Mfumo wa Uchaguzi Tanzania na ufadhili wa kisiasa

Chapakazi

Chapakazi

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2009
Messages
2,880
Points
1,195
Chapakazi

Chapakazi

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2009
2,880 1,195
[FONT=&quot]Je, Tanzania yahitaji kubadili mfumo wake wa uchaguzi kuepukana na yaliyoikuta Kenya na Zimbabwe?[FONT=&quot][/FONT][/FONT]
[FONT=&quot]Mfumo wa uchaguzi wa Tanzania ni kama mifumo itumikayo Kenya na Zimbabwe. Tunatumia mfumo uitwao First Past the Post. Mfumo huu unatumika na nchi nyingi duniani, ikiwa pamoja na zilizoendelea kama Marekani na Uingereza. Lakini kutokana na 'constitution arrangement' yetu (mfumo wetu wa katiba), sisi tunafanana zaidi na majirani zetu: Kenya na Zimbabwe [/FONT]
[FONT=&quot]Tatizo lilitojitokeza ndani ya mfumo huu hivi karibuni katika nchi zetu jirani ni kushindwaji wa mfumo huu katika kuipa nchi serikali, au serikali yenye uwezo wa kuwahudumia wananchi ipasavyo. [/FONT]
[FONT=&quot]Swali: Je Tanzania inafanya/imefanya nini iweze kujiepusha na tatizo hili? Au twasubiri kukumbwa na janga kabla ya kubadilika![/FONT][FONT=&quot][/FONT]
 
Kamende

Kamende

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2008
Messages
415
Points
0
Kamende

Kamende

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2008
415 0
mtoto
Pamoja na kuwa na mfumo mbaya sana wa uchaguzi, pia tuna matatizo makubwa katika sheria yenyewe ya uchaguzi, sheria yenyewe ya uchaguzi, sheria ya vyama vya siasa na hatimaye Katiba nzima ya Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania.

Nikukumbushe kuwa hata ripoti ya jaji Nyalali alipotoa maoni ya tume yake kuhusu Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa haija tekelezwa kwa kufikia nusu yake.

CCM imeamua kuwalazimisha watanzania kufanya siasa za chama kimoja kwa kutumia vyama vingi. Kuna kazi kubwa kuirudisha nchi katika mstari wakati huu ambao tuko chini ya chama cha watu wanaofikiri kuwa Tanzania imeumbwa waitawale na kuila wao.

Nichukue nafasi hii kuwaomba watanzania wenye moyoj na nchi yao waanze kudai kwa nguvu Katiba mpya inayokidhi mahitaji ya siasa za nyakati hizi na marekebisho ya sheria zote zinazokinzana na uhuru na ushiriki huru wa mambo ya siasa.

Tusipodai haki zetu hakuna wa kutupa kwa huruma.
 
Chapakazi

Chapakazi

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2009
Messages
2,880
Points
1,195
Chapakazi

Chapakazi

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2009
2,880 1,195
Katika sehemu ya kwanza, nilizungumzia ni jinsi gani, huko mbeleni, mfumo wa uchaguzi unaotumika Tanzania kwa sasa waweza kutuletea matatizo katika kutupa serikali yenye nguvu.

Kwa leo ningependa kuongelea swala linalosumbua hata nchi zilizobobea katika demokrasia - Political Funding, na hasa Campaign Funding.
Tupende au tusipenda, pesa ina nafasi kubwa sana katika kumchagua mshindi wa chaguzi za rais na wabunge. Ni wazi kabisa kuwa chama au Mbunge mwenye pesa ana uwezo wa kusambaza sera zake kwa watu wengi na hivyo kupata wapiga kura zaidi (Na wakati mwingine KUHONGA!!!). Hali hii imefanya nchi zilizoendelea kama vile Marekani, Uingereza, nk, kupitisha sheria zinazojaribu kudhibiti tatizo hili.

Kuna njia kuu mbili zinazoweta kutumika katika kutatua hili tatizo:
1. Kuweka 'limitations' (kiwango cha juu) katika pesa ambayo chama au mbunge anaweza kupokea wakati wa uchaguzi; au
2. Kuweka 'spending limit/cap' (kiwango cha juu) ambacho chama au wabunge wanaweza kutumia wakati wa uchaguzi.

