihamba! unasogeza mpaka nusu mita tu waweza kuishia kuzikwa! Malawi wanapima maji na sisi twasema diplomasia, diplomasia gani wakati tangu awali tunavua, tunakunywa, tunasafiri humohumo ziwani? Kwani Msumbiji wao mpaka wao umepita wapi? Viongozi changamkeni wananchi tunachokozwa.
 
Yafaa pia askari wetu wawe tayari kwa lolote. Iwapo Wamalawi watapeleka ndege zao za utafiti katika eneo letu. Tunakila sababu ya kuwapiga. Ni undawazimu kudai kuwa ziwa lote ni la malawi wakati ziwa hilo watu wote walipewa na mungu.

askari gani?
askari wote wapo busy na kuzuia maandamano ya chadema tu...
 
RPC wa mwanza amefariki kwakupigwa na watu wanaoaminiwa na serikali ya ccm kuwa ni majambazi, kama tunashindwa kulinda viongozi wetu je mipaka ya nchi itakuwaje?
 
Yericko-Nyerere

Halitakuwa jambo zuri kwa nchi yetu kutumia mabavu kwa sababu kadhaa; mojawapo ikiwa ni kutokana na ukweli kuwa watanzaia leo hatuna utaifa tena kama ilivyokuwa wakati wa uvamizi wa Amin. Jambo la pili ambalo ni la mhimu zaidi ni kuwa kufanya hivyo kutasababisha sisi majirani tuwe wagumu kukubaliana mambo yanayotuhusu. Kwa Malawi kuacha kujenga ujirani mwema kwa kutegemea kuwa Uingereza na Marekani watakuwa upande wao kwa sababu ya mafuta wakati hawajajua kama kweli mafuta hayo yapo ni aibu sana kwetu waafrika.

Sisi tuendelee na njia zote za kidemokrasia ikiwamu umoja wa mataifa kama alivyofanya Membe na Kikwete wakati wa mkutano wa viongozi wa dunia mwaka huu.
 
Hili jambo bila mahakama ya kimataifa halitaisha.

Mkuu, itakula kwetu tukienda ICJ. JK anasema mkataba wa Heligoland una makosa. Lakini mkataba huo hata AU inautambua kikao chake cha mwaka 2007

Ninachokiona ni kwamba ziwa ni la Wamalawi. Ujerumani haikuwa na mpango wa maziwa. Ujerumani ilikuwa na meli 1 tu wakati Ureno ina 2 na Uingereza ilikuwa na 19 humo kwenye ziwa Nyasa

MBAYA ZAIDI mwaka 1898 kulikuwa na JOINT BOUNDARY COMMISSION ilihakiki mpaka wa Tanzania, Zambia na Malawi. Ujerumani ikaja kusaini mwaka 1901

Nimesoma Nyasaland colonial report ya mwaka 1920 inasema Malawi ipo kati ya longitude E33 na 36, pia Latitude S9 45' na 17 16'. Kwahiyo yale madai Wamalawi walibadili mpaka miaka ya 1950 tutupie mbali
 
Mkuu, itakula kwetu tukienda ICJ. JK anasema mkataba wa Heligoland una makosa. Lakini mkataba huo hata AU inautambua kikao chake cha mwaka 2007

Ninachokiona ni kwamba ziwa ni la Wamalawi. Ujerumani haikuwa na mpango wa maziwa. Ujerumani ilikuwa na meli 1 tu wakati Ureno ina 2 na Uingereza ilikuwa na 19 humo kwenye ziwa Nyasa

MBAYA ZAIDI mwaka 1898 kulikuwa na JOINT BOUNDARY COMMISSION ilihakiki mpaka wa Tanzania, Zambia na Malawi. Ujerumani ikaja kusaini mwaka 1901

Nimesoma Nyasaland colonial report ya mwaka 1920 inasema Malawi ipo kati ya longitude E33 na 36, pia Latitude S9 45' na 17 16'. Kwahiyo yale madai Wamalawi walibadili mpaka miaka ya 1950 tutupie mbali

Tujiandae vema kabisa na hoja zetu, lakini tusikwepe kwenda Mahakama ya kimataifa. Iwapo Mahakama ya kimataifa itaamua ziwa lote ni la Malawi - itabidi tukubali matokeo.
 
Am not sure ata kama TZ tuna hizo fast attacking boats to deploy on lake nyasa...leo nimeshuhudia UGANDA kwenye sherehe zao za uhuru jinsi walivyo display different type of jet fighter tena za kisasa nilichopenda zaidi ni military helicopter za aina km 3 na zingine zikiwa ni attack copters...Always hua naona helicopter moja ya police yenye two blade sasa sijui tunawezaje vipi kujidefende ktk mipaka yetu..IRAN is another story kwani ktk military power imo na hiyo caspian lake is owned by Russia,Azebaijan na IRAN lakini waliweza kusimama kidete dhidi ya hayo makampuni na kikaeleweka

Unaijua nguvu ya Tanzania wewe? Hata Banda analijua hilo ndo maana haongei/kutoa tamko lolote bila kuwasiliana na wanaomtuma.
 
Hawa wamalawi dawa yao ni kuwashikisha adabu tu, wakithubutu kupitisha ndege zao ama manowari zao katika eneo la nchi yetu washughulikiwe kisawasawa.

Hata kama wamarekani na waingereza ndio wako nyuma yao lakini hatuwezi kuruhusu ardhi yetu ichukuliwe kienyeji kiasi hicho.


tatizo siyo tu kutokufannya exploration ndani mpaka wetu, bali kuna tatizo hata tukibaki na eneo letu na wao wakiendelea na zoezi lao ndani ya mipaka yao, hiyo gas ipo ndani ya ziwa lote yaani upande wao na wetu (kimantiki watakua wanaiba na gas yetu pia kwa sababu itakua inaflow upande wao) hii moja na kingine upande wetu utaathirika na hizi shughuli kimazingira hata kama hao waingereza watadai wana teknolojia nzuri ya kuchimba hiyo gas bila ya kuvuruga mazingira. Kuna kelele, disruption of fishing routes etc ambayo itawaathiri wakazi wa eneo letu wasiopata faida yeyote ya hiyo gas. Kwa hiyo hata mipaka ikibaki kama ilivyo sasa (bila malawi kudai ziwa lote) bado hili zoezi linahitaji mazungumzo ya ujirani mwema na makubaliano kwa sababu ya athari zake kwa watu wetu.

suluhisho hapa ni maamuzi magumu sana.
 
Back
Top Bottom