Mfunze Mwanao kujiajiri, mwambie maisha hayaanzi akiajiriwa, wasomi wakiwa wengi ajira zinakuwa chache

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
11,164
15,846
Sasa hivi sio watoto tu wanaolalamika kuwa hakuna ajira bali mpaka wazazi wa watoto hao wanalalamika ajira hakuna jambo ambalo linafanya familia nzima inalaumu tu mwanzo mwisho na hakuna anaezinduka hapo.

Ni bora aliyejiajiri akawa anapitia magumu wakati huu kuliko yule ambaye hana ajira kabisa wakati huu can you imagine the situation?

Hii ni kwa sababu mzazi alimjenga mwanawe tokea zamani kuwa soma upate ajira,soma upate ajira mwanangu.

Hii ni sumu mbaya sana kwa watoto mwisho wa siku mtoto anaona kuwa bado hajaanza maisha mpaka apate ajira kwanza,wakati maisha yanaanza unapojitambua na kuwa na malengo yako.

Kwa ambao wana ajira wakomae na ajira zao.

Mwambie mwanao sasa hivi wasomi wengi sana na ajira zinakuwa chache mno hasa katika mambo ambayo wengi wanasomea, kumbuka ukisoma H.R kuna mamia huko nyuma wamesoma kwa hiyo usitegemee kuwa wewe ni mtu muhimu sana uajiriwe wewe peke ako,pengine ukakosa jipange kisaikolojia.

Kiukweli maisha yanakoenda inaonekana kuwa watu wanashida sana na ajira kuliko hiyo ajira ilivyokuwa na shida na watu.

Bwana einsten aliwahi kusema kuwa : where there is a difficult,there is an opportunitiy.

usitake mambo rahisi rahisi tu alafu mafanikio yaje simple kana kwamba unafanya peke yako jambo hilo.

Watu ni wengi,wasomi ni wengi ajira ni chache sana.serikali yenye akili haiwezi kuwaajiri watu ambao hawana shida nao,haiwezi kuajiri watu ambao hata wasipokuwepo kazi zitaenda bila shida.hata wewe upo hivyo.

Mwambie mwanao maisha yanaanza akijitambua na kuwa na malengo na maisha hayaanzi akiajiriwa,mwambie hata akiwa shule ana haki ya kujiajiri na kuwa mjasiriamali.


Mtoto harithi ajira ya baba,mtoto anarithi biashara tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njia pekee ambayo serikali itafanya kupunguza wasomi wasiohitajika ni kutowaajiri wapambane na hali zao tu mtaani.

Sasa hivi wasomi wengi hawana ajira.hii inapelekea watoto walioko shule wawe na kazi moja tu ya kuondoa ujinga mana hskuna matumaini ya kuwa na ajira za kutosha kutokana na wimbi la wasomi wengi.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna sehemu rahisi kufungua biashara kama Tanzania, nashangaa sana wanaokaa ofisini wanalipwa vilaki moja au hata kamilioni, sasa kamilioni kwa mwezi unafanyia nini?

😅watu wamejiajiri wanapiga milioni kila siku wengine ambao hawapo vizuri angalau inaingia kila wiki profit hiyo ni ya kutumia. Uvivu mwingi sana
 
Hakuna sehemu rahisi kufungua biashara kama Tanzania, nashangaa sana wanaokaa ofisini wanalipwa vilaki moja au hata kamilioni, sasa kamilioni kwa mwezi unafanyia nini? watu wamejiajiri wanapiga milioni kila siku wengine ambao hawapo vizuri angalau inaingia kila wiki profit hiyo ni ya kutumia. Uvivu mwingi sana
Biashara ipi unafanya mkuu ?
 
Nilipomaliza chuo cheti changu nilikiona kama likaratasi tu lisilokuwa na msaada wowote ktika maisha yangu. Nikakifungia kabatini. Nimejiajiri na mpaka sasa sifikirii kuajiriwa.

