Mfumo wa usajili wa magari Tanzania

Mfumo wa usajili wa magari Tanzania

Mr pianoman

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2019
Posts
2,644
Reaction score
6,468
Watu wamekuwa wakijiuliza ni kwa nini kuna gari zina namba A, nyingine B, nyingine C, na nyingine D na muda si mrefu itaingia "E" japo kuna tetesi kuwa namba "E" imesha anza kutumika.

Sasa hizi namba zinakuaje mpaka zinabadilika kutoka A, kuja B, kuja C kuja D na sasa tunaelekea E

Ipo hivi, Tuchukulie mfano wa namba "D" tuliyo nayo sasa hivi ilipo anza kutumika gari yake ya kwanza kabisa kupewa usajili wa SERIES hii ya namba "D" ilipo anza ilikuwa ni (T 101 DAA.) hii ndio gari ya kwanza kisha gari ya pili ikaja (T 102 DAA) kisha gari ya tatu ikaja (T 103 DAA) ikaendelea mpaka gari namba (T 999 DAA).

Baada ya gari namba T 999 DAA tutakuwa tumemaliza series ya herufi DAA na kisha kuhamia series ya DAB yaani katika series ya DAB gari ya kwanza itakuwa ni (T 101 DAB)

Kumbuka katika Alfabeti A mpaka Z kuna herufi 26 lakini katika herufi hizo kuna herufi mbili hazitumiki katika mfumo wa kusajili Magari herufi hizo ni "I" na "O". Hizi herufi hazitumiki kwa sababu zinaweza kuwa namba pia. Kwa mfano "I" inaweza kusomeka moja (1) na "O" inaweza kusomeka sifuri (0). Hivyo hizo herufi zimetolewa na kubaki 24.

Hivyo basi kutoka series ya DAA kuna magari 899 yamesajiliwa ndio ikaja DAB. Yaani( T 101 DAA mpaka T 999 DAA ).

Hivyo ili tuingie kwenye DBA chukua 899x24 =21,576

Na ili tutoke kwenye namba D tuingie kwenye namba E chukua 21,576x24=517,824

517,824 hii ndio idadi ya magari iliyo kuwa inafika na mfumo kubadilika kutoka kwenye namba A kuja B kuja C kuja D na sasa muda si mrefu itaingia namba E.

Gari ya mwisho ya namba D Itakuwa ni T 999 DZZ na baada ya hapo itaingia
T 101 EAA. Baada ya kutimia gari 517,824 tutaingia T 101 FAA.

Kumbuka unapo kariri namba za gari either iliyo fanya tukio lolote la kuhatarisha usalama unashauriwa Kukariri namba zote kama zilivyo. Usikariri nusu.

Yaani kama ni gari namba T 574 DAA ikariri kama ilivyo usikariri namba za mwisho tu DAA. maana kwenye DAA kuna gari 899 zimesajiliwa kwenye hiyo herufi DAA.

nimejaribu kuelezea ila najua kuna wajuzi zaidi wataelezea. Karibuni
 
Watu wamekuwa wakijiuliza ni kwa nini kuna gari zina namba A, nyingine B, nyingine C, na nyingine D na muda si mrefu itaingia "E" japo kuna tetesi kuwa namba "E" imesha anza kutumika.

Sasa hizi namba zinakuaje mpaka zinabadilika kutoka A, kuja B, kuja C kuja D na sasa tunaelekea E

Ipo hivi, Tuchukulie mfano wa namba "D" tuliyo nayo sasa hivi ilipo anza kutumika gari yake ya kwanza kabisa kupewa usajili wa SERIES hii ya namba "D" ilipo anza ilikuwa ni (T 101 DAA.) hii ndio gari ya kwanza kisha gari ya pili ikaja (T 102 DAA) kisha gari ya tatu ikaja (T 103 DAA) ikaendelea mpaka gari namba (T 999 DAA).

Baada ya gari namba T 999 DAA tutakuwa tumemaliza series ya herufi DAA na kisha kuhamia series ya DAB yaani katika series ya DAB gari ya kwanza itakuwa ni (T 101 DAB)

Kumbuka katika Alfabeti A mpaka Z kuna herufi 26 lakini katika herufi hizo kuna herufi mbili hazitumiki katika mfumo wa kusajili Magari herufi hizo ni "I" na "O". Hizi herufi hazitumiki kwa sababu zinaweza kuwa namba pia. Kwa mfano "I" inaweza kusomeka moja (1) na "O" inaweza kusomeka sifuri (0). Hivyo hizo herufi zimetolewa na kubaki 24.

Hivyo basi kutoka series ya DAA kuna magari 899 yamesajiliwa ndio ikaja DAB. Yaani( T 101 DAA mpaka T 999 DAA ).

Hivyo ili tuingie kwenye DBA chukua 899x24 =21,576

Na ili tutoke kwenye namba D tuingie kwenye namba E chukua 21,576x24=517,824

517,824 hii ndio idadi ya magari iliyo kuwa inafika na mfumo kubadilika kutoka kwenye namba A kuja B kuja C kuja D na sasa muda si mrefu itaingia namba E.

Gari ya mwisho ya namba D Itakuwa ni T 999 DZZ na baada ya hapo itaingia
T 101 EAA. Baada ya kutimia gari 517,824 tutaingia T 101 FAA.

Kumbuka unapo kalili namba za gari either iliyo fanya tukio lolote la kuhatarisha usalama unashauriwa Kukalili namba zote kama zilivyo. Usikalili nusu.

Yaani kama ni gari namba T 574 DAA ikalili kama ilivyo usikalili namba za mwisho tu DAA. maana kwenye DAA kuna gari 899 zimesajiliwa kwenye hiyo herufi DAA..

