Mgambo Auawa Stand ya daladala Mwenge

Mgambo Auawa Stand ya daladala Mwenge

hawa mgambo nao wamezidi, hawana hata huruma kwani wamekuwa wakichukua vitu vya machinga na kwenda kuviuza , vyakula vya mama lishe na vya wakaanga chips na kuku wanakwenda kuvila na familia zao, sasa huo ni mwanzo tu kwani mara zote muosha huoshwa.
 
masikini pole sana kwa familia ya huyu mgambo..
mambo mengine ni ya kujitakia wewe unaebda kubomoa sehemu aanyopatia riziki mwenzio bila kujiandaa unategemea nini?
 
hawa mgambo nao wamezidi, hawana hata huruma kwani wamekuwa wakichukua vitu vya machinga na kwenda kuviuza , vyakula vya mama lishe na vya wakaanga chips na kuku wanakwenda kuvila na familia zao, sasa huo ni mwanzo tu kwani mara zote muosha huoshwa.


kwahiyo kama wamedhidi ndiyo wauwawe.? wapi utawala wa sheria?naomba wizara ya mambo ya ndani na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vifanye uchunguzi wa kina katika haya mauaji ya mgambo na wahusika wote wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria na hatua kali dhidi yao za kisheria zichukuliwe wakibainika kutenda kosa hilo la kinyama.
 
Takribani wiki moja iliyopita niliweka thread hii iliyokuwa na title "ubabe wa askari wa jiji hadi lini?".,ukiangalia kwa undani kilichotokea hapo mwenge ni matokeo ya hiki nilichokuwa nimekiandika..,marehemu alale mahali pema peponi.,Amen

Hii ni hoja binafsi....

Kwa kweli nasikitishwa sana na hili 'jeshi' la mgambo wa jiji.,sipingi uwepo wao kwani limetoa ajira kwa vijana wengi tu wa Tanzania.,kinachonikwaza mimi ni utendaji wao wa kazi, sina hakika kama wanapatiwa mafunzo ya kutosha ikiwa ni pamoja na hata basic knowledge ya sheria na haki za binadamu au ndio wanaokotwa tu hovyo hovyo na baada ya siku mbili tatu wanapewa magwanda na kuingia mitaani.
Hawa jamaa naona wao ndio wanakuwa kero badala ya kutusaidia kupunguza kero hapa jijini.,sina shaka kuwa ni mambumbumbu wa sheria ndiyo maana utendaji kazi wao una walakini sana hebu angalia jinsi wanavyowavamia wafanya biashara na kuwapora vitu vyao, ona jinsi wanavyobeba masufuria ya mama lishe na hata wasiyafikishe huko ofisi za jiji badala yake wanazunguka kona na kula chakula chote.,wale wanaozunguka na breakdowns ndio usiseme wananuka rushwa kupita kiasi.
Nahisi walioanzisha 'jeshi' hili hawakujipanga vizuri, ndio maana wala hawaheshimiki, inabidi waangalie upya hii kada ambayo naona ikitumiwa vizuri inaweza sana kusaidia walau kuwapunguzia mzigo polisi.,naomba tu Mungu wakuu wasijiloge wakawapa hawa jamaa bunduki tutaisha wote huku mitaani.
Nawasilisha.
 
masikini pole sana kwa familia ya huyu mgambo..
mambo mengine ni ya kujitakia wewe unaebda kubomoa sehemu aanyopatia riziki mwenzio bila kujiandaa unategemea nini?
FL1 mzima
Jamani hawa mgambo si huwa wanatekeleza amri tu ya mabosi wao? So wa kuwalaumu ni mabosi wa migambo na si wagambo wenyewe.

RIP Mgambo shujaa ulokufa ukitekeleza majukumu yako. Apewe nishani ya ushujaa kama yule askari aliyekufa pale Ubungo akiokoa pesa za NBC!
 
Serikali iwe Makini maana kila mwaka inazalisaha Wamachinga malaki sasa Baada ya Miaka kumi kutakuwa na Jeshi kubwa sana la Wamachinga na Hao Mgambo hawataweza kupambana


tutatumia jeshi na ffu baadala ya mgambo sasa
 
Back
Top Bottom