Mgogoro wa Kafulila: Ruhuza azomewa Kasulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgogoro wa Kafulila: Ruhuza azomewa Kasulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by johnmashilatu, Jan 11, 2012.

 1. j

  johnmashilatu JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 538
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  katibu mkuu wa chama cha NCCR mageuzi Bw Sam Ruhuza jana amezomewa na wakazi wa mji wa kasulu wakati alipojaribu kueleza sababu za chama hicho kumfukuza uanachama mbunge wa kigoma kusini Bw David Kafulila

  Tukio hilo limetokea jana katika stendi ya mabasi ya kasulu mjini wakati katibu mkuu huyo wa NCCR mageuzi alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara

  Bw Ruhuza alizomewa na wananchi waliohudhuria mkutano huo baada ya kuwaeleza wananchi kuwa angependa kutoaufafanuzi juu ya hatua ya chamaya kumfukuza uanachama Bw Kafulia

  wananchi hao walipiga kelele wakitaka chama kimrudishe Bw kafulila vinginevyo hawakitaki chama hicho. kelele hizo ziliendelea na bw Ruhuza alishindwa kuendelea na hotuba hali iliyomlazimu kumwomba mbunge Bi Zaitun Buyogele kuwatuliza wananchi hao


  hata hivyo Bi Buyogele alishindwa kuwatuliza wnanchi waliokuwa wakipiga kelele na kuzomea hali iliyompelekea kumwomba diwabni w akasulu mjini kupitia NCCR mageuzi Bw Issack mkewema kuwatuliza wananchi hao


  katika mkutano huo ambao mbunge wa Kasulu mjni bw Moses machali hakuhudhuria bila kutolewa sababu, wananchi waliendelea kusisitisha kuwa hwakitaki chama hicho kama hakitamrejesha Bw Kafulia
   
Loading...