Ngoja nione kama huu mfano utaeleweka kwako....
Ni maelezo rahisi
Kwanza, tuna system A, tuiite Server A (Mf. Website ya chuo) ambayo inakutaka wewe client ulipie kiasi fulani cha fedha ili kuendelea na hatua zinazofata
Server A inakupa kumbukumbu namba ambayo ni namba ya kipekee/unique inayokutambulisha wewe,
(kila client atapewa kumbukumbu namba yake unique)
Kisha utatumia hii kumbukumbu namba kufanya malipo kwenye system B, tuiite Server B (Mobile money provider kama Mpesa etc)
Server B ita 'handle' mchakato mzima wa malipo,na kama mchakato utafanikiwa
Server B itazungumza na Server A(nyuma ya pazia) kuhusu malipo yaliyotoka kufanyika ikiwepo kiasi ulicholipa, kumbukumbu namba yako na taarifa nyingine zinazohitajika
Communication protocol inayoruhusu Servers tofauti kuzungumza inaitwa API
(Application programming interface)..
Ni namna tu ya programs mbili za computers kubadilishana taarifa bila kujali jinsi gani hizo programs zinafanyaje kazi (internally)
So program iliyoandikwa kwa C++ inaweza zungumza na program iliyoandikwa kwa Typescript na zikaelewana
Kwa kutumia taarifa ilizopata kutoka kwa server B (Muhimu zaidi kumbukumbu namba yako) Server A, itatambua kua mtumiaji mwenye kumbukumbu namba hii tayari ameshafanya malipo
Uki refresh page,Server A itaku ku redirect moja kwa moja kwenye step inayofata
Na kama inatumia web socket itafanya hii process automatically bila ya wewe ku reload the page..
Kuna namna nyingi za ku integrate mifumo ya malipo ila key concept ni API..
Cause always utahitaji mazungumzo kati ya code bases mbili tofauti