Mgogoro wa wakulima na wafugaji Manga,Tanga: Rais Magufuli atoa wiki 1 Hakimu Laizer awe amehamishwa kituo cha kazi

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,513

Rais Magufuli amesema changamoto zipo na atazitatua, Rais ameahidi kuwa zile wilaya mkinga, Bumbuli lushoto, Kilindi ambazo hakupitia atazipitia.

Amesema pia umeme utaletwa katika awamu ya tatu, Rais ameongea mkulima mama huyo anasema mipaka inawasumbua.

Pia ameongea na mfugaji amesema kuwa wapo muda mrefu na hakuna malalamiko yoyote na amesema hawana kesi na wakulima.

Ameongea na Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe amesema kesi zikienda mahakamani hakuna ushahidi, Mahakama ya Mwanzo kuna Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Mazingara anaitwa Laizer anasumbua sana kesi za wafugaji ndio wanashinda ndio maana wakulima wanalalamika.

Rais Magufuli amesema kuwa wafugaji kwasababu wana pesa wamekuwa wanahonga viongozi, awaomba wafugaji wasilishe mashamba ya wakulima, na wasinyanyase wakulima, na amewaambiwa wakulima wasionee wafugaji.

Pia amewaambia RCO na TAKUKURU wawachunguze viongozi.

Rais Magufuli amempa hakimu Laizer wiki moja awe amehamishwa kituo cha kazi.

Rais awashukuru viongozi wa mkoa, waheshimiwa mkuu wa mkoa mbunge , pia amewashukuru wana Manga kwa kumchagua na amemaliza ziara yake ya mkoa wa Tanga
 
Punguza ngenga kijana. Mgogoro wa wakulima na wafugaji ni janga la Taifa. Rais anapigilia msumari tu na kuwakumbusha wenye mamlaka.

Hakupaswa kutoa order kwa muhimili mwingine unaojitegemea.Hawezi kujua kwanini kesi hiyo imechelewa,inawezekana watendaji wake pia ndiyo wenye matatizo na siyo Hakimu.

Alitakiwa asitoe tamko bila ya kumuhisha Kaimu Jaji,kwamba nimepata malalamiko haya hebu fuatilia nini tatizo.

Uongozi bila HEKIMA na BUSARA ni sawa na kusonga Ugali bila maji na moto
 
Safi sana kuna wengi tu inabidi wahamishwe vituo na kuchunguzwa kwa rushwa.
 
Hakupaswa kutoa order kwa muhimili mwingine unaojitegemea.Hawezi kujua kwanini kesi hiyo imechelewa,inawezekana watendaji wake pia ndiyo wenye matatizo na siyo Hakimu.

Alitakiwa asitoe tamko bila ya kumuhisha Kaimu Jaji,kwamba nimepata malalamiko haya hebu fuatilia nini tatizo.

Uongozi bila HEKIMA na BUSARA ni sawa na kusonga Ugali bila maji na moto
Kalia ujinga wa kukariri tu !
 
Rais Magufuli azungumza na wakulima na wafugaji, awaomba wafugaji wasilishe mazao ya wakulima, na wakulima wasionee wafugaji, amewaambia TAKUKURU wawachunguze viongozi.

Pia amempa hakimu huyo wiki moja awe amehamishwa kituo cha kazi.

Sitasahau siku niliposhuhudia wafugaji na silaha zao za jadi wakilisha mifugo kwenye shamba la Mkulima Kilosa, maskini mwenye shamba na mkewe wakitazama kwa masikitiko tuu. Wafugaji wana roho mbaya, pia wanahonga Watendaji (VEOs, WEOs) . Ni njia ya Lumbiji, dhuluma!! Sasa ikome !!
 
Sio mahakimu tu, watendaji na polisi kwenye hii migogoro ya wakulima na wafugaji ndio wanaifanya iendendee kwani wanachukua fedha nyingi kwa wafugaji na kuwakandamiza wakulima na ndio maana wana viburi sana kwani fedha wanayo ya kuwahonga hawa wala rushwa!
 
Hakupaswa kutoa order kwa muhimili mwingine unaojitegemea.Hawezi kujua kwanini kesi hiyo imechelewa,inawezekana watendaji wake pia ndiyo wenye matatizo na siyo Hakimu.

Alitakiwa asitoe tamko bila ya kumuhisha Kaimu Jaji,kwamba nimepata malalamiko haya hebu fuatilia nini tatizo.

Uongozi bila HEKIMA na BUSARA ni sawa na kusonga Ugali bila maji na moto
Umejiuliza in kwa kwa nini katoa agizo hilo hapo?

Vijana jueni Rais ni taasisi na anatumia mamlaka yake. Acheni wivu 2020 nawe gombea ushinde utoe matamko yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tatizo hawa mahakimu wanakaa muda mrefu sana eneo moja hadi wanazoeleka jambo linalo pelekea kupoteza sifa za kuwatendea haki wananchi.

kutokana na jinsi hiyo ilivyo ni busara mahakimu wawe wanahamishwa angalau kila baada ya miaka mitatu(3) na sio kama ilivyo sasa, wanakaa muda mrefu sana eneo moja hivyo wanakuwa chanzo cha migogoro.

ukifanya tathimini ktk miji mikuu kama Dsm, mwanza, arusha, tanga nk utakuta mahakimu wamekaa zaidi hata ya miaka 10 hii sio sawa ktk jukumu la utoaji haki!

mhe Rais ametoa tu mfano wa eneo moja lkn kuna haja ya kuchukua hatua kwa nchi nzima ili kuboresha upatikanaji wa haki kwa wananchi.
 
Kalia ujinga wa kukariri tu !

Ndiyo sababu JPM amewatukana mawaziri wake sababu ya kupiga makofi bila kuchukua hatua stahiki kumbe watu wenyewe wanamawazo kama yako kila kitu ndiyo hata akinya barabarani utapiga makofi
 
Hakupaswa kutoa order kwa muhimili mwingine unaojitegemea.Hawezi kujua kwanini kesi hiyo imechelewa,inawezekana watendaji wake pia ndiyo wenye matatizo na siyo Hakimu.

Alitakiwa asitoe tamko bila ya kumuhisha Kaimu Jaji,kwamba nimepata malalamiko haya hebu fuatilia nini tatizo.

Uongozi bila HEKIMA na BUSARA ni sawa na kusonga Ugali bila maji na moto
Sasa kesha sema tengua wewe basi aliyosema.
 
Back
Top Bottom