Mfumo wa kutahini wa NBAA utazamwe upya

Mfumo wa kutahini wa NBAA utazamwe upya

Joined
Aug 10, 2011
Posts
35
Reaction score
13
MFUMO WA KUTAHINI WA NBAA UTAZAMWE UPYA

Naishangaa sana NBAA. Wakati nchi nyingine za muungano wa jumuia ya Afrika Mashariki zikifanya kila juhudi kuhakikisha wananchi wake hawaachwi nyuma kielimu,NBAA yenyewe inafanya kila juhudi za kupunguza watu wenye CPA hapa Tanzania.

Wakati nchi kama Kenya sasa hivi imeanza kuwapa kila mtoto wa darasa la kwanza Laptop yake huku Tanzania hata Yule wa Chuo kikuu haijulikani atapewa Laptop lini.

Jumuia ya Afrika Mashariki inakaribia kuanza shughuli zake zote kama jumuia.Ikiwemo watu kusafiri nchi moja hadi nyingine bila ya kikwazo chochote yaani itakuwa hakuna kudaiwa passport wala kibali cha kusafiria kutoka nchi moja kwenda nyingine, tunachokiona hapa ni kwamba jumuia ya Afrika Mashariki ikianza shughuli zake bila kikwazo basi Watanzania wengi watapoteza ajira zao. Kwa sababu watanzania wengi hawana vyeti vya kazi wanazozifanya sasa.Utakuta mtu anajiita Mhasibu Mkuu wa idara au wizara au kampuni fulani lakini CPA hana.Kwa nini hana ? Alishafanya sana mitihani ya CPA lakini hakufaulu kutokana na ugumu wa mitihani hiyo.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba serikali itafute namna nyingine ya kuongeza ufaulu kwa watahiniwa wa mitihani ya NBAA , la sivyo jumuia ya Afrika Mashariki ikianza rasmi , kazi zote za masuala ya uhasibu na ukaguzi wa mahesabu zitachukuliwa na wakenya na waganda kutokana na ukweli kwamba huku Tanzania watu wenye CPA ni wachache sana kutokana na ufaulu mdogo sana wa watahiniwa wa mitihani ya NBAA.

Mpaka sasa hapa Tanzania watu wenye CPA wapo elfu tano na hiyo idadi imefikiwa kuanzia tangu mwaka 1972 ambapo hiyo NBAA ilipoanza kutahini mitihani ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu.Kati ya hao elfu tano wenye CPA , wapo ambao tayari wameshakufa siku nyingi,wapo ambao wana CPA lakini hawazitumii kufanya kazi za uhasibu(kwa mfano ma-lecturer), wapo ambao wana CPA lakini wameshaondoka hapa nchini siku nyingi.

Tunaiomba serikali iitazame upya utungaji,ufanyaji ,usahihishaji na upangaji wa matokeo wa hii bodi ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu-NBAA la sivyo milango ya jumuia ya Afrika Mashariki ikifunguliwa, basi watanzania wengi watapoteza ajira zao zinazohusiana na uhasibu na ukaguzi wa mahesabu kutokana na kukosa CPA .
 
Mfumo wa sasa ndio unaoifanya CPA na fani ya uhasibu iwe na heshima kubwa. Mabadiliko unayoyataka ni kutaka kuifanya fani hiyo ipoteze heshima yake
 
Unajua wewe unaongea mambo muhimu sana yanayohusu mustakabali wa Taifa letu katika jumuia ya AFrika Mashariki.Lakini nani wa kukusikiliza na kukuelewa unachoongea? Diwani anajua kusoma na kuandika tu, mbunge kaishia kidato cha nne.Hiyo CPA unayoisema wataijulia wapi ? Huyo waziri wa fedha wa Tanzania nzima hiyo CPA hana ! Kama hutaki bisha !
 
Mie naenda mbali zaidi kuuliza je kwanini watu hawafaulu hiyo mitihani? Je unaposema mitihani migumu, inamaana ipo nje ya sylabus? Je vitu vinavyotakiwa kusomwa katika ngazi mbalimbali za CPA ni tofauti na kinachosomwa kny uhasibu ulimwenguni kote? Mie nadhani tatizo sio NBAA wahangaike kuongeza ufaulu. Wakifanya hivi watatoa wataalam ambao hawajaiva vema. Kikubwa ni kutengeneza standards, wanafunzi watengenezewa miundombinu mizuri kama learning resources na wawekewe hizo standards zilizo kuwa benchmarked against good perfromers in the world. Uganda na Kenya sio benchmark nzuri kielimu, tunawataalam wakitanzania wanaosifika Uganda na Rwanda kwa elimu yetu hii hii. Kwa hiyo kikubwa ni kuboresha tu elimu yetu maana kama ni standards nzuri tulikuwa nazo
 
Mitihani ya CPA ni lazima iwe migumu kwani hiyo ni professionalism siyo academic.hapo anatafutwa a future consultant, mkuu kuitwa consultant maana yake ushauri wowote utakaotoa wewe kama CPA holder ni authority. Jitahidi kusoma maeneo makubwa ya silabi ya CPA na kuyaelewa kwa ufasaha.
 
wewe km umeshindwa bwana tuachie sisi tupambane, kwani ho wanaotunga si watu?? kwanini wewe unakata tamaa haraka
 
HV huyu mchumi wetu daraja la kwanza wa ccm mwigulu mchemba anayo hii kitu cjui c.p.u au ccp ooo samahan jamani namaanisha C.P.A. huyu kislip anayo kweli
 
Hatutaki junks katika fani yetu. Kwanza nafikiri NBAA wamelegeza viwango vya ufaulu siku hizi.
 
