Mfumo wa Ajira za Utumishi wa Umma inabidi ubadilike ili kufanikisha maendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfumo wa Ajira za Utumishi wa Umma inabidi ubadilike ili kufanikisha maendeleo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kpm, May 21, 2012.

 1. k

  kpm Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 57
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 15
  Mipango yote ya kiserikali inafanywa na wataalamu wa sekta husika (kama nishati,n.k) walioko wizarani. Lakini wengi wa wataalamu wetu wamepanda mpaka kufika vyeo vya juu kabisa bila ya kuwa na uelewa wa mambo halisi yalivyo katika fani hizo kwani huajiriwa baada ya kuhitimu masomo na kupandishwa vyeo serikalini kwa kufuata muda wa utumishi wa umma na mtandao ulio nao ndani ya wizara. Ni vizuri nafasi hizo zikawa zinatangazwa na kuombwa na watu wenye ujuzi (practical experience) kuliko kukaliwa na watu wenye utaalamu wa mezani tu! Ndio maana hakuna mipango madhubuti inayokamilika (mfano changamoto za nishati) kwa sababu inafanywa na watu wasiokuwa na uwezo halisi wa mambo. Ni muhimu tubadilishe mfumo.
   
 2. L

  Laizer Ole Naibio Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inaelekea wewe hujui tatizo la nchi yetu. Hayo usemayo si kweli hakuna mtu anapanda cheo bila ya kuwa na experience. Kimsingi watumishi wa Serikali wana ufahamu mkubwa sana wa mambo labda wanaangushwa na watu wachache icluding politicians. Mara nyingi ukiona mambo yaliyofanikiwa yametokana na ushauri wa Wataalamu hao. Hata akija mtu unayemwita wewe mtaalamu wa Sekta husika ni lazima ajifunze mambo yanavyokwenda kabla hajajua sekta hiyo ilivyo. Kuna changamoto nyingine katika utendaji wa kiserikali ukiwa ni pamoja na utaratibu wa malipo (Salary package) nk.
   
 3. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wizarani kuna section ambazo zina wataalam wa fani husika na utawala kama watu wa mipango na utawala. Kazi kubwa za wataalam ni kushauri kurugenzi husika na mkurugenzi kumshauri katibu mkuu. Katika section hizo kuna vyeo kuanzia assistant officer-officer-senior officer-principal officer- mkurugrnzi/kamishna. sehemu nyingi vyeo hupanda kutokana na uzoefu wako kazini, elimu na mchango wako. Kwa mfano principal ana uelewa mzuri wa sekta husika iwe maji, kilimo, madinink. Kwahiyo unavyosema wizarani hakuna watu wenye practical experience huo ni upotoshaji. Labda tuseme mfumo na ukiritimba pamoja na watu wachache kujinufaisha wenyewe ndio unachangia sekta nyingi kutoendelea.
   
Loading...