Hali ya huduma za Afya kwa kweli inazidi kuwa mbaya wakati ambao watu toka kila upande wameweza kutoa maoni yao bila mafanikio. Kwa kuwa Serikali imeweka wazi uamuzi wake ambao haujaweza kubadili msimamo wa wataalamu hawa muhimu naona tumefikia mahali pa kushindana nguvu. Swali la msingi kujiuliza ni, Je hali hii itaendelea mpaka lini.
Kwa mchango huu naona kwamba kwa kuwa makundi haya mawili yote yameshindwa kufikia mwafaka kinachohitajika ni kuwa na mpango wa usuluhishi. Kama watu waungwana, nafikiri tufike mahali tukubali ya kuwa maoni yetu yameshatolewa na tuanze kutafuta ufumbuzi wa kweli. Pendekezo la Muhimu ni kuwa tunahitaji neutral body itakayotafuta namna ya kusuluhisha makundi hayo mawili. Tunaomba taasisi au kundi litakalochukua mtizomo wa kati kuandaa mazingira yatakayowezesha pande hizi mbili kukutana ili kuweza kufikia mwafaka.
Vyama vya kijamii, wateteaji wa haki, taasisi za usuluhisi nk. tunaomba mtafute njia ya busara na kuweza kuwakutanisha wahusika hawa wawili.
Nawasilisha.