Mgao wa umeme waanza rasmi Bukoba

Mgao wa umeme waanza rasmi Bukoba

washwa washwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2012
Posts
1,613
Reaction score
728
Wadau kuanzia leo mgao mkali wa umeme umeanza Bukoba.Muda wa mgao ni kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni kwa muda wa wiki 40. Ikumbukwe kuwa umeme unaotumika Bukoba unatoka Uganda na Museven ni swahiba wa Kagame. Ni afadhali hizo bifu zao wakazimaliza kwa kuwa wanaoumia ni wananchi na uchumi utaathirika kwa kiasi fulani.
 
Hivi kweli tumefika huko? Kati ya mkoa ambao haujawahi kuonja adha ya mgao wa umeme ni Kagera hasa Bukoba mjini. Siamini kama tumefika hapo.
 
ukimya wa Tanesco utasababisha speculations - au pengine wameshindwa kuilipa Uganda. Museveni huku ni kwao hawezi weka roho mbaya kiasi hicho. Sema tumezoea kuweka bajeti zisizotimilizika wala kutekelezeka. Zambia ilikuwa hivyo2. Biashara na Uswahili ni vitu viwili tofauti kabisa
 
''Yeye siyo mvua akanyeshe mto Kagera'' ...hivihivi kimasihara JK anachekelea hapa nchi ilipo.
 
Nimeona wachache wetu hapa jf tokea mkoa huo wanashabikia vita na mwendekezo wa mgogoro huo. Wamesahau kuwa wanakata mti waliokalia. Waathirika wa mgogoro huo ni Kagera na viunga vyake...dar/bagamoyo baadae sana. Tuna haki yakushinikiza kumalizwa kwa mgogoro huo kidiplpmasia. JK ametumia hasira kufurusha wahamiaji na bado wapambe wake wanachochea mgogoro huo visivyo.
 
Du! Hiyo kali. Wiki 40 si karibia mwaka mzima?
 
Mara nyingine huwa najiuliza,hivi nchi hii inasonga mbele au inarudi nyuma?ukiangalia kwa umakini utaona tunapoteza zaidi kimaendeleo kuliko kupata(gaining)!
 
Niliona Tangazo la TANESCO kuwa kuna matengenezo upande wa Uganda. Sasa nikawaza 40weeks? Kama miezi kumi hivi! Matengenezo ya wiki kumi!
 
Alafu najiuliza hivi hii ishu ilianza baada ya mabasi mawili kutekwa kule Kagera,sasa je,JK alilenga kudeal na wezi na watekaji ama alilenga kuwaondoa wasio raia wa Tz? hivi ni vitu 2 tofauti na vina approach mbili tofauti,kwanini kama ni watu kurudi kwao haifati diplomasia balozi zikakaa watu wakrudi kwa amani? hii ni ghasia na kuhatarisha amani ya watz walioko maeneo husika
Sikatai lakini kwa hili JK analeta matatizo kanda ya ziwa kama hivi kukata umeme,akafanye kwao B/moyo vinginevyo arudishe mahusian
 
Nimeona wachache wetu hapa jf tokea mkoa huo wanashabikia vita na mwendekezo wa mgogoro huo. Wamesahau kuwa wanakata mti waliokalia. Waathirika wa mgogoro huo ni Kagera na viunga vyake...dar/bagamoyo baadae sana. Tuna haki yakushinikiza kumalizwa kwa mgogoro huo kidiplpmasia. JK ametumia hasira kufurusha wahamiaji na bado wapambe wake wanachochea mgogoro huo visivyo.
Mgao wa umeme tu mmeanza kupoteza uzalendo, nyinyi ni sawa na wazimbabwe wa Tsavangrai au wayahudi wa Musa waliolilia masufuria ya nyama za utumwani?
 
Hivi kweli tumefika huko? Kati ya mkoa ambao haujawahi kuonja adha ya mgao wa umeme ni Kagera hasa Bukoba mjini. Siamini kama tumefika hapo.
Chakuazima hakisitiri ------. Kama Songea wanatumia umeme wa genereta, basi hata kagera wepelekewe waachane na kuazima kwa jirani.
 
Mimi nimefanya kazi serikalini hapo Bukoba mjini sikuwahi kusikia tatizo kubwa la umeme kama hili.
Umeme ukikatika masaa mji mzima unahamaki!!
Sababu ya tatizo ni vizuri ikajulikana!!!
 
Wadau kuanzia leo mgao mkali wa umeme umeanza Bukoba.Muda wa mgao ni kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni kwa muda wa wiki 40. Ikumbukwe kuwa umeme unaotumika Bukoba unatoka Uganda na Museven ni swahiba wa Kagame. Ni afadhali hizo bifu zao wakazimaliza kwa kuwa wanaoumia ni wananchi na uchumi utaathirika kwa kiasi fulani.
Ni kweli uchumi utaathirika lakini lazima muwe wajasiri, muache kulialia maana bila kumuondoa huyo jirani yenu yatajirudia tena ya idd amin, achilia mbali na hao waliokuwa wanawalazimisha msafiri kwa escort ya polisi.
 
Du! Hiyo kali. Wiki 40 si karibia mwaka mzima?

Hii itakuwa mpango maalum wa kuidhoofisha Bukoba.. haingii akilini matengenezo yachukue miezi kumi.. Nadhani serikali (kama inajielewa hata kiduchu) inatakiwa iliangalie hili kwa makini
 
Du! Hiyo kali. Wiki 40 si karibia mwaka mzima?