Swali: Je imefikia wakati muafaka kwa Tanzania nao kuweka sheria kama hii? Na kama ipo, je inafuatwa?

Tukiangalia matumizi ya chama kimoja katika uchaguzi wa 2005, tunaweza kupata picha kwa mbali ya pesa iliyotumika. Kwa data zinazopatikana katika uchaguzi 2005, kulikuwa na wapiga kura takriban 11,000,000. Chadema kilitumia Tsh753,786,505/-. Hii ni sawa na Tsh68/- kwa kila mpiga kura. Nimeshindwa kupata data za vyama vingine pamoja na jumla iliyotumika na vyama vyote katika uchaguzi huo.

Je wadau mnaonaje bei/gharama ya kura zenu?
Je ungependa bei/gharama ya kura yako ipande au ishuke?
Je tunahitaji kuweka kiwango kimoja kitakachotumika kwa vyama vyote? - Kwa mfano sh billion 1, na hivyo kufanya kampeni zisiwe za kumwaga au kuchangisha pesa bali kujadili mambo yanayotuhusu sisi wananchi?

Mwisho kabisa ni swala la hiyo pesa watakaopewa wabunge na vyama kwa ajili ya uchaguzi.
Je mnakubali kodi yenu itumike katika kuvipa vyama pesa za uchaguzi, kama itasaidia kufanya hizo chaguzi ziwe wazi zaidi?

P.S: Je Kagoda ingekuwepo? hehehehe:rolleyes:
 
Chapakazi

Chapakazi

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2009
Messages
2,880
Points
1,195
Chapakazi

Chapakazi

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2009
2,880 1,195
Katiba mngependa ibadilike hasa sehemu gani?
 
K

Kipimautu

Member
Joined
Nov 23, 2007
Messages
8
Points
0
K

Kipimautu

Member
Joined Nov 23, 2007
8 0
Kwa kweli huu mjadala umekuja vizuri japo umechelewa.

Naomba nichangie kwa kuibua hoja,
Kwanini tunachagua?
Je demokrasia ya moja kwa moja (direct democracy) imeshindikana kabisa? sasa tuboresheje demokrasia ya uwakilishi? haya ni maswali wanazuoni wengi wangependa kuanza nayo kama utangulizi. Hata hivyo mimi naona kuwa changamoto katika chaguzi zimegawanyika katika makundi matatu.
Kundi la kwanza - changamoto zinazomkabili Mpiga kura:
Je, anafahamu kwa nini anapiga kura?
Je, anaweza kweli kufanya maamuzi sahihi katika kupiga kura?
Je, anaridhika na matokeo ya kupiga kura?

Kundi la pili ni changamoto zinazomkabili Mpigiwa kura
Je, Kwa nini anaomba kura?
Je, Kuna mazingira ya kumfanya apigiwe kura na wale wanaopenda kumchagua?
Je, ana sifa za kupigiwa kura? [kama hana - je ana takrima?
Je, naridhika na matokeo ya kura? hata kama ameona kuwa ameibiwa?

Kundi la tatu ni changamoto zinazohusu Msimamizi wa kura
Je, Yuko huru au ana shinikizo?
Je, Anapendelea upande Fulani?
Je, Anakubalika na kuaminiwa na wapiga kura?
Je, wapigiwa kura wanaridhika na maamuzi yake?
Je, taratibu na sheria zinatenda haki?

Unajua mjadala kuhusu mfumo wa uchaguzi kimsingi unatokana dosari kadha wa kadha, mathalan - :
-Matumizi ya nguvu na vitisho toka katika vyombo vya dola
-Wananchi kukosa hamasa katika kupiga kura
-Rushwa itolewayo na wagombea
-Rushwa idaiwayo na wapigakura
-Maamuzi mabovu ya wasimamizi wa chaguzi
-Utamaduni wa kutokukubali kushindwa
-Wananchi kunyimwa haki ya kupiga kura
-Wizi wa kura
-Ugawaji mbovu/wa hila wa majimbo ya uchaguzi
- [new invention] muafaka wa hila wa mwizi na mwibiwaji wa kura - mfano Kenya na Zimbabwe.

