Mfumo wa uongozi wa chama cha ACT-Tanzania

Mfumo wa uongozi wa chama cha ACT-Tanzania

WE ARE ANONYMOUS

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2015
Posts
217
Reaction score
284
Salaam JF,

Mimi nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za vyama vya upinzani hapa Tanzania, pamoja na mifumo yake ya uongozi, sasa kuna hiki chama kipya cha ACT Tanzania, naomba washika dau wa hiki chama ikiwezekana Zitto mwenyewe anifafanulie hili ili Watanzania wengine tuweze kufahamu.

Kwa ufahamu wangu, sijajua bado ACT inafuata mfumo upi wa uongozi unaoruhusu kuwa na Kiongozi Mkuu wa Chama, Mwenyekiti wa Chama na Katibu Mkuu wa Chama.

Mara nyingi ndugu yetu Zitto Kabwe amekuwa akijipambanua kwamba ni muumini wa demokrasia na anayeheshimu katiba, na nilipata kusikia kutoka kwa viongozi wa ACT kwamba katiba ya ACT hairuhusu mtu ambaye hajatimiza miezi sita ndani ya chama kugombea uongozi wa chama, sasa hii nafasi ya kiongozi mkuu wa chama, imetoka wapi? na jee aligombea na nani hadi kushinda nafasi hiyo maana majina yaliyotolewa wakati wa uchaguzi yalikuwa ya nafasi nyingine za uenyekiti na ukatibu etc, je katiba yao inaelezeaje kuhusu upatikanaji wa kiongozi mkuu wa chama? Kuna umuhimu gani wa kuwepo kwa mwenyekiti kama kuna mtu anayeitwa kiongozi mkuu?

Nikipata majibu ya kuridhisha kwa swali hili, huenda nikapata ushawishi wa kutaka kujua zaidi tofauti iliyopo kati ya chama hiki kipya na vyama vingine vya siasa na huenda nikafanya maamuzi sasa.

-
WeAreAnonymous
 
Nafasi ya kiongozi mkuu wa chama amepewa mwenye chama, yaani mwanzilishi wa chama Ayatollah Zitto na hairuhusiwi kugombewa na mtu mwingine.
 
Nafasi ya kiongozi mkuu wa chama amepewa mwenye chama, yaani mwanzilishi wa chama Ayatollah Zitto na hairuhusiwi kugombewa na mtu mwingine.

si ni ZZK huyuhuyu akiwa CDM alikana kuanzisha ACT!? Mbona unamnenea uongo?
 
Act hawataki kuamin threads zao sasa zimebuma kwenye media!..this iz Tz buana, only 3wks in media,
 
Nenda kachukue kadi ya Chadema kaka huna haja ya kujishauri kujiunga ACT.Hiki chama ni cha wazalendo
 
Jana alikiri mwenyewe kwenye Hotmix ya EATV kwamba walianzisha ACT akawatanguliza wenzake.

hahahahahhahaahah
unafki mbaya sana..haya wanaomfata ZZK waangalie hizi ndimi mbili mapema, zitawagharimu baadae
 
Tufike mahali tuwaache ACT wajenge chama chao. Tunafahamu chama kipo na kina mfumo wake na viongozi. Mfumo na muundo wa chama ni kwa ajili ya matakwa ya wanachama. Kama sio utaona huuelewi basi jua chama hikikuhusu.
 
Wakuu naombeni tofauti kati ya ACT~Tanzania na ACT~Wazalendo.....
 
Mbona Jibu Rahisi sana.

Chama hiki ndio kimeanza kuwa na viongozi Rasmi sasa. Kwa hiyo Katiba inaanza kazi baada ya kuwa na Uongozi Rasmi na Umeanza wiki iliyopita!
 
Nenda makao makuu ya ACT - wazalendo yapo kijitonyama watakufafanulia vizuri. Humu unatuchosha tu.
 
Act hawataki kuamin threads zao sasa zimebuma kwenye media!..this iz Tz buana, only 3wks in media,
 
Kwani ACT wana ajenda gani? ya kupambana na chama kubwa CHADEMA au C2M maana naona wanaungwa mkono hata na Nape tuambieni
 
Back
Top Bottom