Hii itakuwa mpango maalum wa kuidhoofisha Bukoba.. haingii akilini matengenezo yachukue miezi kumi.. Nadhani serikali (kama inajielewa hata kiduchu) inatakiwa iliangalie hili kwa makini
 
Sie tunaotokea kule kwenye maeneo husika hatupingi wanyarwanda kurudi kwao hoja hapa ni mikoa husika tunataka yafuatayo;
Usalama wetu,kama ishu ni kuwatoa jamaa hawa kwa shari alafu baadae waanze kurudi na kufanya uhalifu watakaoumia ni sisi wa pale na si mtu kutoka Tanga,Morogoro ama Singida, tunataka ulinzi wa uhakika wa masaa 24
Pili,kwa vile mgogoro huu unaanza kuathiri hata umeme tunaitaka serikali itimize wajibu wake ilete majereta walau mgao huu upungue ama sivyo mkoa ule mnauangamiza.
 
Maamuzi yoyote magumu huwa yana gharama zake, lakini suala zuri kwenye maamuzi magumu ni kwamba ni maamuzi ambayo yanakupeleka kwenye heshima na mafanikio, sasa swali la kujiuliza kwa mtu yoyote yule anayetaka kuchukua maamuzi magumu ni kwamba, je uko tayari kuzikabili gharama zake ? na suala hili wakati mwingine linahitaji ujitoe kwelikweli na wakati mwingine linaweza hata kukukatisha tamaa kwa kufikiria kwamba labda uamuzi huo ulioufanya sio sahihi kutokana tu na gharama zitakazokuwa zinakukabili, lakini kitu kizuri ni kwamba wahenga walisema kwamba : ''Ukiona usiku unakolea ujue asubuhi inakaribia''. Sasa swali la kujiuliza ni kwamba : Je ni wazalendo wangapi wa nchi yetu ambao wako tayari kulivulimia giza hili totoro la usiku ili kuingojea asubuhi ? Wakati mheshimiwa rais wetu Jakaya Kikwete alipokuwa anatolewa maneno ya kejeli na dharau toka kwa viongozi wa Rwanda na vyombo vya habari vya nchi ya Rwanda (nukuu taarifa mbalimbali za vyombo vya habari) naamini kwamba watanzania wengi waliumia kusikia maneno haya ya kejeli na ya dharau hasa ukizingatia kwamba utamaduni wa mtanzania mara nyingi unamfanya kumheshimu mtu mwingine yoyote na hasa mtu huyo anapokuwa mgeni kutoka nchi nyingine. Ile ilikuwa ni dharau ambayo watanzania wengi hawakuitegemea na naamini kwamba mpaka leo hii wapo atu ambao hawaamini maneno yale yalisemwa. Ndio hawaamini, lakini ukweli utabaki kuwa ukweli, Rais wetu amekejeliwa na kudharauliwa na hii ni kejeli na dharau kwetu sisi wote watanzania. Kinachotuponza sisi ni utamaduni wetu wa kuheshimu utu na udugu kati ya watu, hili sasa naweza kutamka wazi kwamba ni KOSA, hili ni kosa na limetugharimu na litaendelea kutugharimu kama tusipoamua kuliacha na kuchukua maamuzi magumu. Tumeanza kuchukua maamuzi magumu lakini kama ilivyo maamuzi magumu yoyote yana gharama, itakapofikia kuanza kulipa gharama hizo inatubidi tuwe tayari kwani faida za maamuzi haya magumu ni kubwa kuliko gharama hizo ambazo tunatakiwa tuzilipe. Gharama hizi ni za muda tu na wala zisitukatishe tamaa. Gharama hizi zimewekwa na maadui zetu ili watukatishe tamaa, lakini hata wao wanajua kwamba baada ya muda fulani gharama hizi zitakuwa hazina maana tena, lakini kitu kitakachotusaidia kuzikabili gharama hizi ni UZALENDO, uzalendo wa wananchi katika kuzivumilia na kutafuta mbinu mbadala na uzalendo wa viongozi katika kuwawezesha wananchi kuzikabili gharama hizi huku suluhu ya kudumu ikitafutwa, narudia tena kusema kwamba KITU KITAKACHOTUSAIDIA KUZIKABILI GHARAMA HIZI NI UZALENDO, watanzania tunatakiwa tufahamu kuwa tunapita katika moja ya vipindi vigumu katika nchi yetu na kitakachoweza kutusaidia kupita katika kipindi hiki kigumu ni UZALENDO KWA NCHI YETU.

Kwahiyo sitegemei wakazi wa mkoa wa Kagera waanze kulialia kuhusu suala la mgawo wa umeme, waelewe kwamba ndio wanaanza hivyo kulipia gharama za maamuzi magumu kama itakavyokuwa kwa Watanzania wengine wote nchini.
Kwani mlifikiri kwamba Rais Paul Kagame aliposema kwamba muda sahihi ukifika atampiga Rais Jakaya Kikwete (''when the right time will come i will hit him'') mlifikiri kwamba atampiga kwa ngumi za mikono yake ?, je mlishawahi kuona maraisi wa nchi wakipigana ngumi hadharani ?
NAOMBA KUWASILISHA.
 
kwa hiyo mnataka umeme kwa gharama ya kuachia wahamiaji haramu wazaliane nchini? badala ya kuishinikiza serikali yetu ilete umeme wetu, nyie mnalilia wa wenzenu akili gani hii!
 
Back
Top Bottom