Mgawanyo mpya wa majimbo ya uchaguzi

Mgawanyo mpya wa majimbo ya uchaguzi

Ni kweli kabisa ukubwa wa Wilaya kigiografia hakuna madhara ya kuwa na mwakilishi mmoja. Maana Mbunge kazi kubwa ni kupeleka mawazo ya wengi kwenye General assembly
Hapo mbunge ana faida gani kwenye ukubwa wa wilaya?labda uniambie wilaya zigawanywe ila sio kuzalisha jimbo.mbunge mmoja anatosha,zaidi ya hapo ni kupeana vyeo tu

2020
 
Kama Wilaya ni kubwa kigiografia ni suala la kuongeza mafuta Tu.
Yaani Waziri anazunguka nchi nzima then wewe Mbuge unashindwa kuzunguka Jimbo lako? Umspewa gari na dereva na mafuta ya kutosha Leo unasema huwezi kuzunguka Wilaya yenye vijiji 80 au chini ya hapo.
Pamoja na umri huo hujui faida ya mbunge jimboni kwako ?

Hebu chukua wilaya kubwa kama Igunga mbunge mmoja mpaka anamaliza miaka mitano hajawahi kufika baadhi ya kata.

Sent using Jamii Forums mobile app

2020
 
kukiwa na Rais mwenye maono na mawazo chanya, haihitaji kuwa na wabunge wengi nchini. Maana tuna wasomi wengi sana kama ni sheria zinaweza tungwa vyuoni alafu zinapelekwa kwa Rais kwa ajili ya kupitishwa basi. Lakini kumchukua mbunge asiyesoma au taaluma isiyoeleweka alafu akawa mstari wa mbele kutunga sheria ya mambo asiyo na uelewa nayo inatugharimu sana kama nchi. Unaona kabisa kuna wabunge wengine kichwani hamna kitu hadi unajiuliza huyu wananchi waliomchagua walizingatia kigezo gani hupati jibu..ila ndio hivyo kawa mbunge. Tungepunguza mrundikano wa wabunge bungeni kwa kupunguza majimbo ama kwa kuyaunganisha baadhi ya majimbo
 
Mbunge achoke vip wakati mkuu wa Wilaya ni mmoja lakini halalamiki ukubwa wa Wilaya na anatembea kila kijiji. Wewe Mbunge unashindwa kutembelea vijiji 80.
Mfano kama Mbunge Una vijiji 80 then unatembelea vijiji 2 kila siku ni sawa na siku 40 Tu Kwa mwaka umemaliza. Kabla kama unakaa mbali na Jimbo hapo ndio hutoweza.
Idadi ya watu haitoshi kuwa kigezo kwani inategemea hao watu wanaishi vp? Mfano, unakuta jimbo linakuwa na eneo kubwa la utawala na watu wanakuwa Scattered hivyo uwakilishi nao unakuwa mgumu sana. Hivyo basi Mbunge mmoja huchoka ndio sababu Wilaya moja inakuwa na zaidi ya jimbo moja!

Sent using Jamii Forums mobile app

2020
 
Mkuu nina imani na utawala wa wa sasa kwa kubana matumizi. Hii inawezekana kabisa suala ni kusubiri Bunge livunjwe then ndio NEC ifanye huo mgawanyo. Unajua wakigawa sasa hivi watagoma kupitisha bajeti na pia watapiga kelele sana. Lakini mwezi wa Saba baada ya kuvunjwa Bunge hakutakuwa na kizuizi coz hakutakuwa na Bunge. Yaani NEC ikiamua inaweza kabisa Kwa mwezi July. Mungu mkubwa ngoja tuombe.
kukiwa na Rais mwenye maono na mawazo chanya, haihitaji kuwa na wabunge wengi nchini. Maana tuna wasomi wengi sana kama ni sheria zinaweza tungwa vyuoni alafu zinapelekwa kwa Rais kwa ajili ya kupitishwa basi. Lakini kumchukua mbunge asiyesoma au taaluma isiyoeleweka alafu akawa mstari wa mbele kutunga sheria ya mambo asiyo na uelewa nayo inatugharimu sana kama nchi. Unaona kabisa kuna wabunge wengine kichwani hamna kitu hadi unajiuliza huyu wananchi waliomchagua walizingatia kigezo gani hupati jibu..ila ndio hivyo kawa mbunge. Tungepunguza mrundikano wa wabunge bungeni kwa kupunguza majimbo ama kwa kuyaunganisha baadhi ya majimbo

2020
 
Pamoja na umri huo hujui faida ya mbunge jimboni kwako ?

