Mfumuko Wa Bei Mwezi Huu

BowBow, et al:
Simenti imepanda bei kwa sababu inauzwa nje - Afrika Kusini kuliko na ujenzi wa viwanja, n.k; na DRCongo inapendwa sana kwa ubora wake.
Na kwa wenye viwanda, of course ni priority kwao ku-export kuliko kuuza kwa madafu, and there is nothing you and I can do about it!

..hiyo si sababu ya pekee. infact hiyo imechangia kuadimika,baadhi ya maeneo simenti.

..tatizo liko kwenye gharama za uzalishaji na usafirishaji!
 
ni kule kwetu zenji mpaka miguu ya kuku inauzwa kwa kilo sasa.

..inaonekana hiyo miguu inasoko sana. ila zenj si wafugaji hasa,wao hupenda kununua na hii ndo inapandisha bei za nyama huko!

natamani huyu rais naye tungekuwa tunapanga foleni pamoja pale darajani kununua mkate ili na yeye akaonja yale wanyonge wanayoyaonja.

..mkate upi yakhe?boflo au wa bakhresa?
 
Ni kweli bei ya cement Dar imepanda. Mimi nina shuguli ya ujenzi kwa wiki tatu sasa nilianza kununua mfuko kwa shs 15000/=. lakini kuanzia wiki iliyopita mpaka jana mchana nimekuwa nikinunua mfuko kwa shs 16000/= maeneo ya Yombo Vituka (karibu na Airport. Na bei hii ya shs 16000/= ilibadilika siku moja kutoka shs 15000/=.

..ndio,hata leo imesemwa kwenye radio!
 
..kwa wale tunaopenda biriani. mchele mzuri nao umeganda kwenye wastani wa 1000/= muda mrefu sasa!
 
Ibrah,
Umenifurahisha sana ulipojumuisha betri ktk vitu vyako maanake umenikumbusha kuwa Bongo kil mtu ana tochi yake na betri zinanunuliwa sana kuliko Umeme wenyewe. Ajabu kubwa nilipouliza kwa nini wanazo hizo tochi wakati kuna Umeme walinambia ebu tazama vizuri!... umeme upo majumbani tu hakuna mabarabarani kote giza!... na kweli barabara nyingi za miji yetu hazina taa za umeme..ati tunabana matumizi.
 
Ibrah,
Umenifurahisha sana ulipojumuisha betri ktk vitu vyako maanake umenikumbusha kuwa Bongo kil mtu ana tochi yake na betri zinanunuliwa sana kuliko Umeme wenyewe. Ajabu kubwa nilipouliza kwa nini wanazo hizo tochi wakati kuna Umeme walinambia ebu tazama vizuri!... umeme upo majumbani tu hakuna mabarabarani kote giza!... na kweli barabara nyingi za miji yetu hazina taa za umeme..ati tunabana matumizi.

..milingoti ya taa inaanza kufungwa baadhi ya maeneo hapa mjini. na zile za zamani zinawekwa taa mpya kama haziwaki.

..kama sikosei hili ni agizo la jk.
 
Tanzania Daima reports

HADI sasa hakuna chombo cha kudhibiti bei ya bidhaa zinapomfikia mlaji wa mwisho.
Kama chombo hiki kipo, basi ninaamini hakifanyi kazi yake!

Serikali inatangaza bei ya bidhaa kwenye bajeti ya kila mwaka.

Bei hizi zinatangazwa kwenye vyombo vya habari, wananchi wanasikika kwamba sukari ni bei fulani, mafuta ya taa ni bei fulani, soda ni bei fulani, lakini bei hizo zinabaki kwenye maandishi tu!

Kawaida mlaji wa mwisho anawekwa kitanzini na bei tofauti na ile iliyotangazwa na serikali. Ni wazi kuna gharama za usafirishaji. Bei ya mafuta ya taa ya Dar es Salaam, haiwezi kulingana na ile ya Karagwe. Lakini kwa serikali inayojali, bei hizi haziwezi kutofautiana sana. Mafuta ya taa ni muhimu Karagwe vijijini ambako hakuna umeme.

TRA inawabana wafanyabiashara kuhakikisha wanalipa ushuru, serikali inayojali ni lazima itoze ushuru.

Wakorofi wanaokataa kulipa ushuru wanatozwa faini, na kuna wengine wanaokubaliana na TRA kwa kulipa kitu kidogo na hatimaye anayeumia kwenye mzunguko huu wa biashara ni mlaji wa mwisho.

Katika makala hii, ningependa kumjadili mlaji wa mwisho wa kijijini. Huyu ndiye anayeumia zaidi, na Watanzania wengi wanaishi vijijini.

