Mfumo wa malipo ya mafao baada ya kustaafu uboreshwe

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,896
Mfumo tulionao wa malipo baada ya kustaafu unafaa uangaliwe upya ili kuboresha kuendana na ukali wa maisha ya Mtanzania wa leo. Mfumo wa kupata malipo kwa mkupuo si mfumo mzuri kwa vile kuna kupunjwa kwa wanaokatwa pesa zao na si wote wenye uzoefu wa kuzipangia bajeti pesa wanazopa kwa mkupuo kwa matumizi ya maisha yao baada ya kustaafu.

Pesa zinazokatwa huwa zinazalishwa kwa njia mbalimbali, na pia zimewekwa katika vitegeuchumi mbalimbali, lakini anachoambulia mstaafu hakiingii kinywani zaidi ya mara moja. Tunabaki na maswali yasiyojibika kwamba pesa za mfanyakazi anazokatwa maisha yote awapo kazini na muda wote huo aliokuwa anafanya kazi pesa ya makato ilikuwa inaendelea kuchuma kwa njia mbalimbali kama mikopo,ujenzi ma majengo ya kukodisha, mabenki nk. Amana zote hizo hazimsaidii mstaafu, anachoambulia ni kidogo tu kwa mkupuo mmoja na baada ya miezi michache anabaki maskini kana kwamba hakuchangia mfuko wa mafao baada ya kustaafu.

Utaratibu mzuri wa mafao ya mfanyakazi baada ya kustaafu ni ule wa kupewa kiwango fulani kila mwezi kwa maisha yake hadi atakapokufa. Hii inatokana na ukweli kwamba muda wote aliofanya kazi na kukatwa mafao ya uzeeni pesa yake ilikuwa inazalisha, na hivyo si vema kwamba apate mgao mdogo tu usiomwezesha kuendesha maisha yake hadi atakapokufa, kwani wengi wao baada ya kustaafu wanaishi maisha magumu na ya ziki isivyo kifani.

Mfumo huo ndio unaotumika katika baadhi ya mataifa yaliyoendelea, ingawa hawawezi pata pesa ya kutosha kama mfanyakazi, lakini ana uhakika wa kupata kiasi fulani kila mwenzi na hivyo kumsaidia kuendesha maisha katika mahitaji muhimu ya kila siku kwake na familia yake.

Ni mategemeo yangu serikali itaibua hoja ya mswada wa kufanyia marekebisho mfumo mzuri wa malipo ya mafao baada ya kustaafu ili wastaafu waishi maisha ya utulivu na kufurahia ustaafu wao
 
kuna umuhimu wa kuboresha viinua mgongo vya wafanyakazi kwa maisha ya leo
 
Mkuu unazungumzia Mafao ya Mfuko upi wa Pensheni. Kuna mifuko mingine kama ya LAPF hoja yako siyo applicable.
 
Back
Top Bottom