Mganga wa jadi awania kiti cha Rostam ubunge jimbo la Igunga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mganga wa jadi awania kiti cha Rostam ubunge jimbo la Igunga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makaayamawe, Nov 6, 2009.

 1. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mganga wa jadi awania kiti cha Rostam ubunge jimbo la Igunga


  Nora Damian na Ellen Manyangu, Date::11/5/2009

  MGANGA mmoja wa jadi, ametangaza azma ya kuwania ubunge katika Jimbo la Igunga, mkoani Tabora, ambalo kwa sasa linawashikiliwa na Rostam Aziz.

  Mganga huyo Bakari Nyorobi (26) maarufu kama Profesa Vibuyu, alitangaza azma hiyo jana, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

  Alisema atagombea nafasi hiyo kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho Rostam pia ni mwanachama wake.

  Nyorobi alisema hakuna mapungufu yoyote aliyoyaona kutoka kwa Rostam na kwamba azma hiyo inatokana na utashi binafsi na si vinginevyo.

  “Mimi sijatumwa na mtu yeyote ila ni utashi wangu mwenyewe, nataka niendeleze yale aliyoyaanzisha Rostam,”alisema Nyorobi.

  Alisema pamoja na mambo mengine kilichomsukuma zaidi kugombea ubunge katika jimbo hilo ni kutaka kuleta nguvu mpya katika ulingo wa siasa hasa kwa kuzingatia kuwa Rostam amekuwa akiwawakilisha watu wa Igunga tangu mwaka 1994.

  Alisema sababu nyingine zilizomfanya awanie nafasi hiyo ni kutaka kuwaletea maendeleo wananchi wa Igunga.

  Huku akionekana kuzidiwa na maswali kutoka kwa waandishi wa habari, mganga huyo alisema alianza siasa miaka 12 iliyopita akiwa kada wa CCM.

  Alipoulizwa kuhusu elimu yake alisema alisoma hadi kidato cha sita lakini alishindwa kutaja shule aliyosoma.

  “Nikiwa kama mtaalamu wa tiba za asili nataka kutumia nafasi hii kushiriki kikamilifu na kuleta mawazo mapya bungeni kuhusu namna ya kupambana na mauaji ya kikatili kwa albino,”alisema. Nyorobi aliwaomba wakazi wa Igunga kumuunga mkono wakati harakati za uchaguzi zitakapoanza.
   
Loading...