Mfungwa aliyekuwa akitamba mitaani Mwanza akamatwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfungwa aliyekuwa akitamba mitaani Mwanza akamatwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Msongoru, Sep 23, 2008.

 1. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2008
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Na Frederick Katulanda,Mwanza


  SIKU moja baada ya kubainika mfungwa aliyehukumiwa kutumikia kifungo jela miaka mitano kuwa nje, jeshi la polisi limeeleza kuwa limemtia mbaroni kijana huyo na kwamba, anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Kirumba jijini Mwanza.


  Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jamal Rwambow alisema kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa na kwamba, anashikiliwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kesi hiyo.


  Kamanda Rwambow ambaye wakati akizungumza na simu na gazeti hili alikuwa safarini kuelekea wilayani Ukerewe, alisema amepigiwa simu na ofisa msaidizi wake Khamis Bhai na kumueleza kuwa mfungwa huyo amekamatwa jana.


  Kamanda alisema kutokana na maelezo hayo ameagiza kufanyika uchunguzi wa kina haraka kujua alitokaje ikiwa ni pamoja na kupitia nyaraka za mahakama pamoja na zile za jeshi la polisi ili kujua alitoka vipi.


  “Nimepigiwa simu na msaidizi wangu na amenieleza kuwa wamemkamata, sasa nimewaagiza kuwa wamshikilie na wampeleke mahakamani Jumatatu ili kufanya uchunguzi kujua alitoka vipi, sasa kwa vile niko safarini sina maelezo zaidi nadhani Jumatatu nitakuwa na cha kueleza” alisema Kamanda Rwambow.


  Hata hivyo uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, katika kujinusuru na kuwa nje kwa mtuhumiwa huyo tofauti na maelekezo ya kamanda, maofisa wa polisi katika Kituo cha Polisi Kirumba ambako anashikiliwa mfungwa huyo wameandika maelezo upya ya mfungwa huyo na kumshinikiza kueleza kuwa yuko nje kwa dhamana na kwamba, kesi yake ilikuwa ikiendelea mahakamani.


  Habari zilizopatikana kutoka kituoni hapo zinadai kuwa sambamba na mfungwa huyo pia mlalamikaji ameitwa kituoni hapo na kutakiwa kutoa maelezo upya kwa madai kuwa kesi hiyo itafikishwa mahakamani Jumatatu kwa ajili ya shauri lao kuendelea kusikilizwa.


  Hatua hii inazidi kudhihirisha kuwepo kwa njama za maofisa hao wa polisi kutaka kujinusuru na njama zao za kumwachia mfungwa huyo, kama ambavyo iliripotiwa jana na gazeti hili.


  Katika habari hiyo ilielezwa kuwa mtuhumiwa huyo Peter Ideka wa kesi namba 78/2008 ambaye ni fundi redio katika mtaa wa Kilimahewa yuko nje akiishi bila ya hatua zozote kuchukuliwa kutokana na maofisa wa jeshi la polisi kupanga njama siku ya hukumu yake hivyo kutomkabidhi kwa maofisa wa magereza kutumikia kifungo hicho.


  Kesi hiyo ilihukumiwa Julai 25 mwaka huu, mbele ya hakimu mkazi E. Mpuya wa mahakama ya wilaya ya Mwanza ambapo mtuhumiwa alihukumiwa kutumikia miaka saba jela kutokana na kupatikana hatia ya kumshambulia mteja wake Godfrey Makasi aliyekwenda kumdai radio yake aliyopeleka kutengenezwa baada ya kukiri kosa mbele ya mahakama na kuomba kusamehewa ambako alipunguziwa adhabu hadi miaka mitano.
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  heeeeeee sasa hapo ni kimeo mpiganaji Rwambow kazi unayo kusafisha jeshi lako pande hiyo....hii ni aibu sasa....no coordination hadi mtuhumiwa hajulikani kama yuko nje au amefungwa na hukumu imeshapita?hapo kuna kitu jamani
   
 3. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2008
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sio kwa Rwambow tu, ishu inaanzia juu yake na inawachanganya wote, Polisi na magereza!
   
Loading...