Mgao Fedha za IMF kwa Afya umejaa upendeleo

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,240
4,466
Kwanza niipongeze serikali kwa investment kubwa ya Afya kupitia hizi pesa za IMF, japo pia tungeweza ongeza zaidi kwa sababu sehemu kubwa ililenga kwenye afya.

Pamoja na hayo yote huu mgao ulipashwa uzingatie mgawanyo wa kikanda. Kuna sehemu miaka na miaka hawakuwa na huduma za CT scan wala MRI. Huduma zote hizi zipo Arusha, Dar, Dodoma, Kilimanjaro na Mwanza.

Unapeleka mashine 4 za MRI
Muhimbili, Hospitali ya Kanda ya Mtwara, Ocean Road na Hospitali ya Kanda Chato. Wale wa Chato si ipo jirani Bugando? Hiyo hospitali ya Kanda Mtwara, kwanini nao wasianze na CT Scan kwanza? Wana wataalamu wa hizo mashine? Kwanini mnaongeza Muhimbili MRI na CT scan wakati wanazo na wakati huo huo mnataka madaktari wapunguze kuwatuma wagonjwa kwenye Muhimbili na hivyo mambo yaishie hospitali za Mkoa na Kanda?

Hivi inaleta mantiki, mgonjwa kutumwa toka Rukwa ambako kuna CT Scans halafu anaenda Hospitali ya Mbeya ambako kuna CT scan tena ndogo sana na hapo hapo, madaktari wanamtuma akafanye MRI Muhimbili au Dodoma. Nasikia Mbeya hata CT scan waliyonayo walipewa na Wamarekani. Na ati miaka na miaka wameahidiwa kupelekewa MRI kupitia mradi wa Oriomi, lakini hola. Lakini hivi kupeleka CT scan kila mkoa mna radiologists wangapi kwenye hizo hospitali? Tunaweza kuziendesha?

Mashine za kuzalisha Oksijeni zote mwajaza hapa Dar es Salaam (Lugalo, Bugando, Serengeti, Tarakea, Ngorongoro, Nyasa, Masasi, Mzena na Polisi kilwa road). Wale ndugu zetu wagonjwa wanaopelekwa Hospitali zetu za kanda watatibiwa na nini kama hazina Oksigeni ya kutosha? Mbona hatujaona KCMC wakipata oxygen wakati juzijuzi tu mtambo wao ulizidiwa na ilikuwa ndio habari? Bugando wana mtambo wa kutosha? Mtwara? Mbeya? Benjamin Mkapa?

Ndio ubaya wa kuwa na miradi ya ghafla, watu hawakujipanga.
 

Attachments

  • MPANGO WA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA SEKTA YA AFYA KUPITIA MKOPO WENYE MASHARTI NAFUU KUTOKA SH...pdf
    24.3 MB · Views: 12
Wewe Mimi mkoa wangu staki CT scan ije wapeleke mikoa wanayoumwa

Mleta mada una shida wewe waweza kuwa mmoja unayejidai ohh Mimi sitibiwi Tanzania natibiwa Ulaya na Marekani utafikiri kuugua Ni Sifa.Oh Mimi nikikohoa tu ndege inakuja kunibeba kunipeleka Ulaya!! Kama kuumwa Sifa!!!


Hiyo Mi CT scan waipeleke mikoa ambayo kutwa wanaumwa kuanzia kipindupindu Hadi kaswende
 
Back
Top Bottom