Katika sehemu ya kwanza, nilizungumzia ni jinsi gani, huko mbeleni, mfumo wa uchaguzi unaotumika Tanzania kwa sasa waweza kutuletea matatizo katika kutupa serikali yenye nguvu.
Kwa leo ningependa kuongelea swala linalosumbua hata nchi zilizobobea katika demokrasia - Political Funding, na hasa Campaign Funding.
Tupende au tusipenda, pesa ina nafasi kubwa sana katika kumchagua mshindi wa chaguzi za rais na wabunge. Ni wazi kabisa kuwa chama au Mbunge mwenye pesa ana uwezo wa kusambaza sera zake kwa watu wengi na hivyo kupata wapiga kura zaidi (Na wakati mwingine KUHONGA!!!). Hali hii imefanya nchi zilizoendelea kama vile Marekani, Uingereza, nk, kupitisha sheria zinazojaribu kudhibiti tatizo hili.
Kuna njia kuu mbili zinazoweta kutumika katika kutatua hili tatizo:
1. Kuweka 'limitations' (kiwango cha juu) katika pesa ambayo chama au mbunge anaweza kupokea wakati wa uchaguzi; au
2. Kuweka 'spending limit/cap' (kiwango cha juu) ambacho chama au wabunge wanaweza kutumia wakati wa uchaguzi.
Swali: Je imefikia wakati muafaka kwa Tanzania nao kuweka sheria kama hii? Na kama ipo, je inafuatwa?
Tukiangalia matumizi ya chama kimoja katika uchaguzi wa 2005, tunaweza kupata picha kwa mbali ya pesa iliyotumika. Kwa data zinazopatikana katika uchaguzi 2005, kulikuwa na wapiga kura takriban 11,000,000. Chadema kilitumia Tsh753,786,505/-. Hii ni sawa na Tsh68/- kwa kila mpiga kura. Nimeshindwa kupata data za vyama vingine pamoja na jumla iliyotumika na vyama vyote katika uchaguzi huo.
Je wadau mnaonaje bei/gharama ya kura zenu?
Je ungependa bei/gharama ya kura yako ipande au ishuke?
Je tunahitaji kuweka kiwango kimoja kitakachotumika kwa vyama vyote? - Kwa mfano sh billion 1, na hivyo kufanya kampeni zisiwe za kumwaga au kuchangisha pesa bali kujadili mambo yanayotuhusu sisi wananchi?
Mwisho kabisa ni swala la hiyo pesa watakaopewa wabunge na vyama kwa ajili ya uchaguzi.
Je mnakubali kodi yenu itumike katika kuvipa vyama pesa za uchaguzi, kama itasaidia kufanya hizo chaguzi ziwe wazi zaidi?
P.S: Je Kagoda ingekuwepo? hehehehe