Mfumuko wa bei wa Taifa umepungua; Mafuta ya taa 16.6%, Dizel 4.2, Petrol 5.3

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575
takwimu.jpg

Mfumuko wa bei wa Taifa umepungua hadi asilimia 6.5 kutoka asilimia 6.8
Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini imetoa ripoti ya mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Januari,2016 ambapo umepungua hadi asilimia 6.5 kutoka asilimia 6.8 ilivyokuwa mwezi Desemba,2015.

Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa ya watu na takwimu za Jamii, Bw.Ephraim Kwesigabo amefafanua kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Januari,2016 kutoka 100.00 ambazo ni Fahirisi za mwezi Desemba,2015 zilizofanyiwa marejeo.

Hata hivyo amebainisha kuwa, kupungua kwa mfumuko wa bei wa mwezi Januari,2016 kumechangiwa hasa kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Januari,2016 zikilinganishwa na bei za mwezi Januari,2015.

Mkurugenzi huyo alizitaja bidhaa hizo zisizo za vyakula zilichongia kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na mafuta ya taa kwa asilimia 16.6, Dizel kwa asilimia 4.2, Petroli kwa asilimia 5.3 na bidhaa za elekroniki kwa asilimia 2.0.

TAKWIMU4.jpg

Kaimu Meneja wa Idara ya takwimu, Bi.Ruth Minja (kulia) akizungumza na wanahabari wakati wa mkutano huo mapema leo. kushoto ni Mkurugenzi wa Sensa ya watu takwimu za jamii, Bw. Ephraim Kwesigabo
 
Hujionei huruma? Kitu umekipost zaidi ya saa mzima hakuna mchangiaji?viwavi bwaana
 
Bado mfumuko upo tena mkubwa nilitegemea umeshuka hadi 3%
 
Takwimu hewa....huku site hatuoni tofauti kwenye consumer goods...bei ya sukari Leo na ilivyokuwa 6 months ago...no tofauti...
 
Asante kwa taarifa..achana na huyo mchangiaji wa kwanza,endelea kutupa taarifa hizi ambazo ni muhimu kwa mtanzania kujua mheshimiwa
 
Back
Top Bottom