Mgogoro wa kisheria Tz bara na Tz visiwani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgogoro wa kisheria Tz bara na Tz visiwani

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Goheki, Sep 19, 2011.

 1. Goheki

  Goheki JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 270
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Katiba inatamka Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar,cha ajabu kuna mamlaka zinaitwa za Tanzania na wakati huo huo,Tz visiwani nao wanaanzisha mamlaka hiyo hiyo,ila kwa jina la Zanzibar,kwa tuna kituo cha uwekezaji (TIC)visiwani wana cha kwao pia,hii imekaaje?
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Sep 19, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Umewahi kusikia nchi zifuatazo:
  • Tanzania
  • Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
  • Tanzania Bara
  • Tanzania visiwani
  • Tanzania Zanzibar
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Pasi na shaka wewe ni mbumbumbu wa sheria za nchi yako.

  Kwa kukujuza muungano wa Tanganyika na Znz ni wa KIMKATABA NA WALA SI WA KISHERIA. Kuna mambo ambayo mkataba huo umeyabainisha kuwa ni hayo tu ndio ya muungano na mengine yanakuwa nje ya muungano.

  nakupa homnework fuatilia hayo makubaliano ya muungano baina ya Tng na Znz utajua mengi.

  Kila la kheir
   
 4. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hapo hakuna mgongano maana kuna mambo ya Muungano na mengine siyo ya Muungano, Mgogoro uliopo ni suala la marekebisho ya katiba ya Zanzibar ya 2010, kwani wao wameweka makamu wawili wa rais na kumuondoa waziri kiongozi wakati katiba ya JMT bado inamtambua waziri kiongozi na haiwatambui hao makamu wawili
   
 5. Goheki

  Goheki JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 270
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  <br />
  <br />
  Hayo ni mawazo
   
 6. H

  HAKI bin AMANI Senior Member

  #6
  Sep 19, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye red ndiyo sahihi kwa uelewa wangu, ingawa huandikwa na kutamkwa JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. Ukisema Jamhuri ya Muungano 'wa' Tanzania, je Tanzania wameungana na nani. Kwa sababu jina TANZANIA, tayari ni Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar. Kwa hiyo ni Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na siyo wa Tanzania. Ni mawazo yangu tu.
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,067
  Trophy Points: 280
  Inawezekana hata mimi mbumbumbu pia....unaposema muungano sio wa kisheria unataka kusema nini hasa?
   
Loading...