Mgawanyo mpya wa majimbo ya uchaguzi

Mgawanyo mpya wa majimbo ya uchaguzi

Ukweli hatuna Wabunge,tuna wachumia tumbo. Ukijumlisha na wale wapiga vigelegele 113 basi. Lakini ukweli Idadi ya Wabunge ni kubwa, si rahisi hata kupata nafasi ya kutoa mchango, hata kama wanachangia kwa njia nyingine ikiwemo maandishi.

Unakuta wamelala, hadi kupishanisha vifungo vya makoti kwa sababu ya shibe. Lakini dhana ya uwakilishi haiko wanavyoifanya. Kuna wakati unatamani, huo Mhimili ufutwe tu. Kwa sababu CD wanayocheza ni ile ile ya Kivukoni High School.

Naunga Mkono hoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga Mkono hoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa jinsi watanzania tulivyo na wawakilishi tunaowachagua, hata tukiwa na bunge lenye wabunge 25 tu hatuna hasara.

390 waliopo kazi ni kusifu tu usiku na mchana.
 
Wastani kwa mkoa kuwe na wabunge 3 hadi 2. Inatosha sana.

Hawa sio watendaje mahala popote ni blabla tu ya kujua changamoto na kuzisemea.

Hii itawafanya kuwa wawajibikaji zaidi na wale wavivu wataukimbia wenyewe ubunge.

Wachache walipwe vizr lakino majukumu yawe mlima.

Mtu akimaliza 5 years ajitafakari mwenyewe kama atahitaji kuongeza muda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wafute viti maalum bungeni, zile nafasi 10 za rais futa, wale wazenji wa tano kutoka baraza la wawakilishi nao futa! Kisha punguza idadi ya majimbo, hakuna tija yoyote ile kuwa na idadi kubwa ya wabunge! Bunge kama hili la Ndugai lina faida gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wewe ndo hujui,mbunge hafanyi kazi peke yake ana madiwani wanakaa kwenye kamati za halmashauri kupata mipango na changamoto za kila kata. Mbunge hafanyi kazi peke yake kama shetani ana madiwani,DC,watendaji wa kata,DAS na wakuu wa wilaya, ana kamati ya mfuko wa jimbo wote hao wamesambaa kila mahali. yupo mkuu wa mkoa. wabunge wazembe wa CCM ndio chanzo cha kuona majimbo ni makubwa. hawapo majimboni na vikao hawahudhulii. Mfano huyo Kafumu vikaoni hayupo. Seif Gulamali hayupo vikaoni anawindana na mkurugenzi. Hapo lazima uone Igunga kubwa
Kwanza 90% ya watu uliowataja wote ni watendaji wa serikali ambao siyo wawakilishi wa wananchi.

Madiwani wapo kwajili ya kutekeleza ilani na manifesto zao kwenye kata zao siyo za mbunge.

Wananchi wanahitaji uwakilishi kero zao zifikishwe serikalini na wabunge ndiyo msimamizi na watetezi wa wananchi sasa unapotaka wapunguzwe nashindwa kuona mantiki hapa.

Pale juu nimesema kubana gharama za uendeshaji bunge ni heri tupunguze mishahara ya wabunge na posho mbalimbali hii itaondoa wajasiriasiasa kama hao kina Gulamali na Kina Kafumu ambao ni wengi sana.

Hoja yako ya Madc Rcs na Das ingekuwa na mashiko kama hao DCs na RCs wangekuwa ni wa kuchaguliwa na wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wilaya ziongezwe kusogeza huduma karibu kwa wananchi then majimbo ya punguzwe since wilaya zikiongezwa madiwani watajadili then mawazo yatabebwa na mbunge husika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Idadi ya watu haitoshi kuwa kigezo kwani inategemea hao watu wanaishi vp? Mfano, unakuta jimbo linakuwa na eneo kubwa la utawala na watu wanakuwa Scattered hivyo uwakilishi nao unakuwa mgumu sana. Hivyo basi Mbunge mmoja huchoka ndio sababu Wilaya moja inakuwa na zaidi ya jimbo moja!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwamfano Zanzibar wabunge waliopo ni wengi mno sasa Zanzibar ina watu kama million moja na point halafu kuna majimbo 50 wakati Tanganyika ina watu million kama 55 halafu kuna majimbo 214 ya uchaguzi. Huu ni muungano feki zaidi kuwahi kutokea duniani.
Kuna majimbo 214 Tanzania Bara na majimbo 50 Zanzibar.
  • Wabunge 264 waliochaguliwa katika majimbo ya uchaguzi
  • Wabunge 113 walioingia kupitia viti maalumu kwa wanawake
  • Wabunge 5 walioteuliwa na Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar
  • Wabunge 10 walioteuliwa na Rais wa Tanzania
  • Mwanasheria Mkuu