Hebu chukua wilaya kubwa kama Igunga mbunge mmoja mpaka anamaliza miaka mitano hajawahi kufika baadhi ya kata.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hajawahi kufika baadhi ya kata, ni kwamba huyo mbunge ana mambo yake tu, miaka mitano na shangingi juu ana shindwa kufika jimbo lote mbona mgombea wa urais miezi mitatu tu anakuwa kesha fika kata zote za nchi.
 
kukiwa na Rais mwenye maono na mawazo chanya, haihitaji kuwa na wabunge wengi nchini. Maana tuna wasomi wengi sana kama ni sheria zinaweza tungwa vyuoni alafu zinapelekwa kwa Rais kwa ajili ya kupitishwa basi. Lakini kumchukua mbunge asiyesoma au taaluma isiyoeleweka alafu akawa mstari wa mbele kutunga sheria ya mambo asiyo na uelewa nayo inatugharimu sana kama nchi. Unaona kabisa kuna wabunge wengine kichwani hamna kitu hadi unajiuliza huyu wananchi waliomchagua walizingatia kigezo gani hupati jibu..ila ndio hivyo kawa mbunge. Tungepunguza mrundikano wa wabunge bungeni kwa kupunguza majimbo ama kwa kuyaunganisha baadhi ya majimbo
Hii hoja inaweza kutolewa na mtoto wa darasa la pili tu.

Hujui hata utungaji wa sheria unavyofanyika ?

Rais mwenye maono chanya ?? Hayo maono unayapima vipi kuwa ni chanya ?

Vyuo vitunge sheria kama mihimili ya dola au kama nini ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbunge achoke vip wakati mkuu wa Wilaya ni mmoja lakini halalamiki ukubwa wa Wilaya na anatembea kila kijiji. Wewe Mbunge unashindwa kutembelea vijiji 80.
Mfano kama Mbunge Una vijiji 80 then unatembelea vijiji 2 kila siku ni sawa na siku 40 Tu Kwa mwaka umemaliza. Kabla kama unakaa mbali na Jimbo hapo ndio hutoweza.

2020
Kwani wakuu wa wilaya hutembelea kila kona ya wilaya ?

Mara nyingi hawa hutembelea maeneo ya wilaya zao kwa matukio maalumu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nina imani na utawala wa wa sasa kwa kubana matumizi. Hii inawezekana kabisa suala ni kusubiri Bunge livunjwe then ndio NEC ifanye huo mgawanyo. Unajua wakigawa sasa hivi watagoma kupitisha bajeti na pia watapiga kelele sana. Lakini mwezi wa Saba baada ya kuvunjwa Bunge hakutakuwa na kizuizi coz hakutakuwa na Bunge. Yaani NEC ikiamua inaweza kabisa Kwa mwezi July. Mungu mkubwa ngoja tuombe.

2020
Haya mambo yanafanyika law mujibu wa sheria siyo kwa matakwa ya rais.

Unaposema utawala huu hautakubali maana hiyo unakiri kuwa NEC siyo chombo huru siyo ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pendekezo langu ni kama ifuatayo.
1. Kuwepo na bunge la mkoa; kazi yake itakua kupanga na kuratibu mapato yatokanayo na mkoa baada ya kupokea mipango ya baraza la madiwani la halmashauri mbalimbali. Bunge hili litakua na wawakilishi wa kuchaguliwa na wananchi na mgawanyiko utokane na idadi ya watu kwa kila mkoa.

2. Kuwepo na mshahara unaoratibiwa na sheria ya kazi na ajira kwa kushirikiana na utumishi wa Umma ili kuweza kuleta uwiano wa kimapato kati ya hawa wawakilishi na watumishi walioajiriwa serikalini.

3. Kuwepo na mwakilishi mmoja au zaidi kutoka kila Bunge la mkoa ili kukutana Bunge la Jamhuri ya Muungano kama mwakilishi wa mkoa.

4. Wakuu wa wilaya na mikoa zifutwe kwa kufanya maboresho zaidi kwa RAS na DAS ki majukumu.

5. NEC ivunjwe na kuboreshwa zaidi kwa kua na wawakilishi kuanzia ngazi ya mtaa na iwe ni taasisi inayojitegemea chini ya wizara ya yoyote itakavyopendekezwa. Nafasi za watumishi wa NEC watokane na usahili kama kazi zingine; kuwepo na bodi ya kuratibu na kuchunguza maamuzi ya NEC kabla ya NEC kutangaza au kutoa maamuzi yoyote kwa umma. Bodi ya uratibu ziwe ni nafasi zinazopendekezwa na Rais lakini wanapigiwa kura Bungeni.

