DOKEZO Mfumo wa malipoa wa serikalini uboreshwe

DOKEZO Mfumo wa malipoa wa serikalini uboreshwe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Super Msouth

Senior Member
Joined
Dec 28, 2014
Posts
145
Reaction score
128
Habari wanajamvi!

Utaratibu wa ulipaji serikalini wa fedha zote huanza na maombi ya fedha kwa jambo linalokusudiwa mfano manunuzi au posho na haya maombi ya fedha kwa namna nyingine huitwa dokezo.

Maombi yote huenda sambamba na vielelezo (viambata) vinavyohalalisha uwepo wa maombi hayo.

Maombi yakishaandikwa yatapitia kwa mkuu wa idara husika (kutegemea aina ya maombi na muombaji) ambapo maombi hayo anaandikiwa mkuu wa taasisi husika ambaye ni mlipaji.

Mkuu wa taasisi akishajiridhisha na malipo yanayokusudiwa kuna uhali wa kufanyika na fedha ipo anamuomba mweka hazina aendelee na mchakato wa ulipaji.

Mweka hazina naye hujiridhisha kama fedha ipo na inafaa kulipwa kama maombi yalivyokuja akijiridhisha naye anaruhusu kuendelea na ulipaji.

Muhasibu wa ulipaji akishapokea dokezo ambalo tayari limeruhusiwa kufanywa kwa ulipaji ataandika hati ya malipo (payment voucher) na atapandisha dokezo pamoja na viambata vyake kwenye mfumo wa ulipaji ambapo mweka hazina atapitia tena kuhakikisha hakuna makosa na kuruhusu malipo yaendelee na mkuu wa taasisi naye pia ataruhusu.

Baada ya mkuu wa taasisi kuruhusu malipo ofisi ya hazina kanda (mkoa husika) na watapitia maombi ya ulipaji na wanatakiwa waruhusu malipo yaendelee.
Baada ya ruhusa (approval) kutoka hazina BOT nao wanapitia maombi na kuruhusu malipo kufanyika kwa kutoa namba za malipo kwa malipo yaliyoruhusiwa.

Michakato ya ulipaji mara nyingi inachelewa kwenye hatua za awali endapo mfumo wa ulipaji utakua na shida au wahusika wakiamua kuchelewesha malipo kwa makusudi, shida kubwa ipo BOT kuna wakati wanaamua kuchelewesha ulipaji au hawaruhusu kabisa malipo haswa kipindi cha mwisho wa mwaka wa fedha na mwanzo wa mwaka wa fedha hali ambayo mara nyingi huzalisha madeni kwenye taasisi za serikali maana anayekusudiwa kulipwa malipo yake yalishaandikwa hatoandikiwa tena malipo.

Serikali itafute namna bora hatua hii ya mwisho ya mchakato wa ulipaji kabla fedha kumfikia mlipwaji ili kuondoa madeni ambayo hayakua na ulazima kutengenezwa.
 
Back
Top Bottom