Majimbo yanatofautiana kwa kiasi kikubwa katika idadi ya wakazi. Wastani wa Tanzania bara ni mbunge mmoja kwa wakazi 227,461. [3] Kuna majimbo katika mikoa ambako mbunge mmoja anawakilisha watu wengi zaidi kama vile Dar es Salaam (wakazi 546,542/mbunge 1), Mwanza (346,999) na Kagera (309,953). Kinyume chake kuna majimbo mengine ambako mbunge anawakilisha watu wachache kama vile Pwani (wakazi 133.104/mbunge), Katavi (128.513), Njombe (120.795) au Lindi (112.192).

Tofauti ni kubwa zaidi huko Zanzibar. Kwa mfano Wilaya ya Kaskazini B katika Mkoa wa Unguja Kaskazini ina wakazi 81,675[4] pekee lakini inachagua wabunge 4 katika majimbo ya Bumbwini, Donge, Kiwengwa na Mahonda.
Source: Bunge la Tanzania - Wikipedia, kamusi elezo huru.

Leo katika mchango wake wa Bungeni Mheshimiwa Kessy ameikumbusha NEC kupitia upya mgawanyo wa majimbo kwa kuzingatia idadi ya kata na watu kwa kila jimbo. Akatolea mfano wa baadhi ya Halmashauri kuwa na kata 10 na zingine kuwa na kata 30.

Kwa upande wangu naona ni vyema wazo hili likaangaliwa upya kwa vile sioni sababu ya kuwa na wabunge zaidi ya 390 kwa mgawanyo wa hivi sasa maana hata fursa ya kushiriki mijadala ya bungeni inakuwa hafifu.

Ninashauri kigezo kikuu kiwe ni kila wilaya iwe ni jimbo moja tu kama zamani. Mfano Tanzania Bara tuna wilaya kama 135 na zanzibar wana wilaya 10 tu ambapo ukiweka na wanawake angalaau unapata wabunge wasiozidi 200.

Naombeni michango itakayowezesha hili wazo liboreshwe na kufanyiwa kazi hata kama si kwa mwaka huu.

Hii itasaidia kupunguza gharama kubwa katika kuendesha bunge na pia itawezesha wabunge wachache kushiriki vyema katika mijadala Bungeni.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dhana ya Uwakilishi inakuwa na mashiko kama Wawakilishi wanatekeleza Majukumu yao kikatiba. Kutunga Sheria na kuisimamia serikali.

Lakini badala yake wanachofanya ni kutunga Sheria kandamizi dhidi ya raia, na kuiruhusu serikali iwasimamie. Yaani ni kama inawanyia collaboration policy ( inaungana na Wawakilishi kuwadefeat raia baada ya hapo wote wanakuwa under control ya Serikali).

Namna hii si ni bora mahitaji ya Wananchi yapokelewe kwa Mtendaji wa Mtaa/Kijijini afu yasukumwe mbele, afu zile hela wanazolipwa kwa kusign na kusinzia zielekezwe kwenye kutatua changamoto za Wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashauri viti maalum viwepo ila wagawane naeneo ya utendaji na mbunge mfano ubungo kwa kubenea tuna viti malum kadhaa iliwagawane hata kata au tarafa bila kujali vyama,maana kila mtu atakuwa na mawazo ya eneo fulani la kuwakilisha wananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna majimbo 214 Tanzania Bara na majimbo 50 Zanzibar.
  • Wabunge 264 waliochaguliwa katika majimbo ya uchaguzi
  • Wabunge 113 walioingia kupitia viti maalumu kwa wanawake
  • Wabunge 5 walioteuliwa na Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar
  • Wabunge 10 walioteuliwa na Rais wa Tanzania
  • Mwanasheria Mkuu
Majimbo yanatofautiana kwa kiasi kikubwa katika idadi ya wakazi. Wastani wa Tanzania bara ni mbunge mmoja kwa wakazi 227,461. [3] Kuna majimbo katika mikoa ambako mbunge mmoja anawakilisha watu wengi zaidi kama vile Dar es Salaam (wakazi 546,542/mbunge 1), Mwanza (346,999) na Kagera (309,953). Kinyume chake kuna majimbo mengine ambako mbunge anawakilisha watu wachache kama vile Pwani (wakazi 133.104/mbunge), Katavi (128.513), Njombe (120.795) au Lindi (112.192).

