Mfumo wa Elimu na Biashara

Ramal Yazid

New Member
Feb 6, 2020
1
0
Habari zenu wana jamii. Natumai afya zenu ni salama.

Ninaomba msaada wenu wa mawazo na ushauri juu ya hili swala nililoliona kama ni changamoto iwakumbao makampuni mengi apa nchini kutokana na mfumo wetu wa Elimu jinsi ulivyo. Na kama ata wewe umeona ni tatizo tafadhali tujadili suluhisho ni nini. Na kama si tatizo toa maoni yako pia

Elimu yetu ya juu (ngazi ya chuo) ya biashara inafundisha kozi mbalimbali mfano. Businesss Administration, Accountant, Human Resource, Procurement and Logistic, Marketting and Sales na nyeninginezo.

Lakini tuzungumzie marketing and sales.

Marketing and Sales, ndio kiungo kinachopelekea kuendelea kuwepo, kukua na kufanikiwa kwa Biashara au Campuni. Marketing and sales ndio inatambulisha na kupeleka Bidhaa au Huduma sokoni na kutoa pesa sokoni kuingiza katika kampuni au biashara. Kozi zilizo bakia ni utendaji kazi tu.

Mfumo wetu wa elimu za kibiashara unachukua miaka 2 adi 3 kukamilika ili mhitimu aweze kua na uwezo kuisaidia kampuni kuperform kama inavyotakiwa na nyoongeza (bonus). Muda wa kuanza masomo kwa mwanafunzi mpka kumalizika, mengi yameshatokea na kubadilika sokoni (marketplace).

Pia mfumo wetu wa elimu hautegemei sana kufundisha katika mbinu na tecnic (strategies and technique) ambazo ziko tayara kutumika na biashara kwa sasa. Mfumowetu wa elimu unafundisha Basics (elimu ya ujumla kuusu kozi fulani). Na hii ni kwa sababu kubadilisha sylabas kila mwaka ni jambo ambalo aliwezekani kulingana na sababu zilikua nje ya uwezo wetu ama atufahamu. Lakini pia inafundisha elimu ya ujumla ama basics au general knowledge juu ya Marketing and sales laikini sio elimu husika kwa biashara husika (specific knowledge for specific industry/business).

Hili huwapa hali ngumu wahitimu kuweza kua na mbinu na tecnic husika ambazo zinafit biashara husika inapo itajika kwa sbabu mhitimu alikua na elimu ya jumla. Ndo maana miongoni mwa watu wengi husema "unachojifunza darasani sio ukikutacho kazini" hii huenda ikawa ni miongoni mwa sababu.

Makampuni mengi yanaangaika kuwapatia training mbalimbali hawa wahitimu muda tu watakapo ajiriwa au baadae baada ya kuajiriwa hii ni kwa ajili ya kuweza kufit na masoko au soko lilivo sasa. Lakini changamoto inakuja kwamba sio kila Market and sales training nisawa kwa kila kampuni. nao watoaji training wameshindwa pia kufanua hilo. Hivyo basi kama biashara zinatofautiana na training zitolewazo juu ya marketing and sales inabidi zitofautiane. Hapo ndipo tatizo linapo kuja.

Hakuna specific platfom ambayo inatoa ťraining juu ya marketing and sales kulingana na aina ya biashara au industry. Hakuna. Hio ndio maaana baadhi ya makampuni mengi hawafanyi training kwa wafanyakazi wao juu ya marketing and sales. Kwababu hakuna platfom sahihi inayotoa training juu ya hilo. Na hii pia ni miongoni mwa biashara nyingi zinazoanzishwa kufa. Sababu ni Marketing and sales, kujua kujitangaza na kuuza.

Biashana na makapuni mengi hukumbwa na hii changamoto. Na hili ni tatzo. Ndgu zangu wana jamii, kwa mtazamo wangu hili ni swala ambalo nililo kua nalifuatilia kwa muda sasa. Naomba tushirikiane kwa kujadili suluhisho la hili kusaidia mfumo wetu wa elimu kwan hauwezi kufanya yote kwa wakati mmoja.

images%20(5).jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom