East African
JF-Expert Member
- Nov 27, 2013
- 704
- 995
Kuna majimbo 214 Tanzania Bara na majimbo 50 Zanzibar.
Tofauti ni kubwa zaidi huko Zanzibar. Kwa mfano Wilaya ya Kaskazini B katika Mkoa wa Unguja Kaskazini ina wakazi 81,675[4] pekee lakini inachagua wabunge 4 katika majimbo ya Bumbwini, Donge, Kiwengwa na Mahonda.
Source: Bunge la Tanzania - Wikipedia, kamusi elezo huru.
Leo katika mchango wake wa Bungeni Mheshimiwa Kessy ameikumbusha NEC kupitia upya mgawanyo wa majimbo kwa kuzingatia idadi ya kata na watu kwa kila jimbo. Akatolea mfano wa baadhi ya Halmashauri kuwa na kata 10 na zingine kuwa na kata 30.
Kwa upande wangu naona ni vyema wazo hili likaangaliwa upya kwa vile sioni sababu ya kuwa na wabunge zaidi ya 390 kwa mgawanyo wa hivi sasa maana hata fursa ya kushiriki mijadala ya bungeni inakuwa hafifu.
Ninashauri kigezo kikuu kiwe ni kila wilaya iwe ni jimbo moja tu kama zamani. Mfano Tanzania Bara tuna wilaya kama 135 na zanzibar wana wilaya 10 tu ambapo ukiweka na wanawake angalaau unapata wabunge wasiozidi 200.
Naombeni michango itakayowezesha hili wazo liboreshwe na kufanyiwa kazi hata kama si kwa mwaka huu.
Hii itasaidia kupunguza gharama kubwa katika kuendesha bunge na pia itawezesha wabunge wachache kushiriki vyema katika mijadala Bungeni.
Nawasilisha.
- Wabunge 264 waliochaguliwa katika majimbo ya uchaguzi
- Wabunge 113 walioingia kupitia viti maalumu kwa wanawake
- Wabunge 5 walioteuliwa na Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar
- Wabunge 10 walioteuliwa na Rais wa Tanzania
- Mwanasheria Mkuu