Mambo yanayopendekezwa
-Kubadili mfumo wa uchaguzi – FPTP kenda PR au PR kwenda FPTP
- kuweka mfumo sahihi wa kuhama chamaCrossing the Floor – bila kupoteza ubunge, udiwani au urais
-mgombea binafsi -Independent Candidates –
- kuweka utaratibu wa wananchi kuwa na mamlaka ya kuwaita wawakilishi wao na kuhoji ufanisi wao ikiwa ni pamoja na kupiga kura ya kutokuwa na imani nao Recalling –

Nafikiri nikipata nafasi nitaandika kwa undani kifungu kwa kifungu cha katiba, sheria ya uchaguzi, sheria ya vyama vya siasa, sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa n.k

Nakubali kuwa upo umuhimu mkuuuuuuuubwa wa kuujadili na kuupatia ufumbuzi mfumo wa uchaguzi utakaotutendea haki watanzania - tumezidi kudanganywa.

naomba kuwasilisha.
 
Hii safi sana...this is the kind of discussions we should be having, na sio kila siku Mengi na Rostam. Lazima tuweke discussion zinazojenga nchi yetu.

Nimependa maswali yako. Ukiweka hivyo vifungu tukavijadili itakuwa safi sana. Hata mimi nataka kuanza kuweka. Maana cha muhimu ni kujua sheria. Bila kujua sheria inayotutawala, tunakuwa kama makondoo tu. Kwa mfano, watu wengi wanaongelea kubadilishwa kwa katiba, lakini hawatoi vifungu hasa vinavyotakiwa kubadilishwa. Na katika ubadilishaji wa katiba, kunahitajika kiasi gani cha wabunge kukubali mabadiliko?
 
I

Interested Observer

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2006
Messages
1,546
Points
2,000
I

Interested Observer

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2006
1,546 2,000
mtoto
Pamoja na kuwa na mfumo mbaya sana wa uchaguzi, pia tuna matatizo makubwa katika sheria yenyewe ya uchaguzi, sheria yenyewe ya uchaguzi, sheria ya vyama vya siasa na hatimaye Katiba nzima ya Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania.

Nikukumbushe kuwa hata ripoti ya jaji Nyalali alipotoa maoni ya tume yake kuhusu Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa haija tekelezwa kwa kufikia nusu yake.

CCM imeamua kuwalazimisha watanzania kufanya siasa za chama kimoja kwa kutumia vyama vingi. Kuna kazi kubwa kuirudisha nchi katika mstari wakati huu ambao tuko chini ya chama cha watu wanaofikiri kuwa Tanzania imeumbwa waitawale na kuila wao.

Nichukue nafasi hii kuwaomba watanzania wenye moyoj na nchi yao waanze kudai kwa nguvu Katiba mpya inayokidhi mahitaji ya siasa za nyakati hizi na marekebisho ya sheria zote zinazokinzana na uhuru na ushiriki huru wa mambo ya siasa.

Tusipodai haki zetu hakuna wa kutupa kwa huruma.
thank you
 
O

Ogah

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
6,232
Points
1,225
O

Ogah

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2006
6,232 1,225
Hii safi sana...this is the kind of discussions we should be having, na sio kila siku Mengi na Rostam. Lazima tuweke discussion zinazojenga nchi yetu.

Nimependa maswali yako. Ukiweka hivyo vifungu tukavijadili itakuwa safi sana. Hata mimi nataka kuanza kuweka. Maana cha muhimu ni kujua sheria. Bila kujua sheria inayotutawala, tunakuwa kama makondoo tu. Kwa mfano, watu wengi wanaongelea kubadilishwa kwa katiba, lakini hawatoi vifungu hasa vinavyotakiwa kubadilishwa. Na katika ubadilishaji wa katiba, kunahitajika kiasi gani cha wabunge kukubali mabadiliko?
mtoto,

shukran kwa mada yako nzuri. Nikiri kuwa mada inayojadili imeshakuwepo hapa (hata katiba yneyewe iliambtanishwa) na wajuvi wa mambo ya katiba walishaanza kuichambua kama sikosei........cha ajabu sana naona haikuwa popular as most of us would imagine............pengine tui-revisit ile mada tuone wenzetu waliishia wapi.

then tunagalie katiba inasemaje kuhusu uchaguzi, je kuna kasoro, mapungufu or vitu visivyohitajika...............

ngoja niitafute ile mada niweke link yake hapa
 
Forum statistics

Threads 1,284,203
Members 493,978
Posts 30,817,141
Top