Mgawanyo wa wizara liwe suala la kikatiba

Desteo

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
494
123
Maana tunaona kila Rais akiingia anapanga baraza lake na kuweka vipaumbele vyake. Wengine wanaongeza wizara kwa sababu za kiufanisi na wengine wanapunguza wizara kwa sababu hizo hizo za kiufanisi. Ifike mahali katiba iseme kutakuwa na wizara ngapi na zipi. Au mnasemaje?
 
Ni ngumu kwa sasa kuwa na wizara kikatiba. Mahitaji yetu ni tofauti na Ulaya au Marekani. Kuna mambo tunahitaji kuyashugjulikia huku kwetu tofauti na mataifa mengine ambayo huko yalishapita kitambo. Wizara ya mifugo, kwa mfano, huwezi kuiondoa. Tuna wafugaji vichwa ngumu wanaopaswa kubadilishwa. Marekani huwezi kusikia wakulima na wafugaji wanauwana! Mahitaji bado yanatufanya tuwe wa kubadili wizara kila tunapopata kiongozi mpya wa taifa. Ni mtazamo wangu tu.
 
Rasimu ya katiba ya warioba ilizungumzia hili ila maccm yakaipiga mateke.
 
Mbona tuliweka hili katika rasimu ya warioba, sema tulitaja idadi ya wizara (sikumbuki vizuri idadi yake) lakini siyo majina yake. Lengo ni kupunguza matumizi na kumbana rais asiongeze wizara kuwapa washkaji ulaji
 
Ni ngumu kwa sasa kuwa na wizara kikatiba. Mahitaji yetu ni tofauti na Ulaya au Marekani. Kuna mambo tunahitaji kuyashugjulikia huku kwetu tofauti na mataifa mengine ambayo huko yalishapita kitambo. Wizara ya mifugo, kwa mfano, huwezi kuiondoa. Tuna wafugaji vichwa ngumu wanaopaswa kubadilishwa. Marekani huwezi kusikia wakulima na wafugaji wanauwana! Mahitaji bado yanatufanya tuwe wa kubadili wizara kila tunapopata kiongozi mpya wa taifa. Ni mtazamo wangu tu.

Chakushangaza kwetu hapa kuna maeneo mengi zaidi hivyo hakukua na sababu ya wakulima na wafugaji kuuana
 
Pokeeni 'like' yangu wadau wote huko juu maana sinayo ya kubofya. Nina imani kuwa tukitumia approach ya 'what if' ambayo hata mataifa makubwa yaliyoendelea yanatumia tunaweza kufika mahali tukasema tunahitaji wizara hizi na hizi. Uzuri tuna think tank ambayo ni tume yetu ya mipango. Taifa lina miaka 54 ambayo inatuwezesha kujua yapi ya kufanya na yapi ya kuacha. Suala la rasilimali naona ndio linaloleta sintofahamu sana kwa kuwa halina mwongozo unaojitosheleza. Nashukuru wadau kwa kuona kuwa liliwekwa kwenye katiba pendekezwa ila hawa ccm wakaona si kitu. Sasa Mwakyembe na Magufuli ni wakati wa kuyafanyia kazi hayo mapendekezo
 
Back
Top Bottom