Mods mnaweza kuediti uzi maana uandishi wangu sio mzuri sana.
HIVI KWELI ITAFIKA T 999 ZZZ SIJANUNUA GARI?
 
Asanteee kwa maana hiyo mpaka tulipofikia gari tulizonazo Tz nzima zinahesabika kama kutoka A series to D series huchukua laki tano
 
Shkrani kwa Elimu hii, walau nami nimetoa tongotongo maana nilikuwa naona mapicha picha tu
 
HIVI KWELI ITAFIKA T 999 ZZZ SIJANUNUA GARI?
Hilo tunakuachia mwenyewe

20211121_213457.jpg
 
Hiyo ni series bila shaka. Ila kwa nini namba zisianzie 001 na kuendelea? Kwa nini sio 100? Ni hayo tu.
 
Historia fupi:-

Usajili wa namba za magari (number plate) ulianza mwaka 1933 kwa upande wa iliyokuwa Tanganyika na mwaka 1950 kwa upande wa visiwa vya marashi ya karafuu na urojo (Zanzibar).
Ukubwa wake kwa wakati huo ulikuwa sawa na Uingereza mpaka miaka ya mwishoni ya 1980.

Tanzania Bara na Zanzibar wanatumia format tofauti za plate number kwenye Usajili wa magari.

Mwaka 1933, Tanganyika ilikuwa ikitumia vibao vyeupe na namba nyeupe. Namba zilianzia Dar es salaam DS zikifuatiwa na namba nne (Mfano DS 2150)

Mwishoni mwa miaka 1980, Tanzania ikaanza kutumua plate number za njano zenye maandishi meusi kwa magari binafsi, plate number nyeupe vyenye maandishi meusi kwa mabasi. Plate number zilianza kwa herufi ''T'' na kufuatiwa na herufi mbili na namba nne (Mfano TAA 1452)

Miaka ya 1990, plate number zikabadilika na kuanza na herufi T ikifuatiwa na herufi mbili lakini namba zikiwa ni tatu tu (Mfano TZL 524). Mfumo huu wa plate number ulifanana sana na mfumo unaoitwa FE-Schrift - unaotumika nchini Ujerumani.

Miaka ya 2000, kukawa na mabadiliko mengine ambapo plate number zikanza kutumia herufi T ikifuatiwa na namba tatu kisha herufi tatu kwenye sequence (Mfano T 109 ABB).

Huu ni mfumo wa plate number ambao ulitumika pia nchini Uingereza

mfano wa plate number ya Uingereza
1640162319225.png

mfano wa plate number ya Tanzania
1640162371725.png

Mabadiliko mengine ni kuwa gari za biashara zinatumia design hiyo hiyo lakini kibao kinakuwa cheupe na maandishi yanabaki kuwa meupe.

Mgawanyo wa namba:-

1. Plate number za magari ya Ubalozi, consular missions; zenyewe zinakuwa vibao vya kijani vikiwa na namba za njano ; huanza kwa herufi ''T'' ikifuatiwa na herufi tatu (kuwakilisha code ya nchi - 001 mpaka 255) ikifuatiwa na CD na namba tatu )
Mfano (T 105 CD 756).

2
. Plate number za magari ya UN pamoja na mashirika yake zenyewe, hizi inahusisha pia magari ya ofisi ya Benki ya Dunia ..nk hizi zinakuwa ni kibao cha blue na maandishi meupe

3042784_1640162757544.png

3. Magari ya serikali ; haya sasa yana namba tofauti kutegemeana na ofisi husika STK, SU, ST, JW, MT na kadhalika.

4. Vyombo vingine vya moto kama pikipiki na bajaji navyo vinausajili wake kwa design tofauti, ambapo Bajaji zinatumia MC 111 CKD

4. Zanzibar, mpaka miaka ya 1980 Tanganyika na Zanzibar tulikuwa tunatumia namba zinazofanana, baadaye namba za Zanzibar zikabadilika na kuanza kutumia vibao vyeupe na maandishi meusi huku ikianza na herufi ''Z'' ikimaanisha Zanzibar, ikifuatiwa na namba 3 kisha kumalizwa na herufi mbili.

Jambo la kuzingatioa ni kwamba kila kibao cha namba kipo tofauti kwa sababu maalumu.

Usichanganye kati ya kutumia jina kwenye kibao na kuweka namba. Kila gari lazima isajiliwe kwa mfumo rasmi kwanza kisha mbwembwe za kuweka kibao tofauti huja baadaye.

1640162757544.png
 
mfano wa plate number ya Uingereza View attachment 2053295

mfano wa plate number ya Tanzania View attachment 2053297

View attachment 2053304
Kuna wakati kulikuwa na namba za mikoa. Mmojawapo ni mfano DOM 125
 
Kumbuka katika Alfabeti A mpaka Z kuna herufi 26 lakini katika herufi hizo kuna herufi mbili hazitumiki katika mfumo wa kusajili Magari herufi hizo ni "I" na "O". Hizi herufi hazitumiki kwa sababu zinaweza kuwa namba pia. Kwa mfano "I" inaweza kusomeka moja (1) na "O" inaweza kusomeka sifuri (0). Hivyo hizo herufi zimetolewa na kubaki 24.
Hoja hii haina mashiko, kwani O ya kwenye keyboard ya computer inafanana na 0 kweli? Au I anafanana na 1, nani ameturoga? Pili kwa mfumo wa namba ulivyo kivipandevipande sidhani kama mtu hataweza kutofautisha sehemu ya namba (101) na (IOI) kwakuwa numbering ina segment mbili, segment ya kwanza ni namba 3 na segment ya pili ni herufi.
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Back
Top Bottom