Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,138
mganga-pic.jpg

Mzee mmoja Salum Mchilowa (kushoto) akimfanyisha mazoezi mgonjwa Ally Said aliyevunjika Mguu Kwa ajali ya pikipiki Mtwara Mjini. Picha na Florence Sanawa

Mzee mmoja mkazi wa Kijiji cha Kilomba, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ambaye ni mganga wa tiba asilia, Salum Mchilowa amesema kuwa amekuwa akitibu watu waliovunjika mifupa kutokana na ajali mbalimbali na wamekuwa wakipona kwakutumia miti shamba huku wengine wakimdhulumu malipo ya matibabu baada ya kupona.

Akizungumza na Mwananchi ilipomtembelea kijijini hapo, amesema kuwa wagonjwa wengi wamekuwa wakifika nyumbani hapo na kupatiwa matibabu na wanapona ndani mwezi mmoja mpaka miwili, huku baadhi wakionyehs ahali ya kutokuwa waaminifu katika malipo.

“Kuna siku alikuja mgonjwa aliyepata ajali alivunjika mkono mguu na kiuno nilijikuta nikitumia muda mrefu kumtibu kuliko wagonjwa wengine ambao hupata matibabu mwezi mmoja na kuruhusiwa lakini huyu alikaa kwangu kwa zaidi ya miezi miwili na hatimaye alipona kabisa,” amesema.

“Wateja wengi wananidhulumu ninawatibu wakidai kuwa hawana pesa, lakini wakipona hawanirudi wala hawanilipi na ukumbuke wakikaa hapa wanakula wanalala lakini malipo yamekuwa magumu hivyo nashindwa kukuza kliniki yangu,” amesema.

Ally Said (mgonjwa) Mkazi wa Mtwara Mjini amesema alipata ajali ya pikipiki na alivunjika mguu ambapo anapata matibabu.

“Nilipata ajali ya pikipiki nikavunja mguu mpaka sasa nna mwezi mmoja tu nikaja huku kupata matibabu, nimeshaanza kupata nafuu nimeanza kukanyagia mguu,” amesema Said.

Naye Fatuma Juma mkazi wa Mtwara anasema kuwa kwa muda mrefu amekuwa akiuguza mguu baada ya kudondoka wakati akimfukuza mtoto nyumbani.

“Nilikuwa namkimbiza mtoto nikadondoka nikavunja mguu ambapo nimehangaika sana lakini sijapata matibabu kwa miezi tisa lakini nilipokuja hapa nashukuru naendeleaga vizuri,” amesema Juma.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Mifupa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini, Lameck Moses amesema kuwa wapo wanaotumia tiba asilia wanapona, lakini baadaye wanarudi tena kwetu na ukiangalia unaweza kuta mfupa umeunga, lakini umeunga vibaya tunalazimika kuuvunja upya na kujaribu kuweka chuma.

“Mfano mtu akija hospitalini anakaguliwa kwa undani na magonjwa mengine kupitia vipimo vya CTSCAN na XRAY ili kuangalia kama katika angle tofuati kama kuna vipande vipande ama kuna sehemu nyingine zimeathirika ili upate matibabu ya jumla,” amesema Dk Lameck.

“Sawa zamani watu walikuwa wanafungwa wanapona miguu inaenda upande, lakini anatembea sasa wananchi wanapaswa kujua kuwa teknolojia imekua, tupo watalaamu wengi nchi hii hadi kanda ya kusini tupo na vifaa vipo, ni vyema ukipata ajali ufike hosptalini kwanza,” amesema Dk Lameck.

Chanzo: Mwananchi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom