Mgogoro CUF: Prof. Lipumba amsimamisha kazi Maalim Seif, amteua Magdalena Sakaya kukaimu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
14368660_10154555173194339_6608631319716628532_n.jpg

Mgogoro wa Uongozi ndani ya Chama cha wananchi Cuf umeendelea Kufukuta ambapo M/kiti wa Chama hicho Prof.Ibrahim Lipumba amemteua Naibu Katibu Mkuu Bara Magdalena Sakaya kukaimu nafasi ya Katibu Mkuu Maalim Seif shariff Hamad baada ya Maalim Seif kukaidi wito wa M/KIti wake kwenda ofisi Kuu Buguruni kwa zaidi ya mara nne.

Prof Lipumba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam pamoja na wafuasi wa chama hicho amesema Maalim Seif amekaidi wito wa kwenda Makao makuu Buguruni tangu Septemba 23 mwaka jana kwa ajili ya kusimamia mkutano wa kamati ya Utendaji ambao ulitakiwa kujadili mambo kadhaa ya chama hicho.

Aidha Prof. Lipumba amewavua madaraka wakurungezi kutoka zanzibar akiwemo Salim Bimani aliyekuwa Mkurugenzi wa habari na Uenezi, Omar Ali Salehe Mkurugenzi Mipango na Uchaguzi, Abdallah Bakar Khamis Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi, Pavu Juma Abdallah – Haki za Binadamu, Mahima Ali Mahima Katibu Mtendaji JUvicuf pamoja na Yusuph Salim Naibu Mkurugenzi Ulinzi na Usalama Cuf wote kutoka Znz.

Chama cha wananchi Cuf kimekumbwa na mgogoro wa uongozi tangu Prof.Lipumba alipotanga kujiuzuru uongozi wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu 2015,ambapo baadae alitangaza kurudi na kufanyika mkutano mkuu ambao ulivurugika na kusababisha mpasuko kati ya Cuf bara na cuf Zanzibar.
 
b038a0856a53b6c28ca73576ef268321.jpg
Mgogoro wa Uongozi wa Chama cha Wananchi CUF umeendelea kufukuta ambapo Mwenyekiti wa Chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili Vyama vya Siasa nchini Prof. Ibrahim Lipumba amemteua Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya kukaimu nafasi ya Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad baada ya Maalim Seif kukaidi wito wa Mwenyekiti wake kwenda Ofisi kuu Buguruni kwa zaidi ya mara nne

Prof. Lipumba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam pamoja na wafuasi wa chama hicho, amesema Maalim Seif amekaidi wito wa kwenda Makao Makuu Buguruni tangu Septemba 23 mwaka jana kwa ajili ya kusimamia mkutano wa kamati ya Utendaji ambao ulitakiwa kujadili mambo kadhaa ya chama hicho

Aidha, Prof. Lipumba amewavua madaraka wakurugenzi kutoka Zanzibar akiwemo Salim Bimani aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Omar Ali Salehe Mkurugenzi Mipango na Uchaguzi, Abdalah Bakar Khamis Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi, Pavu Juma Abdallah - Haki za Binadamu, Mahima Ali Mahima Katibu Mtendaji JUVICUF pamoja na Yusuph Salim Naibu Mkurugenzi Ulinzi na Usalama CUF wote kutoka Zanzibar.

Chama cha Wananchi CUF kimekumbwa na Mgogoro wa uongozi tangu Prof. Lipumba alipotangaza kujiuzulu uongozi wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, ambapo baadaye alitangaza kurudi na kufanyika mkutano mkuu ambao ulivurugika na kusababisha mpasuko kati ya CUF bara na CUF Zanzibar.

Chanzo: ChannelTen
 
Hatutatoka kwenye reli hadi Makonda ajiuzulu. Msitutoe tafaazali
 
Mwambieni huyo pro-pesa Lipumba-vu kama ametumwa kututoa kwenye mjadala wa vyeti vya Daudi Albert Bashite al-maarufu kama Makonda, ameshafeli. Bado tutaendelea kupaza sauti zetu Bashite aonyeshe vyeti vyake kama alivyoonyesha yale majina ya aliowaita dealers wa dawa za kulevya. Hapa vyeti tu, pro-pesa Lipumbavu umebugi!
prof kazini. Usimuonee wivu
 
Back
Top Bottom