Mfumo wa kisiasa [vyama vya kisiasa] ulio bora kwa Tanzania

Katiba mpya ndo inaandikwa hivyo.
1.Kuwepo na vyama viwili au vitatu pekee vya siasa na viimarishwe.

2. TANZANIA iwe na DIRA ya miaka 100 ijayo. Vyama vya siasa vyote vitengeneze Katiba zao na viwe na sera na mipango ya kitaifa ya pamoja, Watofautiane tu jinsi ya kuitekeleza, njia mbadala iliyo Bora.

3. TANZANIA yangu, wananchi waamue Tufuate UBEPARI au UJAMAA na vyama vyote vijengwe ktk misingi hiyo.

4.Malengo ya Vyama vya Siasa yabadilishwe, Lengo kuu lisiwe KUSHIKA Dola pekee, lengo kuu ni KUSIMAMIA MASLAH YA WANANCHI ktk nyanja mbalimbali za kiuchumi,kisiasa n kijamii.
Naudhika sana na lengo kuu la vyama vya siasa Kwa sasa, wanawaza tu kushika DOLA Kwa namna yoyote hata Kwa kumwaga Damu ya wananchi walowatuma.
Nimekupata mkuu👍 umeeleza vizuri. Ila sio tu kuhitaji katiba mpya pia tunahitaji mchakato wa katiba mpya uangaliwe upya yaani uanze upya
 
I
Kwa ardhi ya Tanzania kwa Sasa wala hatuhitaji Siasa nyingi bali utendaji na uzalishaji, Ukizingatia Siasa ni Majadiliano / Maamuzi ya jinsi nini kifanyike na ni vipi tutagawana resources chache, hivyo kwanza tuwekeze zaidi kwenye kuongeza hizo resources... ama sivyo tutaendelea kujadiliana zaidi bila kufanya.....

Kwa dunia mfumo wa Siasa bora kutokana na teknolojia iliyopo the future ni kwenye automation ndio njia pekee ya kuhakikisha ushiriki wa kila raia katika maamuzi ya rasilimali

Ila pasipo misingi bora/ imara ya Kisiasa atuwezi fika huko
 
I

Ila pasipo misingi bora/ imara ya Kisiasa atuwezi fika huko
Kipi kinatangulia.., misingi bora sio necessarily iwe ya kisiasa ingawa siasa ni part ya maisha.., kwahio swali ni tunafanya siasa gani / zipi ?

Siasa za sasa ni za Survival (Upinzani ili wachukue nchi na Watawala ili wabaki kwenye ulaji)
Siasa za Attacks na Defense (Wapinzani wana-attack ili kuwapaka matope watawala na watawala wanadefend kila uchafu unaofanyika ili mradi tu waendelee kukaa hapo juu)
Siasa za Wao na Sisi (haijalishi mwenzako anasema nini hata kama ni kibaya ni sawa na mwingine hata kama ni kizuri ni kibaya)

Kwahio utaona tatizo zaidi ni utamaduni na awareness ya wananchi kukubaliana na hizi siasa za majitaka..., kwahio kabla ya hawa watu kupata uelewa na kuwa-involved zaidi tutaendelea kuvutana na kufanya debates zisizo na mwisho...

Ila kukiwa na uelewa huenda nguvu nyingi zikawa kwenye results na sio kwenye mchakato ili watu wapate tu Kura ili waweze Kula...
 
Ni kweli katika Tanzania tunasiasa za maji taka lakini hiyo haitufanyi tushindwe kurekebisha mahali tulipokosea na kufuata siasa zilizo bora zisizo za maji taka ili tujenge nchi katika mstari bora. au wewe unapendekeza pasiwepo na siasa yoyote kabisa hapa nchini?🤔
 
Ni kweli katika Tanzania tunasiasa za maji taka lakini hiyo haitufanyi tushindwe kurekebisha mahali tulipokosea na kufuata siasa zilizo bora zisizo za maji taka ili tujenge nchi katika mstari bora. au wewe unapendekeza pasipo na siasa yoyote kabisa hapa nchini?🤔
Minimum Politics..., Sio kila kitu ni Siasa.., kama Siasa ni majadiliano ya kufanya maamuzi ya wanajamii, basi kama maamuzi mengi ya basic needs na vitu vya kitaaluma yatafanyika as a matter of fact basi utaona hata mzigo wa politicking utapungua
 
Anhaaa sawa
 
- Pendekezo langu kwa aina ya mfumo wa Kisiasa/ Vyama vya Kisiasa ulio bora unaopaswa kufuatwa katika nchi ya Tanzania ni uwepo wa Vyama vingi vilivyo huru na vyenye kupewa haki sawa.

