Mgogoro wa kisaikolojia na baba

Pole sana aisee. Hata mm nlitaka nikwambie umuulize mama Yako atakua anajua but bora ulifanya hivyo. Kikubwa mzee ameathirika kisaikolojia hivyo msamehe Bado ni mlezi wako.

Sasa we mvumilie tu kuna siku tataisha na atakuthamini na kukuomba msamaha. Mtendee hisani yake kama mlezi wala usimchukie ILA jaribu kumuepuka pindi akiwa na hasira
 
Vipi mkuu kama hao watu walioana iwapo mke alishazaa?
 

Usaliti unauma ndugu na hamna wa kuadhibiwa kwa usaliti zaidi ya yule aliyekusaliti(mwanamke) usimuadhibu mwingine yeyote wala usijiadhibu wewe. Kumbuka mwanamke sio ndugu Ni rafiki tu na kama ujuavyo undugu haufi ila urafiki unakwisha kwa hiyo ukioa ujue kuna kuacha.
 
Nmepapenda hapo mwishoni kwenye NOTE
 
Umshukuru sana mama yako aliyekupa ukweli;
mzee wako ana makosa hakupaswa kukufanyia hivyo;
mzee ni mkatili sana angeweza hata kukuulia mbali, kaa naye vizuri.
sasa umeshakuwa mtu mzima, jitahidi kuendelea kumpa heshima na mahitaji yake kama kawaida;
 
mbona umeya quote maneno hayo machache
 
Mkuu asante nawe kuliona hilo ...Lugha ya staha imekosekana hapo!
samahani mkuu sikujua kuwa nitawakwaza. Ni kutokana Na mapito tuliyopitia wakati mwingine story Kama hizi zinaturudisha nyuma kihisia
 
ondoka hapo nyumbani . ila usiache kumuheshimu. achana nae sio kosa lake . kuchapiwa mke kunauma sana kijana. ila mama yako nae ni noma .
Inawezekana mama aliolewa wakati tayari huyu kijana keshazaliwa, siyo lazima kuwa baba alichapiwa mke!
 
mbona umeya quote maneno hayo machache
Mkuu ni Maneno Mzito sana na Umeyaongea kutoka upande wa ndani kabisa wa Nafsi yako na nilitaka Pia wafuatiliaji walione hilo kwa Undani kabisa Kuwa Mke/Mpenzi/hawala/mchepuko ni Rafiki siyo Ndugu Yako..... Na Rafiki huwa ana Mipaka Japo wao hawataki kuamini kuwa Kunapashwaa Kuwa na Mipaka kwenye Mahusiano.....
 
Heri ushamjua baba yako halisi shukuru, sio unahangaika kumtafta siku unampata mara paaaaap baba ni lemutuz na mnafanana ile mbaya, hahaaaaa my friend utajuta kudadisi
Umenichekesha mkuu japo kwenye vitu serious
 
Mama ana kosa gani?

Hivi mkuu ukikutana na mwanamke ambaye tayari ana mtoto ukakubali kumwoa na kuahidi kulea mtoto, halafu ukajenga chuki na huyo mtoto, nani atakuwa na makosa?
Umenena vema mkuu...wengi wanakurupuka na kulaumu bila kufikiri kwa kina
 
Hapo wakulaumiwa ni mama aliyechepuka (cause) hayo yanayokupata ni effect (matokeo ) tu ambayo huyo baba yako mlezi ni reactions zake kama binadamu wengine tu ambao amesingiziwa mtoto, kuanzia hapo solution ndio unaweza ukupata
Mkuu una uhakika gani kuwa alichepuka?!!
 
Kumbe jibu unalo. hapo mwenye makosa ni mama yako na ndo anatakiwa abebe lawama zako zote. Kumbe anajua baba yako siyo huyo halafu amelazimisha ukuzwe na baba mlishi. Huyo baba mpende kama baba mlezi na mlishi wako lakini mama na baba yako mzazi ndo wanatakiwa wabebe lawama ya wewe kuteseka kwa kukosa upendop wa baba.
 
Uyo baba, yako anakupend sema anashindwa kudeal na kua, wewe sio mwanae wewe ni mtoto jifunze kua understanding
 
Some people in this world doesn't deserve to be loved !!.

Mkuu km unauwezo Wa kutoka home ,embu jitenge nao kwanza ,sure utajikuta anakua MTU wakukukwamisha maishan mwako.

Nakm umeshajitegemea ,punguza ile kasiiiiiii ya kwenda kwenda om ,hakikisha wanakumis ndo unatia maguuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…