Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,372
Wadau,
Mdau wangu ambaye yupo karibu sana na Mfanyabiashara Reginald Mengi amenidokeza kuwa jana amefanya mazungumzo na mfanyabiashara huyo. Mazungumzo yao yalijikita kutathmini hatma ya wawekezaji wa ndani katika kipindi cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015. Katika mazungomzo hayo, Reginald Memgi ameonesha wasiwasi wake na hali ya mambo inavyoenda ndani ya chama tawala, CCM.
Kwamba, ndani ya chama hicho kumeibuka kundi la watu ambao wanautafuta urais kwa udi na uvumba kwa maslahi yao binafsi. Anasema kuwa lipo shinikizo kutoka kwa wafanyabiashara ambao wanageuza siasa kuwa mtaji katika biashara zao.
Mengi anaenda mbali kwa kutukumbusha Watanzania kuwa wapo wafanyabiashara ambao wamegeuka kuwa matajiri kupitia siasa. Kwamba, watu hao hawakuwa lolote kabla ya kuingia kwenye siasa ila baadaye wamegeuka kuwa wafanyabiashara wakubwa tena wakimiliki makampuni ambayo yanashinda zabuni mbalimbali kirahisi.
Reginald Mengi anatoa mfano wa Rostam Aziz. Kwamba, Rostam hakuwa maarufu kabla hajaingia kwenye siasa na kwamba ukiangalia makampuni yake karibu yote yameshiriki kuliibia taifa kwa namna moja ama nyingine hasa kupitia ukwepaji kodi na kushinda zabuni kijanja ujanja.
Reginald Mengi anakumbusha mgogoro wake na Rostam ulioibuka kama miaka minne iliyopita na kusema kwamba mgogoro huo haujamalizika isipokuwa uliahirishwa tu baada ya Rostam kuwa nje ya nchi kwa muda mrefu. Anasema kuwa hakukosea kumuita Rostam kama ni fisadi papa na kwamba amekuwa kikwazo kikubwa katika maendeleo ya nchi. Kwamba, Mengi ataendeleza mapambano yake dhidi ya Rostam.
Mengi anasema kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu, watanzania na hasa chama tawala kinapaswa kuwa macho sana na aina ya watu ambao watateuliwa kuwania nafasi mbalimbali. Anasema kuwa Edward Lowasa ni mtu ambaye wana mahusiano mazuri ila kwa mtazamo wake anasema kuwa hafai kuwa Rais wa Tanzania kutokana na tabia zake binafsi na aina ya watu waliomzunguka.
Anatolea mfano kuwa huwezi kuwa mtu safi ilhali umezungukwa na watu waliojaa madudu na uchafu wa kila aina. Kitendo cha Lowasa kumkumbatia Rostam kunaendelea kumuweka pabaya kwenye harakati zake za kwenda Ikulu.
Wadau, hakika watu wenye akili wameanza kuzinduka.