- Katika mfumo huo wa vyama vingi kunapaswa kuwepo na mfumo wa vyama vikuu viwili shindani vyenye mlengo tofauti au sera tofauti hapa na maanisha pawepo na chama kimoja kikuu cha kijamaa na kingine kiwe chenye mlengo wa kubepari.

- Pia katika mfumo huo wa vyama vingi pia napendekeza katika chaguzi pawepo na kipengele kinacho husisha mgombea asiye na chama chochote/mgombea binafsi.

- Katika mambo ni siyoyapendekeza katika mfumo huo wa kisiasa/vyama vya kisiasa Ni uwepo wa utitiri wa vyama vya siasa yaani namaanisha pasiwepo na usajiri wa vyama vingi nchi visivyo zidi viwili tu vikubwa .

- Kama Kuna utiri wa vyama njia ya kuviondoa hivyo vyama ni kuungana na kuunda chama kimoja kikuu chenye sera moja Mfano .Kama tunavyo fahamu CCM tayari ni chama kikuu kikubwa hapa nchi tayari hicho ni chama kimoja chenye nguvu tumepata kimebaki kimoja na hiki kimoja kitapatika katika njia hii chadema ni chama chenye nguvu kwa upinzani hapa nchi kwa hio vyama vyote vidogo vidogo vinapaswa kuungana na chadema ili kuunda chama kingine chenye nguvu na hivyo kupata vyama vikuu viwili hapa nchi vyenye mlengo tofauti na sera tofauti.

- Mpaka hapo tumepata vyama vikuu viwili nchini ambavyo ni CCM mlengo wake unapaswa kuwa katika ujamaa na Muunganiko wa vyama vya upinzani unaounda chama kimoja kikuu mlengo wake unapaswa kuwa wa kibepari alafu nyongeza pawepo mgombea binafsi ambaye anachukua nafasi ya tatu ambaye atakuwa ajihusishi na chama chochote cha siasa Kati ya hivyo viwili tajwa hapo juu.

Mwisho; kiuhalisia Mimi sifagili uwepo wa utitiri wa vyama vya siasa hapa nchi kwetu bali nafagilia uwepo wa vyama vikuu viwili pamoja na mgombea binafsi Kama nafasi ya tatu.mfano:-
i, CCM
ii, Muunganiko wa vyama vya upinzani na kuunda chama kingine cha siasa kimoja tu
iii, Mgombea binafsi

- Ni hayo tu je wewe unafagilia uwepo wa utitiri wa vyama vingi hapa nchi? Je unafagilia uwepo wa mfumo upi wa kisiasa? Je mfumo wa vyama vingi ndio unapenda? Je chama kimoja ndio unapenda?na je Kama ni mfumo wa vyama vingi ni wa aina ipi viwe viwili tu Kama Mimi , vitatu ,vinne au idadi gani unataka wewe ? .

:- MUNGU IBARIKI TANZANIA ,MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI TANZANIA
VYAMA VIWILI,
MGOMBEA BINAFSI ASIZIDI MMOJA.
 
Kwanini kuna Vyama vingi vya Siasa ?

Tatizo Vyama vya Siasa vilivyopo ni Platform ya watu kwenda kula Keki ya Taifa na sio kusimamia misimamo / itikadi tofauti...

Sababu ni vigumu kulazimisha watu waungane kama fikra za njia ya kuongoza na kugawana Keki ya Taifa ni tofauti

Sasa waungane ili wafanye nini kama wao wenyewe fikra zao ni ardhi na mbingu..., pili kuwapangia / kukataza baadhi ya vyama inakwenda against uhuru wa watu labda cha kufanya ni kuongoza vigezo na masharti ili kuchuja wasiokidhi
Kama umuhimu wa vyama vingi ni kula keki ya Taifa.
Basi hakuna haja ya vyama vingi hata kidogo.
Ruzuku yake ianze kupeleka miradi ya kudumu kwenye watu wanaoishi mazingira hatarishi yasiyo na huduma za kijamii hasa vijijini.
 
Mfumo wa Vyama Vingi siyo ruzuku au kupinga pinga bali ni fikra chanya kama Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya 1977 Ibara ya 3 inavyotabanisha.
 
Kikatiba uko huko sahii.
Lakini lengo hilo kwa sasa si hakisi.
Kwani mitazamo mingi chanya kwa sasa ipo kuimarisha vyama na kuchokonoana kisiasa sio tena kukosoa na kupendekeza ñjia sahii za kufikia maendeleo hitajika.
 
Back
Top Bottom