Tunaposema kwamba Watanzania bado ni masikini, mara nyingi tunawalenga hawa wa vijijini, Lakini jambo la kushangaza ni kwamba, hawa tunaowaita maskini ndio wanaokamuliwa zaidi bila huruma. Hawa ndio hawana mifumo ya kulinda ustawi wao.

Nitoe mfano wa Kata ya Kamuli, Tarafa ya Kituntu-Mabira, Wilaya ya Karagwe. Katika tarafa hii sukari kilo moja inauzwa shilingi 1,500 na inapanda kijiji hadi kingine. Maana yake ni kwamba unaweza kukuta kijiji kingine wanauza sh 1,800!

Wafanyabiashara wanaongeza bei kufidia ushuru na kila hasara inayojitokeza katika biashara yao, soda inauzwa kati ya sh 500 na sh 700, mfuko wa saruji ni sh 23,000 na kuendelea, inategemea saruji imetoka Uganda au hapa hapa nchini.
Chumvi kilo moja ni sh 1,200, sabuni mche ni sh 1,000, mafuta ya taa lita moja ni sh 1,500 hadi sh 1,700, petroli ni sh 2,000, mabati ni sh 12,500 kwa bati moja.

Nimetoa mfano wa Kata ya Kamuli, lakini ukizunguka Wilaya ya Karagwe, utashangaa jinsi bei hizi zinavyobadilika, kijiji hadi kijiji, kata hadi kata na tarafa hadi tarafa.

Wilaya hiyo hiyo, bei ya mafuta ya taa ni tofauti, bei ya chumvi ni tofauti, bei ya sukari ni tofauti nk. Kama tofauti ni senti au shilingi, ni jambo la kawaida, lakini tofauti inapozidi elfu moja, inakuwa hatari.

Inaonyesha jinsi wafanyabiashara wanavyoachiwa uhuru wa kufanya wanavyotaka wakati mlaji wa mwisho anaendelea kuumia na kudidimia!

Pia inaonyesha jinsi viongozi wa serikali kama mkuu wa wilaya, wasivyokuwa na muda wa kuzunguka kukagua maendeleo ya wananchi.

Wanapitapita kuhimiza michango ya kujenga sekondari za kata na zahanati huku wakifumba macho kwa mambo mengine kama hili la bei za bidhaa kupanda ovyo bila mpangilio.

Hata kama hakuna chombo kinachoeleweka cha kudhibiti bei, kiongozi anayejali, hawezi kuona bei za bidhaa zinawaumiza wananchi wake akakaa kimya! Vinginevyo kiongozi huyo hafai!

Kipato cha wananchi wa Kata ya Kamuli, kinategemea mazao: kahawa, maharage, mahindi nk. Kilo moja ya kahawa inauzwa kwa shilingi 700, maharagwe shilingi 700. Mkulima wa kawaida anaweza kupata kati ya kilo 200 hadi 300 za maharage na kahawa kwa mwaka.

Ukiangalia bei ya bidhaa nilizozitaja hapo juu, mkulima huyu anahitaji kilo ngapi za kahawa na maharage ili aweze kuishi maisha bora?

Hadi sasa serikali haijaonyesha nia ya kumsaidia mkulima kuboresha kilimo chake, wakulima wengi bado wanatumia jembe la mkono, wanalima mashamba madogo ambayo hayawezi kuleta mabadiliko ya haraka, na mipango ya kutoa mikopo kwa wakulima, kama ipo, basi haiko wazi.

Bei ya kahawa imepanda karibuni baada ya shinikizo la wanunuzi binafsi. Mbunge wa Kyerwa, amefanya jitihada za kuhakikisha bei ya kahawa inakuwa nzuri, ameonyesha nia njema ya kuwajali wakulima na wapiga kura wake katika Jimbo la Kyerwa.

Pamoja na jitihada hizo, bado kuna haja ya serikali kuingilia kati kuboresha kilimo cha kahawa na kuunda chombo cha kudhibiti bei ya bidhaa zinapomfikia mlaji wa mwisho.

Vinginevyo itakuwa vigumu wakulima wa vijijini kupata maisha bora. Watauza kahawa na kupata pesa nzuri, lakini pesa hizo zitaishia kwenye kununua bidhaa muhimu ambazo bei yake inapanda kufuatana na matakwa ya wafanyabiashara.

Huyu mkulima wa Kamuli, anayekabwa koo na wafanyabiashara, bado anawekwa kitanzini na michango ya serikali, kama vile michango ya sekondari za kata, zahanati, karo, matibabu, nk.