5. Zanzibar isiwe na wabunge kwani idadi ya kura zinazopatikana kwenye kila jimbo la uchaguzi haiakisi maana ya neno jimbo bali Zanzibar nzima wateue mwakilishi mmoja au zaidi kuiwakilisha kwenye Bunge la Muungano.
 
NEC imepewa mamlaka ya kisheria kugawa majimbo so ni kitu kinachowezekana kama wataamua mkuu.
Haya mambo yanafanyika law mujibu wa sheria siyo kwa matakwa ya rais.

Unaposema utawala huu hautakubali maana hiyo unakiri kuwa NEC siyo chombo huru siyo ?

Sent using Jamii Forums mobile app

2020
 
Kuna majimbo 214 Tanzania Bara na majimbo 50 Zanzibar.
  • Wabunge 264 waliochaguliwa katika majimbo ya uchaguzi
  • Wabunge 113 walioingia kupitia viti maalumu kwa wanawake
  • Wabunge 5 walioteuliwa na Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar
  • Wabunge 10 walioteuliwa na Rais wa Tanzania
  • Mwanasheria Mkuu
Majimbo yanatofautiana kwa kiasi kikubwa katika idadi ya wakazi. Wastani wa Tanzania bara ni mbunge mmoja kwa wakazi 227,461. [3] Kuna majimbo katika mikoa ambako mbunge mmoja anawakilisha watu wengi zaidi kama vile Dar es Salaam (wakazi 546,542/mbunge 1), Mwanza (346,999) na Kagera (309,953). Kinyume chake kuna majimbo mengine ambako mbunge anawakilisha watu wachache kama vile Pwani (wakazi 133.104/mbunge), Katavi (128.513), Njombe (120.795) au Lindi (112.192).

Tofauti ni kubwa zaidi huko Zanzibar. Kwa mfano Wilaya ya Kaskazini B katika Mkoa wa Unguja Kaskazini ina wakazi 81,675[4] pekee lakini inachagua wabunge 4 katika majimbo ya Bumbwini, Donge, Kiwengwa na Mahonda.
Source: Bunge la Tanzania - Wikipedia, kamusi elezo huru.

Leo katika mchango wake wa Bungeni Mheshimiwa Kessy ameikumbusha NEC kupitia upya mgawanyo wa majimbo kwa kuzingatia idadi ya kata na watu kwa kila jimbo. Akatolea mfano wa baadhi ya Halmashauri kuwa na kata 10 na zingine kuwa na kata 30.

Kwa upande wangu naona ni vyema wazo hili likaangaliwa upya kwa vile sioni sababu ya kuwa na wabunge zaidi ya 390 kwa mgawanyo wa hivi sasa maana hata fursa ya kushiriki mijadala ya bungeni inakuwa hafifu.

Ninashauri kigezo kikuu kiwe ni kila wilaya iwe ni jimbo moja tu kama zamani. Mfano Tanzania Bara tuna wilaya kama 135 na zanzibar wana wilaya 10 tu ambapo ukiweka na wanawake angalaau unapata wabunge wasiozidi 200.

Naombeni michango itakayowezesha hili wazo liboreshwe na kufanyiwa kazi hata kama si kwa mwaka huu.

Hii itasaidia kupunguza gharama kubwa katika kuendesha bunge na pia itawezesha wabunge wachache kushiriki vyema katika mijadala Bungeni.

Nawasilisha.
Turudi kwenye enzi ya wilaya kuwa Jimbo la ubunge.
Tucheze na ukubwa na idadi ya watu kwa kila wilaya.
 
Nakuunga mkono. Kila Wilaya iwe na Mbunge mmoja na Viti Maalum kwa akina Mama vifutwe.
 
Naomba mtambue maendeleo yetu ya karibu yanaletwa na halmashauri yakisimamiwa kwa pamoja kati ya baraza la madiwani na mtendaji wa serilali yaani mkurugenzi wa manispaa au halmashauri.
Bunge sio tena sehemu ya kusema kuna hoja za kuleta maendeleo zaidi ya kutunga sheria na kupitisha bajeti kuu.

