Queen Esther
JF-Expert Member
- Apr 5, 2012
- 2,195
- 1,417
Wanajamii ma great thinker yangu ni machache. Leo nimewakuta watoto wangu na marafiki zao wakizungumza suala la kusoma PCB combination kubwa wanaochukua madaktari watarajiwa. Hofu imewashika hawaoni kama PCB inalipa baadae. Nawaomba wazazi wenzangu mchunguze athari ya mgogoro huu na hatua stahiki zichukuliwe mapema. Wale wenzetu mnaofanya tafiti liangalieni suala hili mwaka huu iwapo wanafunzi wa PCB wataongezeka au la. Pia athari hii inaweza kuwa kubwa baadae tusipokuwa waangalifu. Kaeni na watoto mjue mawazo yao ukizingatia masomo yenyewe ni ya muda mrefu, post graduate yake pia muda mrefu, shuluba nyingi nk. Mwisho watu wa HAKI ELIMU na wengine wenye mapenzi mema na TZ anzeni kutoa matangazo ya kusafisha hali ya hewa.