Huyu hana maji safi, barabara mbovu, hana umeme na wakati mwingine yuko mbali na hospitali. Kwa maneno mengine, huyu anahitaji mfumo wa kumsaidia kutunza kila senti, maana kila senti inayopotea kwake ni muhimu sana.

Hali hii inanisukuma kuishauri serikali kufikiria kuunda chombo cha kudhibti bei ya bidhaa zinapomfikia mlaji wa mwisho, kwa mfano bidhaa ambazo ni za lazima kwa maisha ya kila siku na zile zinazoboresha maisha ya mwananchi.

Mafuta ya taa, chumvi, sukari, sabuni nk. ni vitu muhimu sana kwa maisha ya kila siku hivyo bei yake isipodhibitiwa, wananchi wataendelea kuishi maisha magumu.

Saruji na mabati ni muhimu sana kwa kujenga nyumba bora na za kisasa. Je, kama bei ya mfuko wa saruji ni shilingi 23,000 watu watamudu kujenga? Na je, kama mabati ni shilingi 12,500 ni wangapi wataweza kujenga nyumba za bati?

Wafanyabiashara wasiachiwe huru kupandisha bei za bidhaa jinsi wanavyotaka. Ni lazima kuwabana! kuwepo na chombo cha kudhibiti bei kwa lengo la kumlinda mlaji wa mwisho.

Serikali ya Awamu ya Nne, imekuwa ikijielekeza katika kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania, hili ni jambo zuri na kila mtu anatamani hivyo, lakini ni ndoto kufikiria kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania bila mifumo mizuri kama vile kudhibiti bei ya bidhaa zinapomfikia mlaji wa mwisho.

Nimetoa mfano wa Kata ya Kamuli, lakini imani yangu ni kwamba maisha ya vijiji vyetu hapa Tanzania yanafananafanana. Nafikiri kilio hiki ni kilio cha vijiji vyote!

Maajabu!!!yaani mkulima kuweza kununua soda inamgharimu kahawa kilo moja. Kununua mfuko wa sementi inamgharimu karibu kilo 33 za kahawa yake; na bati moja kilo 18 za kahawa yake.

Kwa wale wanaoelewa kilimo cha kahawa wanajua gharama zake ndiyo maana wachaga waliamua kungoa mikahawa na kulima mazao mbadala kama mboga mboga na mazao mengine ili mradi mkono uende kinywaji kwani waliona umaskini umeongezeka kwa kasi.

Walipata upinzani mkali sana toka kwa watawala.

Kwa hii ya Karagwe ni kwamba hali ni mbaya na inatisha hivi.

What is the way forward kumkomboa huyu mkulima??
 
Mfwatiliaji:

Mada uliyotoa ni muhimu sana. Lakini kabla ya kutoa lawama ni lazima tuangalie mambo yafuatayo:-

1./ Waziri wa fedha alitoa taarifa ya kupanda kwa shilingi. Kwa watanzania wengi hili lilikuwa ni jambo la kufurahisha.

2./ Upandaji wa shilingi ulitokana na kuchuka kwa dollar ya marekani ambao unatokana na matatizo ya kiuchumi yaliopo sasa marekani.

3./ Bidhaa nyingi zipo PRICED in US dollar. Hivyo kushuka kwa thamani ya dollar kumewafanya wazalishaji wa bidhaa HOT HOT kama mafuta kuongeza bei ya bidhaa zao.

4./ Ongezeko la mafuta lime-TRIGGER ongezeko la bidhaa nyingine zinazotegemea usafiri kumfikia mlaji.

5./ Nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania zinaweka akiba zake katika dollar za Kimerekani au dhahabu. Kama miaka miwili iliyopita tulikuwa na akiba ya dollar billioni 2. Kwa sasa dollar hizo billioni 2 zitakuwa na thamani ya chini kama kuliko miaka 2 iliyopita.

Cha muhimu, Tanzania isiishi kama kisiwa. Na cha muhimu zaidi tuangalie athari za matokeo ya kidunia na uchumi wetu. Watu wamezungumzia mazuri ya kupanda kwa shilingi kulikotokana na kushuka kwa dollar. Vile vile ni muhimu kuangalia mabaya ya ukuaji huo.
 