Na lengo kubwa lilikuwa nikufanya biashara ntakayoachia watoto wangu au familia yangu endapo nikitoweka duniani hapa. Ajira hailishishwi jaman. Tuwaige waindi na waarabu waliopo hapa nchini.

Watoto wao wameenda shule ila mwisho wa siku unakuta wakisimamia makampuni au miradi ya wazazi wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna sehemu rahisi kufungua biashara kama Tanzania, nashangaa sana wanaokaa ofisini wanalipwa vilaki moja au hata kamilioni, sasa kamilioni kwa mwezi unafanyia nini? watu wamejiajiri wanapiga milioni kila siku wengine ambao hawapo vizuri angalau inaingia kila wiki profit hiyo ni ya kutumia. Uvivu mwingi sana

Motivational Speakers bana,ni shiiiiiiiiiiiida.
 
safuher,
Fikra zako si sahihi.

Mtoto hafundishwi kazi Kwa maneno matupu, mtoto hujifunza kwa kuiga. Huwezi kumwambia mtoto "ajira hakuna" wakati wewe mwenyewe umeajiriwa. Anza wewe kujiairi na mtoto ataiga tu, huna haja ya kumfundisha Kwa maneno (action speaks louder than words), asome asisome ataiga tu. Unatakiwa uwe "role model" wa watoto zako wawe vipi.

Halafu hiyo kauli unayosema ya "enstein" umeiandika ndivyo sivyo, hiyo kauli inasema "In the middle of every difficulty lies opportunity" na hata jina haliandikwi hivyo ulivyoandika wewe. Jina huanza na herufi kubwa. Ungeandika Enstein.
 
Hakuna sehemu rahisi kufungua biashara kama Tanzania, nashangaa sana wanaokaa ofisini wanalipwa vilaki moja au hata kamilioni, sasa kamilioni kwa mwezi unafanyia nini? 😅watu wamejiajiri wanapiga milioni kila siku wengine ambao hawapo vizuri angalau inaingia kila wiki profit hiyo ni ya kutumia. Uvivu mwingi sana
Unalinganisha na wapi?
 
Hakuna sehemu rahisi kufungua biashara kama Tanzania, nashangaa sana wanaokaa ofisini wanalipwa vilaki moja au hata kamilioni, sasa kamilioni kwa mwezi unafanyia nini? watu wamejiajiri wanapiga milioni kila siku wengine ambao hawapo vizuri angalau inaingia kila wiki profit hiyo ni ya kutumia. Uvivu mwingi sana
Baba wewe ndoo motivational speaker wa ukweli. Wafanya biashara Tz wote wngekuwa matajiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baba wewe ndoo motivational speaker wa ukweli. Wafanya biashara Tz wote wngekuwa matajiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wengi wazembe hawajui biashara, wangekaa wanasoma business wangeona wanachofanya ni upuuzi, wengi wana hela ila tatizo wanafanya biashara ileile hakuna innovation, mtu moja akifungua hardware shop wote wanaiga, unakuta mwisho wa siku mtaa moja una maduka 10 ya hardware na wote wana product zilezile, hapo unategemea uwe milliioinaire kivipi?

Wabongo wengi sio innovative na hapo ndipo wengine tunawala kichwa, anzisha biashara ambazo wengine kucopy ni ngumu mno, wanaofanikiwa kucopy hadi kuja kukufikia ni miaka ushafika mbali unabadiilisha business. Biashara is like war, you always have to stay ahead au wengine watakuua.
 
Halafu hiyo kauli unayosema ya "enstein" umeiandika ndivyo sivyo,hiyo kauli inasema "In the middle of every difficulty lies opportunity" na hata jina haliandikwi hivyo ulivyoandika wewe. Jina huanza na herufi kubwa. Ungeandika Enstein.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?

Sio Enstein, ni Einstein.

Ujinga ni ujinga tu, hakuna ujinga mkubwa na mdogo.
 
Back
Top Bottom