Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,620
- 6,510
Siku Tanzania ilipoamua kuwa yoyote anaweza kulelewa na baadae kupewa uongozi halafu akili atazipata huko huko katika uongozi, ndiyo siku tuliyoanguka kama taifa.
Mfumo wa nchi na wananchi kwa ujumla wanachanganya uzoefu na akili. Mtu yoyote ukimpa afanye jambo kwa muda wa kutosha, uzoefu utambeba ila ufanisi wake unaweza usiwe mzuri.
Viongozi wana access na taarifa muhimu. Wanapewa siri za watu, siri za taasisi mbalimbali na siri za nchi. Hizo taarifa haziwafanyi wawe bora zaidi ya watu ambao hawana hizo taarifa. Kwanza inaonyesha mfumo mzima wa kuzichakata na kuzitumia hizo taarifa kwa manufaa ya nchi haufanyi kazi. Taarifa zipo tu, inajulikana fulani mwizi, fulani kahaba, fulani fisadi, fulani tapeli, fulani muuaji, fulani mshirikina, ila tunaangaliana tu. Mara moja moja vidagaa vinadhalilishwa majukwaani baasi tunaona tuna viongozi.
Ukitaka kupima ufanisi, na hapa ndiyo akili ya mtu inapoingia, mpime wakati wa kufanya maamuzi yanayohitaji tafakuri ya kutosha. Hapo ndiyo utaona majigambo, utaona maamuzi ya kimhemko na kutishana tishana.
Ingekuwa mtu mmoja au watu wachache wala nisingeongea ila shida kubwa ni kwamba mfumo mzima umejaa watu waliochaguliwa kwa sababu tofauti na uwezo, wakalelewa baadae wakapewa nyadhfa na uongozi ikiaminiwa akili watazipata wakishaitwa waheshimiwa. Ndipo hapa tulipo.