Wanachofanya NBAA ni kuwachenga watahiniwa,
Hiyo mitihani yao ni below standards,na ni kuwakomoa watahiniwa!!
Inabidi wajipange upya,Waige mfumo wanaotumia ACCA
 
HV huyu mchumi wetu daraja la kwanza wa ccm mwigulu mchemba anayo hii kitu cjui c.p.u au ccp ooo samahan jamani namaanisha C.P.A. huyu kislip anayo kweli

aitoe wapi? Wote akina Zitto hawana na hawawezi kuipata. Uchumi ni tofauti sana na uhasibu
 
Unajua wewe unaongea mambo muhimu sana yanayohusu mustakabali wa Taifa letu katika jumuia ya AFrika Mashariki.Lakini nani wa kukusikiliza na kukuelewa unachoongea? Diwani anajua kusoma na kuandika tu, mbunge kaishia kidato cha nne.Hiyo CPA unayoisema wataijulia wapi ? Huyo waziri wa fedha wa Tanzania nzima hiyo CPA hana ! Kama hutaki bisha !

Kuna kaka yangu mmoja alionana na mbunge wetu kule kijijini baada ya kusota muda mrefu bila ya ajira, ili amfanyie mpango kama itawezekana somwhere. Elimu yake ni proffession ya CSP ya NBMM kipindi kile.yule mbunge alimwambia rudi shuleni kwanza itakua ngumu kupata kazi na hii elimu yako ya kuungaunga!
 
ni bora iwe migumu ili tuwapate competent candidates, sio kufaulu tu kama matokeo ya darasa la saba. na pia ili heshima iwepo kitaa.
 
Umesahau kutoa data za wenye CPA kenya na Uganda. Ni kweli kuwa TZ ni wachache but hata kenya pia siyo wengi kihivyo, infact hawajafika 10000.

Hizo standard ndo zinafanya fani iwe na heshima, mnaotaka kufaulishwa shauri zenu. Tunataka watu watakao kuwa na vitu kichwani siyo idadi tu ya watu kuwa wengi.
 
sio watakao kuwa na vitu kichwani bali watakao kremu na kuotea pepa soon cpa nayo itajishushia heshima graduates wengi wanakariri kwa vile ni fresh from schools kwa miaka ya karibuni nawengine nawafahamu tumetoka nao mbali kichwani kawaida sana ila wamegraduate na wanakili pepa waliotea maswali yote walisha solve kwa Rashidi na kule Posta but ndo hvyo bahati imewaangukia cpa ckuiz ni bahat tu kuotea pepa ndo maana wengi wao utakuta bado ni graduates cpa hawajazifanyia kazi na kuwa registered officially kwenye bodi. Nadhani hata mimi nisingesoma banking n finance na mm ningeshaipata
 
Hayo maneno ya mkosaji huyo Rashidi mganwa hamkremishi mtu anakufundisha na unaelewa

Ukweli ni kwamba graduates wengi wanamaliza degree kichwani hamna kitu kabisa, wakati wa review classes wengine wa wafanyakazi hawana muda kabisa, Mtu anahidhuria review lakini hana muda wa kujisomea (rashidi anawasaidia atleast kwa kuweka swali la kutokea)

Na hiyo new syllabus ndo kigongo zaidi BIG UP NBAA

In this world nothing is certain than Tax and Death.
 
Uhasibu wa serikalini ni rahisi sana,kuandika voucher hakuhitaji CPA, pia watu wengi wanakariri maswali
 
Nbaa wanakomoa watu kama unapesa kafanye mitihani ya ACCA
au Cima
 
Mi nadhani tatizo kubwa liko to their standards of setting examinations and syllabus contents...But I believe baada ya kuanza hiyo new syllabus ambayo inaanza kuwa tested November 2014 itasaidia saana kwani itakuwa ni Competency Based Examinations tofauti na sasa ambapo ni Academic Based Examinations. Inatakiwa watunzi wa mitihani wafanye reflection ya what is actually happening in our companies now. So the question scenarios should be based in real environment of Tanzania, na sio kucopy tu maswali kutoka kwenye vitabu vilivyoandikwa na wazungu, they must do research first kabla ya kutunga swali. Kwa mfano wanaweza kwenda hata Kwenye any producer company wakaangalia financial statement zao na kutunga swali kwa wanafunzi ambalo lina reflect the current practice.
Pia wanatakiwa waandae mitihani yenye scenarios tu ambayo inatest competency ya mwanafunzi, maswali kama what are the advantages for something au mention procedures for something without having a scenario explaining the situation ni ya ki academic zaidi and not competency based. Kwa hiyo mi nadhani mambo yatakuwa sawa baada ya kuanza hiyo syllabus mpya, ila pia wajiandae kubadilisha mindset za trainers na examiners. They must be aware of the meaning of competency based examinations schemes.
 
Back
Top Bottom