Krikichino
JF-Expert Member
- Oct 5, 2019
- 651
- 1,097
Asante mno kwa kuweza kufungua uzi huu. Naomba niende moja kwa moja kwenye mada.
Wakorea huwa wanatumia mfumo wa tofauti sana katika kupeana majina. Kwa hapa Tanzania kwa mfano mtu anaitwa JOHN SULUHU KIKWETE.
Maana yake hapo JINA LAKE ni JOHN, SULUHU ni JINA LA BABA alafu KIKWETE ni jina la ukoo. Hiyo inaeleweka sina haja ya kukazia sana.
Sasa kwa upande wa Korea kuna utofauti kidogo.
1. JINA LA FAMILIA LINAKUA LA KWANZA
Yes. Kwa mfano mtu anaitwa LEE MIN HO. Maana yake hapo LEE ni jina la familia au la ukoo alafu MIN HO ndio jina lake alilopewa.
Au tuseme PARK GEUN HYE maana yake hapo PARK ni jina la familia alafu GEUN HYE ndio jina lake.
2. WAKOREA WANA MAJINA MAWILI TU.
Wabongo mtu huwa na majina matatu. Mfano Ali Salehe Kiba. Kwa Korea majina ni mawili ni mawili tu. Mfano KIM YOUNG SAM hapo majina ni Kim la kwanza na Young Sam la pili.
Hawana haya mambo ya jina la baba. Ni jina la mtu na la familia basi.
Sasa kama umeangalia series au movies nyingi za Kikorea utafahamu kuwa wakorea wengi huitwa KIM, LEE, PARK, CHOI na JUNG.
Ukweli uliopo ni kwamba by 2015, watu takribani 10.6 Milion wanatumia jina la KIM hiyo ni sawasawa na 21.5% ya wakorea wote wanatumia jina la KIM.
Maana yake ni kwamba KIM ndio jina linalotumiwa sana na wakorea kama Surname likifuatiwa na LEE pamoja na PARK ambapo kulingana na sensa iliyofanyika 2015 takribani nusu ya wakorea wanatumia majina ya KIM, LEE na PARK.
Sasa kuna kitu kimoja lazima tukielewe haimaanishi kuwa KIM au LEE wote ni ndugu. Maana yake ni kwamba staa LEE MIN HO na LEE SEUNG GI pamoja na kwamba wote ni kina Lee lakini sio ndugu maana Koo zao ni tofauti.
Pia kutokana na sensa y mwaka 2000 kwenye Jina KIM kuna koo kama 348 ikiwemo ANDONG KIM, NAGAN KIM na YASEONG KIM.
Kwenye Jina La LEE pia kuna Koo kama PYEONGCHANG na GYEONGJU watu walioko kwenye Koo hizi, wote hawa wanaitwa Lee .
Muanzilishi wa kampuni ya Samsung LEE BYUNG CHUL, Mkurugenzi wa zamani wa Samsung LEE KUN HEE pamoja na Rais wa zamani wa korea kusini LEE MYUNG BAK wote wanatoka ukoo moja wa GYEONGJU.
Kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2000 huko Korea Kusini inasema kuna jumla ya SURNAMES 286 huku Koo zote jumla.
4,179