Heshima mbele BM
duku duku langu ni kuhusu kudumaa kwa bei ya kahawa ya mkulima ambaye anaonekana waziwazi kukosa mtetezi.
Ndiyo maana nime-highlight bidhaa fulanix2 nikalinganisha na bei ya kahawa anayolipwa mkulima.
Hapa kuna biasness; Kwa nini bei ya kahawa idhibitiwe at the same time bidhaa nyingine zinaapaa? Hapa wajibu wa serikali ni upi?Serikali kazi yake kubwa ni check and balance,hata waanzilishi wa soko huria ndiyo kazi kubwa ya serikali zao. Iko wapi sasa hiyo check and balance hapa kwetu??Huo mfumuko wa bei unatisha ati.Wananchi wa kawaida hawataweza kumudu hayo maisha.Mimi binafsi yamenishinda.
 
..milingoti ya taa inaanza kufungwa baadhi ya maeneo hapa mjini. na zile za zamani zinawekwa taa mpya kama haziwaki.

..kama sikosei hili ni agizo la jk.

basi kama ni agizo la huyu mheshimiwa...ujue kuna ugeni mkubwa hivi karibuni hana lolote
 
abt inflation kichekesho ni kuwa ikitoka statement ya serikali n msela wake BOT tutaambiwa rate ya inflation imeshuka na hali ya maisha yazidi kuwa nzuri na ule mheshimiwa mwingine atazidi kuongezea chumvi kuwa ndege yetu ya maendeleo imeanza kukamatia run way tayari kwa kupaa!!
SHe NZy zao woooooote yani hawaoni hata aibu kudanganya wananchi hiviiiii jamani kwa speed hii ya maisha na gharama hizi mbona wa TZ watakufa kabla ya siku zao??!kama watu hapo dar wanalalamikia bei hizo wakuta ni watu wenye hata kazi za maana na je kule vijijini jamani ndugu zetu watasemaje??
jamani jamani kama wakuu wanasoma JF au hata kuadithiwa waonee huruma wa Tanzania
 
Heshima mbele BM
duku duku langu ni kuhusu kudumaa kwa bei ya kahawa ya mkulima ambaye anaonekana waziwazi kukosa mtetezi.
Ndiyo maana nime-highlight bidhaa fulanix2 nikalinganisha na bei ya kahawa anayolipwa mkulima.
Hapa kuna biasness; Kwa nini bei ya kahawa idhibitiwe at the same time bidhaa nyingine zinaapaa? Hapa wajibu wa serikali ni upi?Serikali kazi yake kubwa ni check and balance,hata waanzilishi wa soko huria ndiyo kazi kubwa ya serikali zao. Iko wapi sasa hiyo check and balance hapa kwetu??Huo mfumuko wa bei unatisha ati.Wananchi wa kawaida hawataweza kumudu hayo maisha.Mimi binafsi yamenishinda.

MFWATILIAJI:

Mimi ni mtazamaji tu ninayeangalia athari za kushuka kwa thamani ya dollar duniani na jinsi gani bei za bidhaa na akiba za nchi zinavyoweza kuwa mashakani.

Ni jinsi gani serikali inaweza kukabiliana na tatizo hilo? Hapo sina jibu au pendekezo lolote lile la maana.

Kwa sasa ninachoweza-speculate ni kuwa shughuli za kilimo cha mazao muhimu ya chakula kama mahindi, mchele, maharage n.k ziendeshwe katika industrial scale ili kuzalisha chakula cha bei nafuu na kuwa na akiba ya kutosha kuweza kuimili matatizo ya kiuchumi duniani. Hii itasaidia serikali kutoa ruzuku katika muundo unaoeleweka na kwa wachache.

Lakini kwa sababu tumehamua kuwa kilimo kitoe ajira kwa wengi, speculation yangu ya kuwa na uzalisha wa industrial scale in UWONGO MTUPU na vilevile inachangia UBEPARI kitu ambacho hatukipendei. Cha muhimu ni kuvumilia maumivu ya sasa kwa matumaini ya kuwa watu watazoea maisha hayo au kungojea mpaka bei za bidhaa zitakapojirekebisha zenyewe.

Na kuhusu wakulima wa mazao ya kahawa, inabidi watanzania wenyewe wachangamke.
 
Bei ya Soda jamii ya Coca cola nayo imepanda, jana nimenunua soda Sprite kwa shiling 350/- nikashituka maana wiki ilopita ilikuwa 300/- nikamuuliza muuzaji kwa nini ametupandishia akasema kuwa Soda imepanda!Leo asubuhi nimempa lifti jirani yangu ambaye ana duka nikamuuliza akanithibitishia kuwa bei ya Soda imepanda tangu Jumanne wiki hii.

So, bei ya Soda jamii ya Coca cola hapa Arusha ni Shilingi 350/- kwa chupa badala ya shilingi 300/-!
Tumetoka mbali haki ya Mungu😂😂
 
Back
Top Bottom