Mgeja aibua tuhuma nzito Barrick | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgeja aibua tuhuma nzito Barrick

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Jun 4, 2012.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  na Mwandishi wetu, Shinyanga

  MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja ameituhumu kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick kwa kuchimba madini ya fedha na shaba kinyemela.Mgeja ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Taifa, amedai kuwa kampuni hiyo pia imekiuka mkataba wake, na sasa inachimba dhahabu nje ya maeneo iliyopewa rasmi.Mwenyekiti huyo ametoa tuhuma hizo juzi katika kikao cha ushauri cha mkoa, akisema zipo taarifa za uhakika kuwa mwekezaji ameingia katika eneo kubwa mno, nje ya lile alilopewa kisheria, na kwamba amekuwa akichimba chini kwa chini umbali mrefu.“Kuna taarifa za vijana wetu zinaonesha kuwa Barrick sasa amekwenda umbali mrefu sana wa zaidi ya kilometa nne na karibu ataingia Mkoa wa Geita.“Hakuna ubishi kwamba huu ni wizi, lazima ufanyike uchunguzi wa haraka, tukiacha wizi huu uendelee, ipo hatari ya vizazi vijavyo vikatusuta,” alisema Mgeja.Alikiri kuwa maisha ya Watanzania wanaoishi jirani na maeneo ya migodi ni magumu kiuchumi, wakati mwekezaji anajipatia kipato kikubwa kutoka katika madini ya shaba na fedha ambayo halipii chochote serikalini.Aliishauri serikali kupitia upya mkataba wa mwekezaji huyo wa Bulyanhulu ili aweze kulipa mrabaha mwingine kutokana na madini ya shaba na fedha anayoyapata kutoka katika mgodi huo wa dhahabu anaoumiliki hivi sasa.Taarifa hiyo iliwashitua baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo ya ushauri ya mkoa, na kutaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya mwekezaji huyo.
   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hilo mbona lipo siku nyingi, au ndiyo inataka kugeuzwa turufu ya kisiasa? Haiwezekani inshu kama hii niliisikia miaka 4 - 5 iliyopita leo mgeja ndiyo anaanza kubwabwaja tena akiwa mkazi wa mkoa husika! Ukimuuliza kafanya nini kwa ajili ya mkoa wa shinyanga, utasikia aaaa! mara Ooooo.
   
 3. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Alikua wapi siku zote? au alisubiri wafike kilimeta nne? pambaf
   
 4. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  Huyu mzee ni mnafiki pia fisadi mkubwa, kwani hizo si ndio sera zenu za chukua chako mapema (ccm), na zaidi ya yote alikuwa wapi?
  Mnafiki sana uyu mzee wala hatudanganyiki wewe mzee mgeja ni mshirika mzuri tu wa mafisadi pia magamba
   
 5. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wameshindwa kuelewana nini tena? Kuna mtu karushwa hapo
   
 6. Josephine03

  Josephine03 JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 752
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Atakuwa kanyimwa mgawo huyo hana lolote, mbona tunaijua toka kitambo

  Sent from my BlackBerry 9910 using JamiiForums
   
 7. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,041
  Likes Received: 8,532
  Trophy Points: 280
  Huo mgodi utaifishwe haraka sana.
   
 8. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mhusika ambaye angeweza kushughulikia hilo swala kesha chukua chake mapema , huyo mzee analeta poroja za barazani kufurahisha umati hana lolote.
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  aaaaa,,,,,,jamani yaan leo ndo bwana hamis amejua ni wizi????,,,anataka tusutwe na nani tena???mimi binafsi nawasuta wao kwa kugawa madini,,,,,,sasa anamwambia nani????,sheria ya madini ni mbovu,na watu washasema sana tu,na tume lukuki zimeundwa,hakua jipya hapo
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  tena na gahawa mkononi,,,,kwani kuna jipya hapo????si kweli kwamba kamishna wa madini hajui hii dili
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  binafsi nimewaza kitu kama hiki,kwa sasa atapewa MGAO,WASHAMSIKIA
   
 12. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #12
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Tukiachana na mambo ya mgao,lakini jamani inakuwaje wawekezaji wanaionea sana tanzania? inakuwaje kuchimba madini ambayo hawaruhusiwi kuchimba

  waziri husika,madudu mengine hayo

  jamani tuvunje mkataba,kuanza upya si ujinga
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huyu Mgeja kachemsha, utachimbaje dhahabu itoke dhahabu pekee? migodi mingi duniani (kama si yote) ya dhahabu huwa inatoa na fedha na shaba kwa kiwango fulani.
   
 14. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  si walishapokea 10%? watulie....
  umeona wapi mtu anasafirisha mchanga nje?

  aaah hivi wale waliopiga wananchi na kuwaua kwa kutumia polisi na kusingizia chama fulani cha siasa walikuwa mgodi upi?
   
 15. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  engmtolera hii kitu si yaleo alikuwa wapi na ni mkazi wa shy?

  Wawekezaji hawaineni tza ni ujinga wetu watz wa kushindwa kuwawajibisha walafi wachache wanaotumikia matumbo yao na famili zao na kuisahau tz na watu wake.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #16
  Jun 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Taijike
  ni kweli kuna jamaa kanitonya hapa anadai tangu 1998 jamaa wamekuwa wakipeleka mchanga wa madini hayo nje,lakini pia mwaka huo tayari walikuwa wamevuka 5km nje ya mkataba,ila viongozi wetu wapo na wanakura raha tu
   
 17. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  engmtolera
  Ni ujinga/umbumbu wetu wa kuangalia na kuridhika na hali yoyote ile inayojitokeza hata kama siya kawaida. Mkataba wao ni dhahabu hiyo shaba na fedha iko ktk mrahaba na mkataba upi? na ilipogundulika kuwa barrick imevuka mpaka wa uvunaji wake wa dhahabu na kuingia mpaka Mkoa mpya wa geita ni hatua zipi zilichukuliwa kwa mali ilikwisha ondoka, kwa upande wa serikali na wakazi wa maeneo husika?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,344
  Likes Received: 2,679
  Trophy Points: 280
  haya ndio malipo ya kuchagua kitu kinaitwa CCM, wanaingia madarakani kwa nguvu za giza na kufunga akili za wananchi kwa nguvu za kichawi ili hata wasihoji maslahi ya Taifa lao....
   
 19. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #19
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  mdau yaan unahisi serikali HAIJUI??????HAKUNA LINALOFANYIKA BILA WAO KUJUA,,,,KAMA KAJUA MGEJA BASI WANAJUA WEEEENGI MNO
   
 20. wantuzu

  wantuzu Senior Member

  #20
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 145
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  nimefanya kazi kwenye huo mgodi husika kwa miaka si chini ya saba nnachoweza kuwashauri wabongo , ni kwenda ofisini kwao pale hamza azizi rd masaki , watawapa kibari cha kwenda kutembea mgodini kwa gharama zao...
  tusishuhudie habari ambazo hatuna uhakika nazo na watu wasitumie udhaifu wa watanzania wa kutafuta usahihi wa habari kujinufaisha kisiasa , acheni !
   
Loading...