Mganga kumrejesha Kaseja, Simba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mganga kumrejesha Kaseja, Simba

Discussion in 'Sports' started by Pdidy, May 23, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,336
  Likes Received: 5,648
  Trophy Points: 280
  Mganga kumrejesha Kaseja, Simba

  Burhani Yakub,Tanga.

  MWANAMICHEZO maarufu nchini na mpenzi wa klabu ya Simba,Profesa Maji Marefu amejitolea kumlipa mshahara wa Sh 1.5 milioni kwa mwezi mlinda mlango wa Yanga, Juma Kaseja endapo atasajiliwa Simba.

  Taarifa hiyo ilitolewa jana na mwenyekiti wa matawi ya Simba ya Tanga, Mbwana Msumari ilieleza kuwa hiyo ni ahadi ambayo ameitoa Maji Marefu.

  Alisema iwapo kamati ya usajili ambayo iko chini ya uenyekiti wa Kassim Dewji, itakubali maombi ya wanachama wa Tanga na maeneo mengine nchini, yeye (Maji Marefu) atakuwa tayari kumlipa mshahara wa kila mwezi ili mradi arejee na kuichezea klabu hiyo.

  "Maji Marefu ni mlezi wa matawi ya Simba yaliyoko Tanga, amefurahishwa na maombi tuliyoyatoa juzi kumtaka Kaseja na ameniomba nitangaze azma yake ya kumlipa mshahara iwapo atasajiliwa na Simba, "alisema Msumari.

  Alisema Maji Marefu ambaye anaishi Nairobi, Kenya alimpigia simu jana mchana akimuomba atangaze azma hiyo ili uongozi wa Simba utilie mkazo.

  Kwa mujibu wa Msumari, baada ya kupigiwa simu hiyo na kuelezwa hilo aliwasiliana na makamu mwenyekiti wa Simba,Omari Gumbo ili afikishe taarifa hiyo kwa kamati ya usajili.

  "Siyo kwamba tunamg'ang'ania Kaseja, bali ukweli ni kuwa Simba ndiyo iliyomtengeneza hadi kufikia kiwango hicho,sasa sisi kama wanachama hatuoni raha kuona akiinufaisha timu ya mahasimu wetu,"alisema.
   
 2. O

  Ogah JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Huyu Maji Marefu si alishakufa huyu....au?
   
Loading...