Mgogoro wa ardhi wanasheria mpo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgogoro wa ardhi wanasheria mpo

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by muzachai, Nov 3, 2009.

 1. m

  muzachai Member

  #1
  Nov 3, 2009
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tembea uone , jamani dar kweli ni kubwa na mgogoro huu nimeupata sehemu fulani hebu pata mkasa ulivyo


  Mzee athumani mwinyi mvua ( sio jina halisi) aliuza shamba lake la heka mia moja kwa bwana michael ( sio jina halisi) mnamo mwaka 1989. Bwana michael akafuata taratibu zote na kulimiliki kihalali eneo hilo mwaka 1990 kwa kupata hati miliki kutoka wizara ya ardhi. Tangu anunue na kuanza kulimiliki kihalali shamba hilo bwana michael alitembelea si zaidi ya mara mbili shamba hilo akiwa na watoto wake wawili moja ana umri wa mika minne na mwingine ana umri wa miaka miwili. Mwaka 1992 alihamia marekani na kwa bahati mbaya alifariki kwa ajali ya gari na kuwaacha watoto wake pamoja na mke wake huko marekani na huo ndio ukawa mwisho wa bwana michael. Hivyo mzee Mwinyimvua ambaye alikuwa ameuza shamba akaendelea kuliangalia shamba hilo na kumweleza siri hiyo mwanae shomari. kuwa alinde shamba la watu na ikitokea watoto wa bwana michael wamerudi wapewe eneo lao. matajiri wengi walilitamani shmaba hilo na walimwendea shomari kwa ahadi lukuki ili awauzie lakini shomari alikataa. Mnamo mwaka 1999 mwenyekiti wa serikali ya mtaa na mjumbe wa eneo hilo bwana chakupewa akauza kwa siri hekari hamsini kwa bwana siyangu na kumwandikia karatasi zote mbili zenye sahihi yake na mihuri kama mjumbe na mwenyekiti wa serikali ya mtaa. mwaka 2000 mzee chakupewa akafariki. hivyo akateuliwa mjumbe na kuchaguliwa mwenyekiti mwingine. Mwaka 2001 bwana siyangu akaja na watu wa ardhi ili afanye tasmini na apate hati miliki. kwa bahati nzuri mtoto wa mzee mwinyimvua , shomari ndio aliteuliwa kushika wadhifa wa ujumbe hivyo alipomwendea shomari na kumweleza kuhusu tasmini shomari alishangaa na kumwambia kuwa ametapeliwa na yeye kama mjumbe mwenye eneo hilo anayemiki kihalali ambaye ni mareheru michel, na huyo mtu aliyemuuzia siyangu sio mmiliki halai wa eneo lile alitumia vyeo vyake kuandaa karatasi na mashahidi wa uwongo. Bwana siyangu alitaharuki baada ya kupewa ukweli na akaamua kuongea na watu wa ardhi wamtengenezee hati miliki kwa kutumia barua za yule aliyemtapeli. na kwa sababu pesa zinaongea bwana siyangu alifanikiwa kupata hati miliki. Bwana siyangu akaliacha eneo lake pasipo kuliendeleza kuanzia mwaka 2001. Mnamo june 2009 wananchi wa eneo hilo baada ya kuona eneo hilo limekuwa ni kichaka na maficho kwa wezi kwani watu walikuwa wanakabwa na wakina mama kubakwa. wakaamua kuvamia shamba hilo la hekari mia zikiwemo zile hamsini za bwana siyangu. wakakata miti na kusafisha eneo lote kuwa jeupe na kila mtu akajigawia kwa jinsi anavyoweza na kuanza kujenga nyumba na wengine misingi. bwana siyangu akajitokeza september 2009 na kuanza kudai heka hamsini zake na kubomoa misingi na nyumba ambazo zilikuwa ndani ya eneo lake na kufungua kesi polisi kwamba watu wavamia shamba lake na kukata mazao yao yenye thamani ya milioni nane. hivyo anawatishia watu polisi na sio kuwapeleka mahakamani akawashitaki.

  Walio bomolewa nyumba wanamuogopa bwana siyangu. Kwani hawana barua yoyote ya kuwatambua kama ni wamiliki halali wa eneo hilo . kwani mjumbe ambae ni bwana shomari anawaona kuwa bwana siyangu na watu wote ni wavamizi wa eneo la marehemu michael. vivyo wanaogopa kumpeleka bwana siyangu mahakamani. na bwana siyangu hataki kuwashitaki mahakamani. kuna watu wengine ambao ni wabishi wameendelea kujenga kwa kujificha wakiogopa polisi ambao bwana siyangu huwa anawaleta kwa kuwatisha na sio kwenda mahakamani kuomba sop warant ili watu wasiendelee kujenga.

  jamani naomba buasra zenu wanasheria
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Nov 3, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Busara kuhusu nini? Be specific pls!
   
 3. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nimesoma haya uliyoyaandika pamoja ingawa kuna matundu na matobo mengi kwenye maelezo yako.
  Kimsingi kwanza maelezo yako yana mapungufu kwa sababu yamekuwa na maelezo ya upande mmoja sana kuliko kuwa na ya pande mbili ingawa umejitahidi ku-link maelezo, kwa hilo hongera.
  Jambo la pili ukisoma sheria za Ardhi namba 4 na 5 za mwaka 1999 zinaweka wazi kuwa kuwa eneo litatambulika kuwa limetelekezwa iwapo mambo yafuatayo yatakuwa yamejidhihirisha:-
  - Mmilikaji hakuwahi kuikalia na kuitumia ardhi kwa madhumuni yoyote ambayo ardhi inaweza kukaliwa na kutumiwa ikiwa ni pamoja na kuipumzisha kwa kilimo kwa kipindi kisichopungua miaka mitano (5).

  - Mbali ya mwanakijiji ambaye sehemu kubwa ya kipato chake inatokana na kilimo au ufugaji, mmilikaji anayedaiwa kodi ya pango, ushuru na madai kudhusiana na masuala ya Ardhi na ambaye ameendelea kudaiwa kodi ya pango hilo, ushuru na madai au sehemu yake yoyote kwa kipindi kisichopungua miaka miwili tangu kodi ya pango hilo, ushuru au madai au sehemu yake yoyote yalipoanza kudaiwa;

  - Mmilikaji wa eneo hilo ameondoka bila kumwandaa mtu yeyote kubeba majukumu ya Ardhi na kuhakikisha kwamba masharti yaliyosababishwa kutolewa kwa hakimiliki yanazingatiwa;

  Katika kutoa uamuzi kama Ardhi imetekelezwa kwa mujibu wa masharti ya hapo juu itabidi kuzingatia mambo yafuatayo

  - Kipato cha mmilikaji wa eneo na iwapo mmilikaji huyo ni mtu mmoja pekee, umri na jinsi alivyo kiafya;

  - Jinsi hali ya hewa kwenye eneo hilo ilivyokuwa kwa kipindi cha miaka mitatu ya nyuma;

  - Desturi za kimila, hususani desturi miongoni mwa wafugaji ambazo huenda zikawa ndizo zimesababisha Ardhi isitumike katika miaka mitatu ya nyuma;

  - Ushauri wowote uliohitajika na Halmashauri ya Kijiji au uliotolewa na Kamishna kwenye Halmashauri hiyo.

  NB: Nimetoa maelezo haya kama sheria za Ardhi zinayosema kwa sababu nimeona maelezo ya mtoa mada yanaendana na Ardhi kama iliyotelekezwa.
  Asanteni
   
Loading...