Wapendwa wana JF,
Najua kuna threads mbili zimo humu kuhusiana na Mfumuko wa Bei moja ikiwa imeanzishwa na Invicible na nyingine ikiwa imeanzishwa na Invisible. Hata hivyo nimeona ziko very general kwa hiyo nimefikiria kuwa ni vema tukawa na Thread ya kudumu kwa jina la "MFUMUKO WA BEI MWEZI HUU" ambayo kwayo tunaweza kufanya updates kila siku/wiki/mwezi na kila baada ya nusu mwaka tufanye tathmini ili tuweze kuangalia wapi tumetoka, wapi tupo na wapi tunakwenda.
Mwezi huu (Desemba 2007) vitu vifuatavyo vimepanda bei na nimegundua baada ya kufanya shopping wiki hii. Mimi mkazi wa Arusha nimegundua haya:-
1. Bei ya Gesi (LPG) ya kilo 40 imepanda kutoka shilingi 64,000/ (mwezi Julai) hadi shilingi 73,000/- mwezi huu wa Desemba!
2. Betri kubwa za Panasonic (Made in Tz) zimepanda kutoka shilingi 400/- kwa betri (Novemba) hadi shilingi 450/- mwezi huu wa Desemba.
3. Balbu za umeme za kawaida zimepanda kutoka shilingi 300/-kwa balbu (mwezi Novembea) hadi shiliongi 400/- kwa balbu mwezi huu wa Desemba.
4. Bei ya Mkate mdogo wa "Super loaf" imepanda kiasi cha kutisha kutoka shilingi 500/- mwanzoni mwa mwaka hadi 550/- katikati ya mwaka na sasa mwezi huu wa Desemba imefikia shilingi 600/-!
Ibrah,
Thanks- tupe source ya data. Je tunanaweza kupata % increse pia kwa kila mwezi au miazi mitatu?
N:B Vipi bei ya cement? Ni kweli Dar ni 16,000 na Mwanza ni 25,000 hadi 30,000?
Asante mkuu,
Source ya data zangu ni madukani ambapo nanunua bidhaa mara kwa mara. KWa mfano LPG (gesi) ya kilo 40 nimenunua juzi tu baada ya gesi yangu ya nyumbani kuisha, mara yangu ya mwisho kununua ilikuwa Julai ambapo nilinunua 64,000/-. Mkate ndiyo kitafunwa changu cha kifungua kinywa; betri kubwa natumia kwa ajili ya tochi (kila betri zikisha nguvu nanunua nyingine.
Kuhusu bei ya cement sina jibu lakini kesho nitawapostia hapa bei ya cement kwa hapa Arusha.
N:B Vipi bei ya cement? Ni kweli Dar ni 16,000 na Mwanza ni 25,000 hadi 30,000?
Inasikitisha kuona such a huge difference due to transportation costs.
Tutaendelea kujenga kwa muda mrefu sana.Kama raw materials za simenti zinaweza kupatikana locally tuwekwe investors wakujenga kiwanda kila kanda, hii itachochea ujenzi sana.
Tuna Dar for the east Tanga for the north east na Mbeya for the south, the west/ziwa needs one. Overtime kinaweza kujilipia kutokana na kupunguza gharama za usafirishaji.
Bei ya Soda jamii ya Coca cola nayo imepanda, jana nimenunua soda Sprite kwa shiling 350/- nikashituka maana wiki ilopita ilikuwa 300/- nikamuuliza muuzaji kwa nini ametupandishia akasema kuwa Soda imepanda!Leo asubuhi nimempa lifti jirani yangu ambaye ana duka nikamuuliza akanithibitishia kuwa bei ya Soda imepanda tangu Jumanne wiki hii.
So, bei ya Soda jamii ya Coca cola hapa Arusha ni Shilingi 350/- kwa chupa badala ya shilingi 300/-!