Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,695
- 149,921
Mgogoro wa Zanzibar ukiwa handled vibaya bila kujali au kuheshima matakwa ya wazanzibari, mgogoro huu unaweza kuwafanya wazanzibari (ukiaacha viongozi wachache wa chama fulani) wakashikamana na hata kuibuka na madai mapya ya kudai kura ya maoni kuamua kama Zanzibar iendelee kuwa sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania au laa.
Busara ikikosekana miongoni mwa viongozi wetu,mivutano ya kisiasa yenye mweelekeo wa ubara na utanganyika inaweza kuja kuibuka na kushamiri siku za usoni na baada ya miaka miwili au mitatu ijayo,tunaweza kujikuta tuko katika mgogoro mwingine kabisa na ambao utakuwa mkubwa zaidi ya huu wa leo.
Matatizo ya muungano hayapo tu katika makaratasi,bali yapo hata kwenye mioyo ya watu hivyo mgogoro huu unaweza kuwa ni sawa kumwagia petroli kwenye moto unaofuka moshi.
Mgogoro wa Zanzibar kwa sasa unaweza kuonekana kama ni mgogoro wa Zanzibar tu ila mambo ya kiharibika,utakuwa ni mgogoro wa muungano na utagusa katiba yetu na majina yafuatayo ambayo uwepo wake kunategemea uwepo wa muunganano.
Tanzania:Hakuna Tanzania bila Zanzibar
CCM:Hakuna kitakachoitwa CCM bila Zanzibar bali tutakuwa na TANU au vinginevyo.
CUF:Hakuna kitakachoitwa CUF bila Zanzibar
CHADEMA:Hakuna kitachojulikana kama CHADEMA bila Zanzibar, n.k.
Mliopewa dhamana ni wakati wenu sasa wa kuamua muingie katika historia ya aina gani ambayo vizazi na vizazi vijavvyo vitakuja kuisoma kama sio kufundishwa.
Time will tell.