Mgawo wa umeme waleta hasara ya Sh40.5 bilioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgawo wa umeme waleta hasara ya Sh40.5 bilioni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Dec 2, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] tanesco-logo.jpg Patricia Kimelemeta na Aziza Masoud
  SHIRIKISHO la Wenye Viwanda nchini (CTI) limesema Sh40.5 bilioni zimepotea serikalini na viwandani mwaka huu kutokana na makali ya mgawo wa umeme.
  Upotevu huo umejulikana baada ya utafiti uliofanywa na Shirikisho hilo kwa muda wa miezi sita kuhusu hali ya upatikanaji wa umeme nchini. Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanyika kwenye viwanda 60 nchini, viwanda vimepoteza Sh31 bilioni na taasisi za Serikali zimepoteza Sh9.5 bilioni.
  Kutokana na matokeo hayo, CTI sasa imependekeza Tanesco igawanywe katika vitengo vya uzalishaji na usambazaji kulipunguzia mzigo na kuliongezea ufanisi.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,Mkurugenzi wa Sera na Ushawishi wa CTI, Hussein Kamote alisema ili kupunguza tatizo hilo Serikali inapaswa kushirikisha wadau mbalimbali ili kuzalisha umeme huo. Alisema kitendo cha kukosekana kwa umeme wa uhakika kunachangia kushuka kwa uzalishaji mali kwenye viwanda, jambo ambalo linaathiri uchumi wa nchi na kukimbiza wawekezaji, kutokana na hali hiyo Serikali inapaswa kuliangalia suala hilo kwa kina ili kuondoa matatizo yanayoweza kujitokeza siku za usoni.

  “Tumefanya utafiti wa miezi sita, ambapo tumeweza kutembelea viwanda 60 vya hapa nchini, lakini tumebaini kuwa, uzalishaji mali kwenye viwanda hivyo umeshuka, hii inatokana na kutokuwapo kwa umeme wa uhakika, jambo ambalo pia limeathiri uchumi wan chi,”alisema Kamote.

  Aliongeza kutokana na hali hiyo viwanda hivyo vimeweza kupoteza zaidi ya Sh31 bilioni kwa mwaka, kiasi ambacho ni kikubwa katika ujenzi wa maendeleo ya Taifa,kutokana na hali hiyo Serikali inapaswa kushirikishaa wadau mbalimbali ili waweze kuzalisha umeme.
  Alibainisha kuwa,mbali na suala hilo pia wananchi wameweza kupoteza ajira zao kutokana na viwanda hivyo kushindwa kufanya kazi kwa muda wa saa 24 kutokana na mgao huo, jambo ambalo limesababisha kuwapo kwa idadi kubwa ya watu wasiokuwa na ajira.

  Alifafanua kwamba ya asilimia 80 ya mapato ya Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco) yanatokana na viwanda, ikiwa vitashindwa kufanya kazi watashinwa kukusanya fedha hizo. Kamote alisema CTI imeishauri Serikali kuharakisha miradi ya umeme waliyokusudia ikiwamo ya kutumia makaa ya mawe ya Liganga na mchuchuma, kampuni ya kuzalisha umeme ya Agrekko, IPTL na Symbion ili iweze kufanya kazi ya kuzalisha umeme huo jambo ambalo wanaamini linaweza kupunguza makali.

  Alibainisha kuwa, mbali na hali hilo pia Serikali ingepaswa kuligawa shirika hilo na kuwa mawili ili kila moja liweze kufanya kazi zake ipasavyo. Alisema sheria iliyopo sasa inazitaka kampuni kuzalisha megawati 10 za umeme kupitia Tanesco, jambo ambalo limesababisha kampuni nyingi za kizalendo kushindwa. Kwa mujibu wa Kamote, CTI iko kwenye mchakato wa kuanzisha kampuni ya kusimamia upatikanaji wa umeme kwa kushirikiana na Tanesco ili waweze kupata umeme wa uhakika ambao utaongeza uzalishaji na kupunguza makali ya mgao.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  chanzo: Mgawo wa umeme waleta hasara ya Sh40.5 bilioni
   
 2. C

  CHIPANJE JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Chanzo chako ndo heading yako.Kua muwazi.
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Lakini pamoja na hasara hiyo, uchumi wa tz umeendelea kukua kwa kasi! Wonders will never cease,huh!
   
Loading...