Naomba kujulishwa wanaJF kama mgawo umeanza au kuna tatizo gani maana huku ubungo (baadhi ya maeneo) umeme umekuwa adimu wiki ya pili hii. Mfano jana umekatwa saa kumi na mbili jioni umerudi leo saa 7 mchana. Ukawaka hadi saa 9 ukakatika. Ukarudi saa 10 jioni. Saa 12 umekatika na haijulikani utarudi saa ngapi. Nijuzeni wapendwa huenda tangazo la mgawo limetolewa mie limenipita.
Siku nyingine umeme unakatika baada ya dk 5 unaludi na kukatika tena,hauludi mpaka asubuhi,wangetangaza tu kwamba kuna mgao ili watu watambue,watu wanapata hasara kila kukicha.