Shine
JF-Expert Member
- Feb 5, 2011
- 11,481
- 1,372
Sehemu nyingi za jiji la dar es salam wape migambo walio wekwa na manispaa husika ili kuwaondo wafanya biashara wanaofanya biashara sehem zisizo rasmi cha kushangaza pindi migambo hao wanapopita sehem hizo zisizo rasmi wamekua wakipeana mikono na machinga hao na pindi utakapogoma kutoa kidogo kitu wanakukamata kuwa ulikua ukifanya sehem zilizokatazwa huku wakiachwa wale waliotoa kidogo kitu (rushwa), na sehem ambazo zimeshamiri ni kariakoo, posta na karume. Je ni serikali imewatuma wajitaftie mishahara? Hilo sijalijua bado je serikali hailioni hili? Na kama imeliona ni hatua gani wamechukua kwani ni muda mrefu naona vitendo hivi vikiendea, kwani ukiona wanavyochukua rushwa utadhani rushwa ni ruksa Tanzania. Je manispaa husika hazishangai migambo wapo kila sehemu na machinga hawaishi? Kama manispaa husika wameshindwa kufuatilia mgambo hao ni bora wawaache wajinafasi na biashara zao.
Wana JF hili mshaliona? Au mmeliona je?
Wana JF hili mshaliona? Au mmeliona je?