Mfumo wa Epicor wafeli kwenye halmashauri za Dar na Pwani

mirindimo

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
892
1,709
Rais amezungukwa na genge la wanafiki wanaojivika ngozi ya mwanakondoo tena wengine kawaweka yeye washkaji zake matokeo yake mifumo na utendaji kazi unakuwa mbovu balaa.

Nitakupeni mfano mmoja tu sasa hivi halmashauri zote zina operate shughuli zake nyingi za kifedha kupitia mfumo wa epicor,lakini mfumo huu kwa wiki unaweza kuwa online mara mbili zaidi sana mara tatu siku zingine zooote mfumo unakuwa hauna network na unakuta watendaji wamekaa wanacheza karata kwenye computer zao, wengine wako mtandaoni wanamsoma Mange,yaani ni headache.

Jaribu kuulizia piga simu Temeke uliza kama wanapata mfumo,piga halmashauri za Pwani Kibaha huko ulizia kama wanapata!!!! Kuongoza hii nchi ni kazi mnooo kuliko unavyodhani lakini muda mwingine namwelewa rais wangu Magufuli.
 
Sasa wewe ulitaka Rais afanye nini ambacho umeshindwa au umekuwa-ignored na immediate supervisors wako? Ninachojua ni kuwa Rais JPM siyo software engineer wala computer wizard. Ni Rais wa JMT anayeongoza si Dar na Pwani tu bali mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar. Sasa inakuwaje suala la network failure ya DSM na Pwani unazi-attribute kwa Rais? Tafadhali tueleze inawezekana kuna kitu unakijua kuhusina na sababu za software ya EPICOR kukosa network hivyo kutokufanya kazi katika mikoa ya Dar and Pwani.
 
Mfumo wa EPICOR kama Ungekuwa unafanya kazi kama ulivyokusudiwa basi hakuna hata senti tano ya Serikali ambayo ingeibiwa kutoka Ofisi yoyote ya umma.

Mfumo huu nakumbuka ulishauriwa na ulianza kwa majaribio wakati Waziri wa fedha ni Marehemu Mgimwa na lengo ilikuwa kuzuia upotevu na wizi wa rasilimali fedha za umma.

Lakini Kuna figisufigisu ktk halmashauri na municipal nyingi kutopenda mfumo juu na kubaki na mfumo wa cash/cheque kwa kutumia voucher ktk malipo mbalimbali ya umma ambapo ni rahisi kufanya malipo hewa au wizi kufanyika!!

Changamoto kubwa ni internet kuwepo kila siku muda wote hilo ni tatizo kubwa sana!!
 
Rais amezungukwa na genge la wanafiki wanaojivika ngozi ya mwanakondoo tena wengine kawaweka yeye washkaji zake matokeo yake mifumo na utendaji kazi unakua mbovu balaa,ntakupeni mfano mmoja tu sasa hivi halmashauri zote zina operate shughuli zake nyingi za kifedha kupitia mfumo wa epicor,lakini mfumo huu kwa wiki unaweza kua online mara mbili zaidi sana maea tatu siku zingine zooote mfumo unakua hauna network na unakuta watendaji wamekaa wanacheza karata kwenye comptr zao wengine wako mtandaoni wanamsoma Mange,yaani ni headache jaribu kuulizia piga simu Temeke uliza kama wanapata mfumo,piga halmashauri za Pwani Kibaha huko ulizia kama wanapata!!!! Kuongoza hii nchi ni kazi mnooo kuliko unavyodhani lakini mda mwingine namwelewa rais wangu Magufuli
Itakuwa wewe ni operator wa Epicor...
Serikali inania njema kuanzisha hiyo mifumu...kuelekea kwenye e government Ila changamoto ni mapungufu ya mifumo yenyewe na mtandao haipo stable.
Mfano imprest kufutiks ni ishuuu....
PlanRep inatumika katika planning tu Ila reporting haitumiki, pia iaweza integrate na Epicor kujua expenditure ya vifungu lakini haitumiki hivyo tracking ya matumizi hufanywa manually kwenye mabatch.
Kifupi ni asilimia 35 -40 ya mifumo hutumika!
 
Mkuu sema una madai yamecheleweshwa basi, wakati mwingine watendaji tunawalaumu bure, wakulaumiwa ni TAMISEMI Dom ndiyo wanaoendesha Epicor na dada yao TTCL(network mbovu). Enough
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Pamoja na Magungufu ya Epicor Kila ofisi ya Serikali imefanya Kazi kwa mafanikio makubwa ukiacha Halmashauri Agency nyingi za Serikali zinatumia Epicor
 
Epicor inapigwa vita na watendaji wapiga dili, imewadhibiti, na ikitumika kwa ukamilifu serikali haitopoteza fedha hovyo. Tatizo la network ni TTCL ndio wasimamizi naona mleta mada una ajenda ya siri
 
Rais amezungukwa na genge la wanafiki wanaojivika ngozi ya mwanakondoo tena wengine kawaweka yeye washkaji zake matokeo yake mifumo na utendaji kazi unakua mbovu balaa,ntakupeni mfano mmoja tu sasa hivi halmashauri zote zina operate shughuli zake nyingi za kifedha kupitia mfumo wa epicor,lakini mfumo huu kwa wiki unaweza kua online mara mbili zaidi sana maea tatu siku zingine zooote mfumo unakua hauna network na unakuta watendaji wamekaa wanacheza karata kwenye comptr zao wengine wako mtandaoni wanamsoma Mange,yaani ni headache jaribu kuulizia piga simu Temeke uliza kama wanapata mfumo,piga halmashauri za Pwani Kibaha huko ulizia kama wanapata!!!! Kuongoza hii nchi ni kazi mnooo kuliko unavyodhani lakini mda mwingine namwelewa rais wangu Magufuli
TATIZO SIO MFUMO ; tatizo ni ISP INTERNET SERVICE PROVIDER ; Inaonyesha Halmashauri wanatumia Modem za simu.

wambie waende
RAHA COM
SIMBA NET
WIA
ZANTEL
TTCL

Wilaya Biharamulo wantumia epical tangu 2003 mpk leo wakajifunze halmashauri hizo
 
Issue ya network haisababishwi na epicor. Network ni miundombinu tu sasa inatakiwa hizo halmashauri iziimarishe network zao ili epicor ifanye kazi vizuri. Epicor inaweza kufanya kazi pasipokuwa na internet na pia zina licence ya web browser kupitia internet pia muache kuwarubuni wananchi
 
Back
Top Bottom