Najua tumechelewa lakini KATIBA ijayo ifute aina hii ya ubunge badala yake ma meya wa halmashauri ndio wawe wenyeviti kwenye balaza la madiwani lakini ndio WAWE wawakilishi bungeni yaani tuwe tUNApiga kura ya rais na madiwani.
halafu kupitia madiwani ndio kuwe na uchaguzi wa meya ambae moja kwa moja anaenda kuwa mbunge kutoka halmashauri husika.

kwa mtindo huu TUTAFUTA pesa ya jimbo ambayo wananchi ni kama hatuielewi na mbunge hufanya kama yake.
TUTAOKOA gharama za uchaguzi wa wabunge.

Upana wa DEMOKRASIA utakuwa mkubwa kwani ili uwe mbunge inakulazimu uchujwe na uteuliwe na watu mara mbili mbili.

UDIWANI utakuwa na nguvu,kuna madiwani hawapo na wananchi kabisa yaani tarura wanajenga barabara wao hawaelezi shida zao watakosa nguvu ya kugombea upya.

Mawaziri watatoka humo humo ila kule kulikoteuliwa waziri wachague meya mwengine ili awe mbunge.

Spika nao uwe kama ilivyo kwa mawaziri.

Sijui kwa sasa tuna halmashauri ngapi lakin TANZANIA Ya sasa haihitaji kuongezeka kwa mkoa wala idadi ya wabunge bali ni kuimarisha halmashauri zetu ziwahudumie wananchi huko waliko na maendeleo yazingatie uwakilishi na hoja za madiwani.
Mipango mikubwa ya kimkakati ya nchi (state interest stategy) ndio iwe miradi ya kujadiliwa bungeni na tuondokane na wabunge wa kulilia barabara na maji.

Miradi yote ya mikoani halmashauri wazilete kwa mkurugenzi na ziombewe bajeti na kama bajeti hakuna,Bunge waeleze kuwa bajeti ijayo hiyo miradi ipewe kipaumbele ili kuweka tija ndani ya muda.

Viti maalum viwepo lakini utoke kwenye uwakilishi wa vikundi yaani
Walemavu,vijana,mashule,wataalam wa afya,wanasheria,wafanyakazi wa vyuo,majeshi, na tuepukane na ubinafsi wa kuwapeleka wake zetu bungeni.

Nimekukubali sana mkuu. Kwa kweli unaitakia mema nchi yetu. Mawazo yako yakifanyiwa kazi na maboresho kidogo tutasonga mbele hakika

Hoja ya ugatuzi wa madaraka ni hoja ya msingi lakini siyo kwa fashion unayoipendekeza hapa.

Hiki mnachokizungumza hapa cha wabunge kupoteza nguvu kunatokana na udhaifu wa mifumo yetu ya udhibiti na pia kunatokana na bunge kuwa rubber stamp ya dola.

Siafiki hoja ya kuacha wakuu wa wilaya na madiwani wawe sehemu ya bunge kwanza hao kimsingi ni viongozi katika serikali za mitaa.

Nakatika mifumo ya republics lazima kuwe na chombo konachotunga sheria na kuhusu idadi ya wabunge kwa sasa inaongozwa viti maalumu ambavyo kimsingi havina maana yeyote kwa sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ondo
Kupunguza wabunge ni kupunguza kiwango cha uwakilishi wa wananchi bungeni.

1. sikubaliani na hoja ya wilaya kuwa ndiyo majimbo ya uchaguzi sababu kubwa ni moja kuna wilaya zingine geografia yake siyo rafiki kwa kuwa na mbunge mmoja tu achilia mbali kigezo cha watu.

2. Hatuwezi kukwepa gharama katika demokrasia ni lazima tukubaliane na hili kuwa demokrasia ni gharama hivyo lazima tuubebe huo mzigo

3. kama tunataka kupunguza gharama katika bunge ni vema tukaangalia kiwango cha mishahara, posho na viinua migongo wanavyolipwa wabunge ni kubwa sana tujaribu kupunguza hapa hii kwanza itasaidia kuondoa wajasiriasiasa bungeni na kuleta watu wenye nia ya dhati ya kuongoza watu.

4. Njia nyingine tufanye ugatuzi wa madaraka kwa viongozi wa wilaya na mikoa kuchaguliwa na wananchi badala ya kuwa na viongozi wengi ambao kimsingi wanatekeleza kazi zinafanana huko TAMISEMI. walau kama tukifanya hivi hoja yako ya kupunguza wabunge itakuwa na nguvu kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ondoa namba 1 na namba 2; Mchango wako utakuwa Bora sana.
 
Back
Top Bottom