Mgogoro wa njia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgogoro wa njia

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by malsa, Mar 3, 2012.

 1. m

  malsa Member

  #1
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wadau,
  Naombeni msaada kwenye hili.
  Mimi naishi maeneo ya uswahilini ambako hakujapimwa.Jirani yangu ana mnazi ambao upo barabarani kabisa na njia ambayo ndo mimi napita na gari kuingia ndani kwangu.Gari yangu inapita kwa shida sana yaani nikifika hapo kwenye huo mti inabidi niwe makini kuilengesha gari ili nisiguse huo mti. Huyo jirani tumemuomba mara nyingi aukate huo mti na tuta mfidia lakini jibu lake ni kwamba ataukata siku anayotaka yeye kujenga lakini sio leo,toka mwaka 2010 hilo jibu ndo aliliolitoa.Kujenga hajengi na mti haukati. Nipeni mawazo wadau,je kuna sheria yoyote inayoweza kunisaidia kupata hiyo njia wakti eneo ni lake,na njia yenyewe inaenda kwenye nyumba kama tatu hivi.

  Halfu kibaya zaidi huyo mzee mwenye huo mti ni mjumbe wa nyumba kumi kumi na pia ni mjumbe wa baraza la ardhi la kata.

  Nipeni ushauri wa kisheria wadau cse mm naamini no one is able the law kma sheria ipo.
   
 2. Caren

  Caren JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Nenda baraza la kata fungua kesi ya kuomba access. sheria ya ardhi ya mwaka 1999 inakuruhusu. Ila kwa ushauri kwa kuwa una gari lazima una kipato cha kuridhisha. Acha ubahili. Tafuta elfu 20 uende kwa wakili uombe ushauri wa kisheria na utapewa. Nahisi ubahili wako umekufanya ukae toka 2010 wakati suluhisho lake ungelipata within 1 week. Watanzania tubadilike jamani.
   
Loading...