Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Juni, 2016 umeongezeka hadi 5.5% kutoka 5.2% mwezi Juni


Donatila

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Messages
3,092
Likes
4,071
Points
280
Age
28
Donatila

Donatila

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2014
3,092 4,071 280
2-jpg.364483


Mfumuko wa bei wa Taifa wa mwezi Juni, 2016 umeongezeka hadi asilimia 5.5 kutoka asilimia 5.2 mwezi uliopita kutokana na kuongezeka kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephaim Kwesigabo amesema kuongezeka kwa mfumuko wa bei kumesababishwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi.

“Mfumuko wa bei umesababishwa na kuongezeka kwa bei za vyakula kama vile mahindi ambayo yameongezeka kwa asilimia 3.2, unga wa muhogo kwa asilimia 2.4, samaki wabichi kwa asilimia 3.8, maziwa mgando kwa asilimia 4.3, maharage mabichi yaliyomenywa kwa asilimia 6.1, kitunguu swaumu kwa asilimia 12.5, njegere kwa asilimia 6.2, viazi mviringo kwa asilimia 2.5, mihogo mibichi kwa asilimia 6.7, magimbi kwa asilimia 4.5, na ndizi za kupika kwa asilimia 2.7,” amesema Kwesigabo.

Amesema bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi za bei ni pamoja na huduma ya kinywa na meno ambayo imeongezeka kwa asilimia 13.8, mafuta ya dizeli kwa asilimia 2.4 na mafuta ya petroli kwa asilimia 4.3. Kwesigabo amesema mfumuko wa bei wa mwezi Juni, 2016 unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.5 ongezeko sawa na mwezi uliopita.

Aidha amesema mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka wa bidhaa za vyakula majumbani na migahawani umeongezeka hadi asilimia 8.3 mwezi Juni, 2016 kutoka asilimia 7.2 mwezi Mei, 2016. Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 103.47 mwezi Juni, 2016 kutoka 103.00 mwezi uliopita.

Kwesigabo amesema uwezo wa Shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia Shilingi 96 na senti 65 mwezi Juni, 2016 kutoka mwezi Disemba, 2015.
 
Chizi Fureshi

Chizi Fureshi

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2010
Messages
1,710
Likes
141
Points
160
Chizi Fureshi

Chizi Fureshi

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2010
1,710 141 160
Sijui hesabu vizuri ngoja waje wenye eneo lao, ila mimi naendelea na yangu tu
 
iparamasa

iparamasa

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2013
Messages
13,461
Likes
14,158
Points
280
iparamasa

iparamasa

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2013
13,461 14,158 280
Wakija wañauchumi wa ccm watasema watasema watanzania walizoea hela za bure......ndio maana wanalia maisha magumu!!!
 
M

mwasu

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2011
Messages
8,497
Likes
6,546
Points
280
M

mwasu

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2011
8,497 6,546 280
Hapo napo tutaendelea kuambiwa maskini tumekumbukwa awamu hii, kazi ipo kweli tumekumbukwa ili tupige kelele na waheshimiwa waendelee kuburudika na mayowe yetu.
 

Forum statistics

Threads 1,237,681
Members 475,675
Posts 29,297,127