Bernard bakari
JF-Expert Member
- Mar 30, 2016
- 407
- 781
Jana nilikuwa Nikimsikiliza Mheshima Maalim Seif Kupitia kipindi cha 360 Kinachorushwa Clouds Tv akihojiwa juu ya mgogoro wa Cuf. Leo pia tulikuwa na Prof Lipumba baada ya kusikiliza pande zote mbili kwa umakini sana nikagundua Tatizo la mgogoro wa Cuf Si Lipumba bali utendaji mbaya wa Maalim sief ndo umefanya Cuf Ifike mahali haitamaniki tena.
Prof Lipumba alijihudhuru tarehe 5/8/2015 nafasi yake ya Uenyekiti kwa mujibu wa katiba ya Cuf inasema kuwa mwenyekiti, makamu mwenyekiti na Katibu mkuu akijihudhuru lazima kuitishwe mkutano mkuu wapige kura ya kuridhia kujihudhuru kwake, Aliyetakiwa kuitisha kikao hicho ni Katibu mkuu wa Chama Ambaye ni Maalim seif Naye hakufanya hivyo mpk mwezi wa sita 2016 Prof alipotengua barua yake ya kujihudhuru.
Maalim Seif angeitisha kikao kwa muda mwafaka nina imani leo Prof asingekuwa na haki wala asingethubutu kurudi kama mwenyekiti ndani ya Chama Cha Wananchi CUF. Kwa maoni yangu hilo kosa la kwanza la Maalim Seif.
Pili Kwa mujibu wa Barua ya Msajiri wa Vyama vya Siasa CUF kupitia kwa katibu wake waliunda kamati ya uongozi ikiongozwa na Julius Mtatiro kimakosa na sheria inayosimamia vyama vya Siasa hairuhusu hilo. Na Msajiri alitoa angalizo hilo kwa Cuf kuwa uongozi huo ni Batili.
Jinsi nilivyofikiri mimi ni kuwa Maalif Seif anafanya kazi kimazoea bila kufata taratibu, kanuni na sheria za kuendesha vyama vya Siasa ndomana uwezekano wa kumshinda Prof ni mdogo sana sababu taratibu za kikatiba ya chama haifatwi. Tatizo hilo si la Cuf tu bali Watanzania kwa ujumla wetu tunapenda shortcut sana, tunapenda kuaminiana na kutojali taratibu. Kosa hilo lilitokea kwa Cuf iwe fundisho si kwa vyama vya siasa bali hata kwa Taasisi zingine zisizo za kisiasa na mtu mmojammoja.
Ushauri wangu kwa sasa Maalim Sief na Timu yake ya akina Julius Mtatiro, Wakae na Prof wafikie mwafaka hawana namna yeyote kuwa wanaweza mshinda Prof Lipumba Taratibu za kujihudhuru kwa mwenyekiti wa Chama hazikufuata kama sheria na taratibu zinavyotaka. Hawana budi kuungaa naye.
Kama hawamtaki Prof Lipumba njia ni mbili tu kuachia ngazi zote za uongozi na kumwachia chama au kukubali kufanya naye kazi na kusubiri uchaguzi ujao wafanye kampeni ya kumfanya asichaguliwe. CUF MNATUANGUSHA WAPI NGANGARI, KIFO CHA MENDE, CHALI, NDEMBENDEMBE. Tunataka CUF yenye umoja si CUF mbili.