Tofauti ni kubwa zaidi huko Zanzibar. Kwa mfano Wilaya ya Kaskazini B katika Mkoa wa Unguja Kaskazini ina wakazi 81,675[4] pekee lakini inachagua wabunge 4 katika majimbo ya Bumbwini, Donge, Kiwengwa na Mahonda.
Source: Bunge la Tanzania - Wikipedia, kamusi elezo huru.

Leo katika mchango wake wa Bungeni Mheshimiwa Kessy ameikumbusha NEC kupitia upya mgawanyo wa majimbo kwa kuzingatia idadi ya kata na watu kwa kila jimbo. Akatolea mfano wa baadhi ya Halmashauri kuwa na kata 10 na zingine kuwa na kata 30.

Kwa upande wangu naona ni vyema wazo hili likaangaliwa upya kwa vile sioni sababu ya kuwa na wabunge zaidi ya 390 kwa mgawanyo wa hivi sasa maana hata fursa ya kushiriki mijadala ya bungeni inakuwa hafifu.

Ninashauri kigezo kikuu kiwe ni kila wilaya iwe ni jimbo moja tu kama zamani. Mfano Tanzania Bara tuna wilaya kama 135 na zanzibar wana wilaya 10 tu ambapo ukiweka na wanawake angalaau unapata wabunge wasiozidi 200.

Naombeni michango itakayowezesha hili wazo liboreshwe na kufanyiwa kazi hata kama si kwa mwaka huu.

Hii itasaidia kupunguza gharama kubwa katika kuendesha bunge na pia itawezesha wabunge wachache kushiriki vyema katika mijadala Bungeni.

Nawasilisha.
Naunga mkono hoja
 
Geografia isiwe kigezo cha kutenga majimbo kwa sababu:
1. Uzoefu unaonyesha wabunge wetu hawatembelei vijiji au mitaa yote. Wengi wana makazi Dar/Dom.
2. Kuna watendaji wengi kwenye wilaya, kama DC, DED, DAS, Afisa Tarafa, Mtendaji wa Kata nk. Hawa wote wanaangalia maendeleo ya wilaya/Jimbo. Kwa hiyo sio lazima Mbunge ndio awe anazunguka kila sehemu wakati kazi hizo zina watendaji.

Kama siyo lazima kuwatembelea Wananchi wao katika maeneo ya vijijini kisa tu wana makazi Dar/Dom basi hakuna haja ya Wabunge huku Vijijini, wabaki huko huko mjini.

Iweje kwenye kamepni aweze kufika kila kona ya Kijiji afu kwenye utekelezaji wa majukumu yake Kijiji kisiwe sehemu yenye ulazima kufikiwa?

Au wakati wa Campaign hao RCs, DCs, DEDs, Afisa Tarafa, Watendaji wa Kata na Vijiji/Mitaa huwa hawapo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Good idea
Ondoa kwanza wabunge viti maalum.
Wabunge 150 wanatosha kabisa 20 Zanzibar na 130 bara. Kati ya wabunge hao nusu ya wabunge wewe wanasheria.
Lakini yote haya hadi katiba mpya,tutazidi kubebeshwa mizigo na waganga njaa.

2020
 
Mkuu suala labuwakiliahi ninji si mnavyoamua number Tu. Uwingi au uchache hauathiri uwakilishi.
Kupunguza wabunge ni kupunguza kiwango cha uwakilishi wa wananchi bungeni.

1. sikubaliani na hoja ya wilaya kuwa ndiyo majimbo ya uchaguzi sababu kubwa ni moja kuna wilaya zingine geografia yake siyo rafiki kwa kuwa na mbunge mmoja tu achilia mbali kigezo cha watu.

2. Hatuwezi kukwepa gharama katika demokrasia ni lazima tukubaliane na hili kuwa demokrasia ni gharama hivyo lazima tuubebe huo mzigo

3. kama tunataka kupunguza gharama katika bunge ni vema tukaangalia kiwango cha mishahara, posho na viinua migongo wanavyolipwa wabunge ni kubwa sana tujaribu kupunguza hapa hii kwanza itasaidia kuondoa wajasiriasiasa bungeni na kuleta watu wenye nia ya dhati ya kuongoza watu.

4. Njia nyingine tufanye ugatuzi wa madaraka kwa viongozi wa wilaya na mikoa kuchaguliwa na wananchi badala ya kuwa na viongozi wengi ambao kimsingi wanatekeleza kazi zinafanana huko TAMISEMI. walau kama tukifanya hivi hoja yako ya kupunguza wabunge itakuwa na nguvu kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app

2020
 
Back
Top Bottom